Kwanini mwaka ya Serikali (Julai - Juni) unatofautiana kwa mbali na mwaka wa kawaida wa kwenye kalenda (Januari - Desemba)? What's the logic behind?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kwanini mwaka ya serikali (July - June) unatofautiana sana na mwaka wa kawaida wa kwenye kalenda (January - December)? What's the logic behind?

Kwanini bajeti ya serikali sio ya kuanzia January mpaka December 2020 bali ni July 2019 mpaka June 2020?

What's the logic behind? Nini mantiki ya hii? Au ni maamuzi tu? Kama ni maamuzi tu kwanini mwaka hauanzi August 2019 mpaka July 2020?

Ninaomba ufafanuzi kutoka kwa wataalam wanaofahamu masuala haya. Karibuni sana wakuu.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Kwanini mwaka uanze January, na kwa nini iitwe January wala si jina lingine.

Kwanini Wakatoliki wadai Christmass ni tarehe 24 December na sio tarehe nyingine.
Kwanini Wachina, Wakorea, Waethiopia na wengine wawe na kalenda mbadala. Kwanini ziwepo Julian na Gregorian calendar kama common.

Maswali kama hilo na haya juu yanaendana ila ni kuwa ilitokea tu. Nadhani ni kutokana na misimu, December ni muda wa mwisho kuna harakati nyingi za kufunga mwaka si sawa kuweka muda wa kuandaa bajeti ya nchi inayotaka siku kadhaa. January ni muda wa kuanza mwaka watu wako busy na malengo.

Katikati ya mwaka ni muda muafaka kwa kupanga mpya, kukagua na kumalizia yaliyopangwa bajeti ilopita.
 
July - June ni mwaka wa kifedha (financial year/ fiscal year)na sio mwaka kwa kufuatana na kalenda (calender year). Kwa makampuni japo sio yote na serikali pia sio zote, mfano UK wanaanza April 1, inasaidia katika uwekaji kumbukumbu za kimahesabu ya biashara na kuyafunga mahesabu vilevile. Ni mchakato ambao , kwa mfano licha ya kuwa huo mwaka unaishia June 30, lakini kuna marekebisho mbalimbali mpaka kufikia kukamilisha kila kitu na pengine vikafika mpaka september ndio yakakamilika.

Kama umeshuhudia kwa Tz, kipindi hiki huwa watu wa serikali na makampuni huwa ni mikikimikiki ya kuweka mambo sawa, hivyo waliovumbua haya mambo, walitofautisha na kalenda ya kawaida ili kuepuka vurugu na shughuli za sherehe za mwisho na mwanzo wa mwaka, ambapo watu wengi wanapenda kuwa na familia zao.

Mahitaji ya kampuni husika, mfano kipindi cha mwisho wa mwaka ndio msimu wa biashara kuwa juu, hawawezi kukamilisha kila kitu, kukusanya mapato, kulipa madeni kwa wazabuni halafu kila kitu kikamilike December 31.
 
Ushafunga mjadala
 
Umefafanua vema mkuu
 
Back
Top Bottom