Kwanini Mungu hakurekebisha kilichosababisha shetani akaasi kabla ya kumuumba binadamu?

WATU wengi wangependa sana kupata jibu la swali hilo. Suala kuhusu sababu inayofanya Mungu aruhusu uovu uendelee linapotokea, watu hufikiria mara moja dhambi ya Adamu na Hawa katika bustani ya Edeni. Wazo la kwamba ‘Mungu anajua kila kitu’ linaweza kuwafanya wengine wafikie uamuzi kwamba lazima Mungu awe alijua mapema kuwa Adamu na Hawa wangekosa kumtii.

Ikiwa kwa kweli Mungu alijua mapema kuwa wanadamu hao wa kwanza ambao walikuwa wakamilifu wangefanya dhambi, hilo lingemaanisha nini?
Tuseme Mungu ambaye yeye mwenyewe ni upendo (siyo kwamba ana upendo)-Ni UPENDO angemuua shetani ili asidanganye-asieneze uongo wake-unadhani huo ungekuwa upendo au ukatili kwa Shetani.
Unadhani shetani yeye hahitaji upendo wa Mungu.
Kumbuka huko mbinguni kuna viumbe ambao wanamjua Mungu kama upendo. Halafu ghafla tu anaangamiza au kumfutilia mbali shetani.
Ametoa nafasi viumbe wote waone ubaya wa shetani ili siku akimuangamiza, itaeleweka
Jambo kama hilo lingeonyesha kuwa Mungu ana sifa nyingi mbaya. Watu wangemwona kuwa Mungu asiye na upendo, haki, na unyofu. Wengine wangesema kuwa Mungu alitenda kwa ukatili kuwaweka wanadamu wa kwanza katika hali ambayo tayari alijua ingekuwa na matokeo mabaya. Huenda ikaonekana kuwa Mungu analaumika kwa kusababisha—au kwa kushiriki kusababisha—uovu na mateso yote ambayo yametokea katika historia. Kwa wengine, Muumba wetu hata angeonekana mpumbavu.

Je, Biblia inaonyesha kuwa Yehova Mungu ana sifa mbaya kama hizo? Ili kujibu swali hilo, acheni tuchunguze yale ambayo Biblia inasema kuhusu kazi za Yehova za uumbaji na sifa zake.

“Kilikuwa Chema Sana”

Kuhusu uumbaji wa Mungu, kutia ndani wanadamu wa kwanza duniani, simulizi la kitabu cha Mwanzo linasema: “Mungu akaona kila kitu alichokuwa amefanya na, tazama! kilikuwa chema sana.” (Mwanzo 1:31) Adamu na Hawa walikuwa wakamilifu, wakiwa wameumbwa wafaane kabisa na mazingira ya dunia. Hawakuwa na kasoro yoyote. Kwa kuwa waliumbwa wakiwa ‘wema sana,’ bila shaka walikuwa na uwezo wa kujiendesha vizuri kama walivyotakiwa kufanya. Waliumbwa “kwa mfano wa Mungu.” (Mwanzo 1:27) Kwa hiyo, walikuwa na uwezo wa kuonyesha kwa kiasi fulani sifa za Mungu kama vile hekima, upendo mshikamanifu, haki, na wema. Kuwa na sifa kama hizo kungewasaidia kufanya maamuzi ambayo yangewanufaisha na kumfurahisha Baba yao wa mbinguni.

Yehova aliwapa viumbe hao wakamilifu na wenye akili uhuru wa kuchagua. Kwa hiyo, hawakuwa kama mashini, yaani, wamepangiwa kufanya tu yale yanayompendeza Mungu. Hebu fikiria jambo hilo. Ungethamini zawadi gani—ile ambayo mtu anakupa kutimiza wajibu tu au ile ambayo anakupa kutoka moyoni? Jibu ni wazi. Vivyo hivyo, kama Adamu na Hawa wangechagua kumtii Mungu kwa hiari, Mungu angethamini sana utii wao. Uwezo wao wa kuchagua ungewawezesha Adamu na Hawa kumtii Yehova kwa sababu wanampenda.—Kumbukumbu la Torati 30:19, 20.

Mwadilifu, Mwenye Haki, na Mwema

Biblia inatufunulia sifa za Yehova. Sifa hizo zinaonyesha kuwa Mungu hawezi kuhusianishwa na dhambi kwa vyovyote. Yehova “anapenda uadilifu na haki,” linasema andiko la Zaburi 33:5. Hivyo, andiko la Yakobo 1:13 linasema: “Mungu hawezi kujaribiwa na mambo maovu wala yeye mwenyewe hamjaribu yeyote.” Kwa kuwa Mungu ni mwenye haki na alimjali Adamu, alimwonya hivi: “Matunda ya kila mti wa bustani unaweza kula mpaka ushibe. Lakini kuhusu matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula, utakufa hakika.” (Mwanzo 2:16, 17) Adamu na Hawa walipewa uhuru wa kuchagua kati ya uzima wa milele na kifo. Je, Mungu hangekuwa mnafiki kuwaonya kuhusu dhambi fulani hususa, huku tayari akijua kwamba wangeifanya na matokeo yawe mabaya? Bila shaka, Yehova ambaye “anapenda uadilifu na haki,” hangewapa uhuru wa kuchagua huku akijua kuwa hapakuwa na uhuru kama huo.

Pia, wema wa Yehova ni mwingi. (Zaburi 31:19) Yesu alielezea wema wa Mungu hivi: “Ni nani kati yenu ambaye mwana wake akimwomba mkate—je, atampa jiwe? Au, labda, akiomba samaki—je, atampa nyoka? Kwa hiyo, ikiwa ninyi, mjapokuwa waovu, mnajua jinsi ya kuwapa watoto wenu zawadi zilizo nzuri, je, Baba yenu aliye mbinguni hatawapa hata zaidi vitu vyema wale wanaomwomba?” (Mathayo 7:9-11) Mungu anawapa viumbe wake “vitu vyema.” Wema wa Mungu unathibitishwa kupitia jinsi alivyowaumba wanadamu na alivyowatayarishia makao ya Paradiso. Je, hungekuwa ukatili kwa Mtawala mwema kama huyo kuwaandalia wanadamu makao mazuri kama hayo huku tayari akijua hawangeishi humo? Hapana. Muumba wetu mwadilifu na mwema hawezi kulaumiwa kwa uasi wa mwanadamu.

“Mwenye Hekima Peke Yake”

Maandiko pia yanaonyesha kuwa Yehova ndiye “mwenye hekima peke yake.” (Waroma 16:27) Malaika wa mbinguni wa Mungu walishuhudia mambo mengi yanayothibitisha kuwa hekima ya Mungu haina kifani. Walianza ‘kupiga vigelegele pamoja kwa shangwe’ wakati Yehova alipotokeza uumbaji wake duniani. (Ayubu 38:4-7) Bila shaka, malaika hao ambao ni viumbe wa roho wenye akili, walifuatilia kwa makini sana matukio katika bustani ya Edeni. Hivyo basi, je, lingekuwa jambo linalopatana na akili kwa Mungu mwenye hekima kuumba ulimwengu wenye kustaajabisha na vitu vingi vyenye kuvutia duniani, kisha aumbe viumbe wengine wawili wa kipekee mbele ya macho ya malaika zake huku akijua kuwa wangeshindwa kumtii? Kwa kweli, ni jambo lisilopatana na akili kabisa kupanga msiba kama huo.

Hata hivyo, mtu anaweza kuuliza, ‘Inawezekana jinsi gani kwa Mungu mwenye hekima yote akose kujua?’ Ni kweli kwamba katika hekima yake nyingi, Yehova ana uwezo wa kujua “tangu mwanzo ule mwisho.” (Isaya 46:9, 10) Ingawa hivyo, si lazima atumie uwezo huo, kama vile tu si lazima nyakati zote atumie kikamili nguvu zake nyingi. Kwa hekima, Yehova anachagua wakati wa kutumia uwezo wake wa kujua mambo mapema. Anautumia katika hali na wakati inapofaa kufanya hivyo.

Uwezo wa kuchagua kutojua jambo fulani mapema unaweza kulinganishwa na jinsi mtu anavyoweza kuamua kutumia kifaa fulani cha kitekinolojia. Kwa mfano, mtu anayetazama shindano la mchezo fulani lililorekodiwa mapema ana uwezo wa kuchagua kutazama kwanza dakika za mwisho za shindano hilo ili ajue matokeo yake. Lakini si lazima atazame sehemu hiyo ya mwisho kwanza. Ni nani ambaye angemlaumu kama angeamua kutazama shindano lote kuanzia mwanzo? Vivyo hivyo, Muumba alichagua kutotazama jinsi ambavyo matukio ya mwisho yangekuwa. Badala yake, alichagua kungoja, na kulingana na jinsi ambavyo hali zingekuwa, aone watoto wake wa kidunia wangejiendesha jinsi gani.

Kama ilivyotajwa mwanzoni, katika hekima yake Yehova hakuwaumba wanadamu wa kwanza wakiwa kama mashini inayofanya tu mambo ambayo imepangiwa kufanya. Badala yake, kwa upendo aliwapa uhuru wa kuchagua. Kwa kufanya uchaguzi unaofaa, wangeweza kuonyesha upendo, shukrani, na utii wao, na hivyo wangekuwa wenye furaha zaidi na pia wangemfurahisha Yehova, Baba yao wa mbinguni.—Methali 27:11; Isaya 48:18.

Maandiko yanaonyesha kuwa mara nyingi Mungu alichagua kutotumia uwezo wake wa kujua mambo mapema. Kwa mfano, wakati Abrahamu mwaminifu alipokuwa karibu kumtoa mwana wake kama dhabihu, Yehova alisema: “Sasa mimi najua kwamba wewe unamwogopa Mungu kwa kuwa hukunizuilia mwana wako, mwana wako wa pekee.” (Mwanzo 22:12) Pia, nyakati nyingine mwenendo mbaya wa watu fulani ulifanya Mungu ‘ahuzunike.’ Je, angehisi uchungu kama huo kama angalikuwa amejua mapema matendo yao?—Zaburi 78:40, 41; 1 Wafalme 11:9, 10.

Hivyo, ni jambo linalopatana na akili kusema kwamba Mungu mwenye hekima yote hakutumia uwezo wake wa kujua mambo mapema ili ajue kimbele kama wazazi wetu wa kwanza wangefanya dhambi. Hakuwaumba wanadamu kusudi tu wafanye mambo fulani ya ajabu huku tayari akijua wangeyafanya kwa kuwa ana uwezo wa kujua mambo mapema. Huo ungekuwa upumbavu.

“Mungu Ni Upendo”

Shetani, adui wa Mungu, alianzisha uasi huko Edeni. Uasi huo ulikuwa na matokeo mabaya, kutia ndani dhambi na kifo. Hivyo, Shetani alikuwa “muuaji.” Pia, alithibitika kuwa ‘mwongo na baba ya uwongo.’ (Yohana 8:44) Kwa kuchochewa na nia mbaya, Shetani anajitahidi kuonyesha kuwa Muumba wetu mwenye upendo hana nia nzuri. Angependa ionekane kuwa Yehova ndiye wa kulaumiwa kwa dhambi ya mwanadamu.

Sifa ya upendo ya Yehova ndiyo sababu kuu iliyomfanya achague kutojua mapema kwamba Adamu na Hawa wangefanya dhambi. Upendo ndiyo sifa kuu ya Mungu. “Mungu ni upendo,” linasema andiko la 1 Yohana 4:8. Upendo unatazamia mema, bali si mabaya. Unatafuta sifa nzuri za wengine. Ndiyo, akiongozwa na upendo, Yehova Mungu alitaka wanadamu wawili wa kwanza wafurahie maisha.

Ingawa watoto wa Mungu wa kidunia wangeweza kufanya uamuzi usiofaa, Mungu wetu mwenye upendo hakuwa na matazamio yasiyofaa wala hakuwa na shaka kuhusu viumbe hao wakamilifu. Aliwaandalia vyote walivyohitaji na kuwaeleza yote waliyohitaji kujua. Hivyo, Mungu alikuwa na haki ya kutazamia utii wenye upendo, bali si uasi. Alijua kuwa Adamu na Hawa walikuwa na uwezo wa kutenda kwa ushikamanifu, kama ilivyothibitishwa baadaye na wanaume wasio wakamilifu, kama vile Abrahamu, Ayubu, Danieli, na wengine wengi.

Yesu alisema, “Kwa Mungu mambo yote yanawezekana.” (Mathayo 19:26) Hilo linafariji. Kwa sababu ya upendo wa Yehova, kutia ndani sifa zake nyingine kuu ambazo ni haki, hekima, na nguvu, tuna hakika kwamba katika wakati ufaao anaweza na ataondoa mambo yote mabaya yanayotokana na dhambi na kifo.—Ufunuo 21:3-5.
Watu wa jumba la ufalme
 
Habari ya jumapili.

Dini inasema shetani aliasi huko juu mbunguni mahala palipotukuka na palipoinuka juu anapoishi mungu. Baada ya shetani kuasi mungu akamtimua na kumshusha huku Duniani.

Dini inasema baadae mungu akamuumba mwanadamu na kumuweka Duniani, maana yake mwanadamu alipowekwa duniani tayari shetani alikua duniani muda mrefu tu anakula zake maisha.

Hadithi ya shetani kuasi iko one sided, yaani inaelezwa kutoka upande wa mungu, hakuna aliewahi kusikia upande wa shetani(tayari binadam wanamshutumu shetani kwa habari ya kuambiwa, one sided story, hivyo shetani anahukumiwa kua ni mbaya bila kusikilizwa).

Dini haisemi kwa nini shetani aliasi na ilikuaje akaasi. Dini inasema mungu anajua kila kitu, all knowing lakini haisemi mungu alishindwaje kujua kua shetani atakuja kuasi ili asimuumbe. Na kama alijua shetani atakuja kuasi kwa nini alimuacha aasi. Mbaya zaidi huo mgogoro wao umetuingiza na sisi binadam ambao hatujui chanzo cha mgogoro. Yaani mungu anarecruit binadam washirikiane nae mwenye mgogoro wake na shetani huku binadam hawajui chanzo cha mgogoro wao. Na mungu anatishia kua yoyote ambae hatashirikiana nae kwenye mgogoro huo atampanish vikali. Unajiuliza hakuaje involved kwenye mgogoro nisioujua chanzo chake na natishiwa adhabu kali kama sitashiriki huo mgogoro ambao in fact haupo kwa sababu mungu hajaonyesha kuwepo, hivyo watu waoga na wajinga wanalazimika kushiriki mgogoro blindly ili kuogopa adhabu.

Kama mungu anawapenda wanadamu kama dini inavyosema alipaswa kurekebisha kasoro zilizojitokeza kabla ya kumuumba mwanadam, lakini pia alipaswa kujua in the first hand kua shetani atakuja kuasi kabla hajamuumba, vinginevyo hajui kila kitu kinyume na inavyosemekana kua anajua kila kitu.

Tukubali tukatae, maovu yote duniani kama mauaji, wivu, kifo, husda, wizi, matetemeko ya ardhi, tsunami, vimbunga, ukame, magonjwa yote chanzo chake ni mungu. Mungu ameshindwa kabisa kutuonyesha kua kweli anatupenda kama anavyosemwa, ameshindwa kuonyesha kweli kua anajali Mbaya zaidi ameyatengeneza alafu ameshindwa kuyaondoa.

Hii mada inaendelea.

Nyongeza ya mjumbe.
Katika mtazamo mpana, sisi binadamu na shetani ni viumbe wa Mungu. Mungu ni upendo. Kwa mazamo wetu shetani alipaswa akatiliwe mbali maramoja baada ya kuasi. Kumbuka na yeye ni kiumbe wa Mungu, Mungu mwenye upendo

Je mnadhani shetani hastahili huo upendo?. Kumbuka kuna viumbe wengine mbinguni-malaika-they are watching-wanaangalia huyo Mungu mwenye upendo anafanyaje.
Je Mungu angemkatilia mbali shetani mara tu alivyoonyesha uasi, ingekuwa sawa.
Hawa viumbe wengine wangemuona Mungu tena kama ni Upendo au ni mwenye upendo? la hasha. Angeonekana mkatili

Hivyo ilipaswa shetani aachwe madhara ya uasi wake yaonekane dhahiri kwa Viumbe wengine ili atakaposhughulikiwa isionekane kuwa kaonewa
Kwa sasa niishie hapo
 
hatuelewi mambo mengi sana kuhusu Mungu lakini kilicho wazi ni kuwa Mungu ana process yake. Yawezekana sana hao malaika na viumbe wengine wanafahamu jinsi Mungu anavyotoa uhuru wa kila kiumbe kumsikiliza au kuchagua ustaarabu wake. ukichagua kuchukua ustaarabu wako uko tofauti na Mungu na akikuwakia huku kila siku anakwambia acha hiki acha kile husikii anayo haki. huyo shetani alishakanywa sana na Mungu kuwa acha hiyo tabia yeye akasema sawa lakini hakuacha mpaka alipofikia hatua ya kusema mimi ni kama wewe Mungu tu na nnaweza kuwa kama wewe. Ndo la kwanza akamuondoa huko mbinguni.

kabla ya hapo shetani aliwaconvince theluthi ya malaika nao wakawa waasi. hivyo alivyotolewa na hawa wakatolewa. kuanzia hapo Mungu akataka huko aliko atubu asamehewe lakini akakataa. Mungu akamuumba mtu kwa utaratibu ule ule wa kumsikiliza bila kulazimishwa akamwambia kitu kirahisi sana kuwa usile tunda lile maana ukilila utakufa. akaja shetani akamdanganya mtu kuwa Mungu ni dikteta anajua ukila utakuwa kama yeye. mtu akamwamini shetani zaidi akachukua tunda akalila na hapo hapo ndipo akagundua kuwa yuko uchi wakati hata kabla ya kula tunda alikuwa hana nguo. sasa kitendo hicho kikamkasirisha sana Mungu ingawa hakufunga mlango wa kumsamehe shetani.

sasa anamsubiri aombe msamaha shetani anakaza. mwisho ili dhambi ya uasi wa shetani iondolewa moja kwa moja ikawa lazima kafara ya binadamu Yesu itolewe kuondoa dhambi kabisa na kuhamisha dhambi yote kwa shetani. hivi sasa Mungu anasubiri muda wake tu ili amfutilie mbali shetani. kwa wakati huu anamwita kila mtu atubu, amwamini Mungu na kuunganishwa naye. hili litaendelea mpaka miaka kadhaa hapo mbele au mpaka mtu anapokufa baada ya hapo Mungu atamfutilia mbali shetani na wote waliomfuata.

ni kweli Mungu ana upendo lakini huwa hataki kuiacha dhambi idumu milele. huwa anaifutilia mbali na wale wasiotaka kuitubu na kuiacha. huyu shetani aligoma kuiacha hivyo ataibeba dhambi yote aliyoifanya na aliyowasababisha wengine waifanye. kwa hiyo kwa kiasi fulani uko sawa anataka ionekane alivyo wa haki kwa sheria yake mwenyewe bila kumwonea mtu.
 
hatuelewi mambo mengi sana kuhusu Mungu lakini kilicho wazi ni kuwa Mungu ana process yake. Yawezekana sana hao malaika na viumbe wengine wanafahamu jinsi Mungu anavyotoa uhuru wa kila kiumbe kumsikiliza au kuchagua ustaarabu wake. ukichagua kuchukua ustaarabu wako uko tofauti na Mungu na akikuwakia huku kila siku anakwambia acha hiki acha kile husikii anayo haki. huyo shetani alishakanywa sana na Mungu kuwa acha hiyo tabia yeye akasema sawa lakini hakuacha mpaka alipofikia hatua ya kusema mimi ni kama wewe Mungu tu na nnaweza kuwa kama wewe. Ndo la kwanza akamuondoa huko mbinguni. kabla ya hapo shetani aliwaconvince theluthi ya malaika nao wakawa waasi. hivyo alivyotolewa na hawa wakatolewa. kuanzia hapo Mungu akataka huko aliko atubu asamehewe lakini akakataa. Mungu akamuumba mtu kwa utaratibu ule ule wa kumsikiliza bila kulazimishwa akamwambia kitu kirahisi sana kuwa usile tunda lile maana ukilila utakufa. akaja shetani akamdanganya mtu kuwa Mungu ni dikteta anajua ukila utakuwa kama yeye. mtu akamwamini shetani zaidi akachukua tunda akalila na hapo hapo ndipo akagundua kuwa yuko uchi wakati hata kabla ya kula tunda alikuwa hana nguo. sasa kitendo hicho kikamkasirisha sana Mungu ingawa hakufunga mlango wa kumsamehe shetani. sasa anamsubiri aombe msamaha shetani anakaza. mwisho ili dhambi ya uasi wa shetani iondolewa moja kwa moja ikawa lazima kafara ya binadamu Yesu itolewe kuondoa dhambi kabisa na kuhamisha dhambi yote kwa shetani. hivi sasa Mungu anasubiri muda wake tu ili amfutilie mbali shetani. kwa wakati huu anamwita kila mtu atubu, amwamini Mungu na kuunganishwa naye. hili litaendelea mpaka miaka kadhaa hapo mbele au mpaka mtu anapokufa baada ya hapo Mungu atamfutilia mbali shetani na wote waliomfuata.
ni kweli Mungu ana upendo lakini huwa hataki kuiacha dhambi idumu milele. huwa anaifutilia mbali na wale wasiotaka kuitubu na kuiacha. huyu shetani aligoma kuiacha hivyo ataibeba dhambi yote aliyoifanya na aliyowasababisha wengine waifanye. kwa hiyo kwa kiasi fulani uko sawa anataka ionekane alivyo wa haki kwa sheria yake mwenyewe bila kumwonea mtu.
Ubarikiwe mkuu. Tumpokee Yesu awe mwokozi wetu
 
Msamaha unatolewa kwa aliyefanya kosa kisha akaomba msamaha. Lakini adhabu hutolewa kwa aliyefanya kosa kisha akakaidi kuomba msamaha. Ibilisi aliasi na hajakubali kwamba alilolifanya ni kosa na khatima yake alitolewa kwenye rehema ya Mungu. Vilevile Adam aliasi kwa kutotii amri ya Mungu ya kutokula kutokana na mti waliyokatazwa hata kutoukaribia, lakini waliomba msamaha na wakasamehewa lakini walitolewa katika ile bustani ambayo waliyokuwa wakikaa kwa raha na bila ya mashaka na tabu.
wakatolewa edeni
Mwanaume atakula kwa jasho
Mwananke atazaa kwa uchungu
Na kila atokae kwenye tumbo LA mwanamke siku zake hapa duniani si nyingi
Msamaha apo uko wapi naomba maelezo tafadhari
 
"Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika checmchem yenye matope meusi" hiyo ni tafsiri ya Quran 18:86, nani aliyeona jua linatua katika chemchem yenye matope meusi? Je ni kweli Mungu anasema ya kuwa jua linazama kwenye matope meusi?
kiarab hapo kimetumia neno 'wajadaha' akalikuta linatua kwenye matope..Sasa hapo mungu anaturipotia kuwa alipofika sehemu ambayo jua huzama alikuta linazama kwenye matope..kuna matatizo mawili apo
1.Hakuna sehem ambayo Jua huzama ambayo unaweza ukaifikia...2.Muhamad anatuhabarisha kuwa alipofika hiyo sehemu alilikuta linazama kwenye matope wala sio kwamba aliliona kama linazama kwenye matope kama ambavyo wewe na watafsiri baadhi baada ya kusoma sayansi darasa la tatu mnabadili maana..Au tuangalie hadith zinalizungumziaje hili au unaogopa?.
Ile picha yako iliyokuwa imeandikwa maneno ya kipuuzi ulikuwa una maanisha nini? (refer to your post #1230)
inaelezea alichoelezea Allah kwenye Quran.
Mungu anajiamini sana kwa upekee wake, ndiyo maana kama ukisoma Qurani huo uwingi anautumia katika kuonyesha utukufu wake kwa kusema "SISI" na mwanadamu ukiona sentensi inayosema sisi basi lazima uzingatie ujumbe wake.
kama anajiamini katika upekee wake na umoja wake..kwanini atumie wingi kama njia ya kuonesha utukufu??kumbe utukufu upo katika wingi sio umoja wake?
 
Habari ya jumapili.

Dini inasema shetani aliasi huko juu mbunguni mahala palipotukuka na palipoinuka juu anapoishi mungu. Baada ya shetani kuasi mungu akamtimua na kumshusha huku Duniani.

Dini inasema baadae mungu akamuumba mwanadamu na kumuweka Duniani, maana yake mwanadamu alipowekwa duniani tayari shetani alikua duniani muda mrefu tu anakula zake maisha.

Hadithi ya shetani kuasi iko one sided, yaani inaelezwa kutoka upande wa mungu, hakuna aliewahi kusikia upande wa shetani(tayari binadam wanamshutumu shetani kwa habari ya kuambiwa, one sided story, hivyo shetani anahukumiwa kua ni mbaya bila kusikilizwa).

Dini haisemi kwa nini shetani aliasi na ilikuaje akaasi. Dini inasema mungu anajua kila kitu, all knowing lakini haisemi mungu alishindwaje kujua kua shetani atakuja kuasi ili asimuumbe. Na kama alijua shetani atakuja kuasi kwa nini alimuacha aasi. Mbaya zaidi huo mgogoro wao umetuingiza na sisi binadam ambao hatujui chanzo cha mgogoro. Yaani mungu anarecruit binadam washirikiane nae mwenye mgogoro wake na shetani huku binadam hawajui chanzo cha mgogoro wao. Na mungu anatishia kua yoyote ambae hatashirikiana nae kwenye mgogoro huo atampanish vikali. Unajiuliza hakuaje involved kwenye mgogoro nisioujua chanzo chake na natishiwa adhabu kali kama sitashiriki huo mgogoro ambao in fact haupo kwa sababu mungu hajaonyesha kuwepo, hivyo watu waoga na wajinga wanalazimika kushiriki mgogoro blindly ili kuogopa adhabu.

Kama mungu anawapenda wanadamu kama dini inavyosema alipaswa kurekebisha kasoro zilizojitokeza kabla ya kumuumba mwanadam, lakini pia alipaswa kujua in the first hand kua shetani atakuja kuasi kabla hajamuumba, vinginevyo hajui kila kitu kinyume na inavyosemekana kua anajua kila kitu.

Tukubali tukatae, maovu yote duniani kama mauaji, wivu, kifo, husda, wizi, matetemeko ya ardhi, tsunami, vimbunga, ukame, magonjwa yote chanzo chake ni mungu. Mungu ameshindwa kabisa kutuonyesha kua kweli anatupenda kama anavyosemwa, ameshindwa kuonyesha kweli kua anajali Mbaya zaidi ameyatengeneza alafu ameshindwa kuyaondoa.

Hii mada inaendelea.

Nyongeza ya mjumbe.
Nikweli kabisa kuna Nguvu inayoitawala dunia, lakini ni tofauti na tunavyoelezwa! Hii yote ni kwa7 dini zimeletwa toka ughaibuni na haziendani na chimbuko la asili ya wafrika na iman zao na tamaduni za kale kabisa!! Hivyo vitabu ni collection za stories(imaginary na zingine za uhalisia wa kihistoria) na hekima za watu wa mashariki ya kati. Ndo maana wachina wana abudu kivyao, wahindu pia, tena hawaamini hayo masuala ya jehanam ,peponi N.k, .

Tulichokosea sisi waafrika ni kuacha tamaduni na imani zetu na kufuata hizo dini za kigeni ambazo hazifit na historia yetu!! Yaan uongo mwingi mno na vitisho(amri)
 
wakatolewa edeni
Mwanaume atakula kwa jasho
Mwananke atazaa kwa uchungu
Na kila atokae kwenye tumbo LA mwanamke siku zake hapa duniani si nyingi
Msamaha apo uko wapi naomba maelezo tafadhari
Ngoja tupate habari ya Adam na Hawa jinsi walivyotolewa kwenye bustani kutoka kwenye Quran 2:35-39 :-
35. Na tulisema: Ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani, na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu tu; mkawa katika wale walio dhulumu.
36. Lakini Shet'ani aliwatelezesha hao wawili na akawatoa katika waliyo kuwamo, na tukasema: Shukeni, nanyi ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Katika ardhi yatakuwa makaazi yenu na starehe kwa muda.
37. Kisha Adam akapokea maneno kwa Mola wake Mlezi, na Mola wake Mlezi alimkubalia toba yake; hakika Yeye ndiye Mwingi wa kukubali toba na Mwenye kurehemu.
38. Tukasema: Shukeni nyote; na kama ukikufikieni uwongofu utokao kwangu, basi watakao fuata uwongofu wangu huo haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika.
39. Na wenye kukufuru na kuzikanusha ishara zetu, hao ndio watakao kuwa watu wa Motoni, humo watadumu.
 
Habari ya jumapili.

Dini inasema shetani aliasi huko juu mbunguni mahala palipotukuka na palipoinuka juu anapoishi mungu. Baada ya shetani kuasi mungu akamtimua na kumshusha huku Duniani.

Dini inasema baadae mungu akamuumba mwanadamu na kumuweka Duniani, maana yake mwanadamu alipowekwa duniani tayari shetani alikua duniani muda mrefu tu anakula zake maisha.

Hadithi ya shetani kuasi iko one sided, yaani inaelezwa kutoka upande wa mungu, hakuna aliewahi kusikia upande wa shetani(tayari binadam wanamshutumu shetani kwa habari ya kuambiwa, one sided story, hivyo shetani anahukumiwa kua ni mbaya bila kusikilizwa).

Dini haisemi kwa nini shetani aliasi na ilikuaje akaasi. Dini inasema mungu anajua kila kitu, all knowing lakini haisemi mungu alishindwaje kujua kua shetani atakuja kuasi ili asimuumbe. Na kama alijua shetani atakuja kuasi kwa nini alimuacha aasi. Mbaya zaidi huo mgogoro wao umetuingiza na sisi binadam ambao hatujui chanzo cha mgogoro. Yaani mungu anarecruit binadam washirikiane nae mwenye mgogoro wake na shetani huku binadam hawajui chanzo cha mgogoro wao. Na mungu anatishia kua yoyote ambae hatashirikiana nae kwenye mgogoro huo atampanish vikali. Unajiuliza hakuaje involved kwenye mgogoro nisioujua chanzo chake na natishiwa adhabu kali kama sitashiriki huo mgogoro ambao in fact haupo kwa sababu mungu hajaonyesha kuwepo, hivyo watu waoga na wajinga wanalazimika kushiriki mgogoro blindly ili kuogopa adhabu.

Kama mungu anawapenda wanadamu kama dini inavyosema alipaswa kurekebisha kasoro zilizojitokeza kabla ya kumuumba mwanadam, lakini pia alipaswa kujua in the first hand kua shetani atakuja kuasi kabla hajamuumba, vinginevyo hajui kila kitu kinyume na inavyosemekana kua anajua kila kitu.

Tukubali tukatae, maovu yote duniani kama mauaji, wivu, kifo, husda, wizi, matetemeko ya ardhi, tsunami, vimbunga, ukame, magonjwa yote chanzo chake ni mungu. Mungu ameshindwa kabisa kutuonyesha kua kweli anatupenda kama anavyosemwa, ameshindwa kuonyesha kweli kua anajali Mbaya zaidi ameyatengeneza alafu ameshindwa kuyaondoa.

Hii mada inaendelea.

Nyongeza ya mjumbe.

Ndugu Hakimu Mfawidhi unaonekana weye ni jahil wa hali ya juu na humu ndani una majihil wenzako kama weye na unaonekana hukusoma wala hujui dini yako sijui ni muislamu au mkristo unaonekana huyo shetani unaemsema sasa amekuingia vyema .Allah ktk Sura Adh-Dhariyat(The Winds that Scatter) aya ya 56 .Mimi sikuumba majini na binadamu ila kwa kuniabudu mimi.

Sitaki nikushoshe sana kwa hoja lkn weye pamoja na wenzako kama weye wenye akili finyu NAKUOMBA USOMEEE.Hizi hoja jako ulizoandika ni za kijinga kabisa hazina mashiko.Soma soma soma.
 
Ndugu Hakimu Mfawidhi unaonekana weye ni jahil wa hali ya juu na humu ndani una majihil wenzako kama weye na unaonekana hukusoma wala hujui dini yako sijui ni muislamu au mkristo unaonekana huyo shetani unaemsema sasa amekuingia vyema .Allah ktk Sura Adh-Dhariyat(The Winds that Scatter) aya ya 56 .Mimi sikuumba majini na binadamu ila kwa kuniabudu mimi. Sitaki nikushoshe sana kwa hoja lkn weye pamoja na wenzako kama weye wenye akili finyu NAKUOMBA USOMEEE.Hizi hoja jako ulizoandika ni za kijinga kabisa hazina mashiko.Soma soma soma.
Sasa umeandika nini mkuu?

Rudi shule uongeze maarifa.
 
Huenda dini inadumaza akili ya binadamu! Binadamu akaamini kulikuwa na vita mbinguni na shetani akatupwa ulimwenguni!! Mungu angemsamehe kuliko kutushushia huo mzigo na anajua akili zetu ni ndogo.
 
Habari ya jumapili.

Dini inasema shetani aliasi huko juu mbunguni mahala palipotukuka na palipoinuka juu anapoishi mungu. Baada ya shetani kuasi mungu akamtimua na kumshusha huku Duniani.

Dini inasema baadae mungu akamuumba mwanadamu na kumuweka Duniani, maana yake mwanadamu alipowekwa duniani tayari shetani alikua duniani muda mrefu tu anakula zake maisha.

Hadithi ya shetani kuasi iko one sided, yaani inaelezwa kutoka upande wa mungu, hakuna aliewahi kusikia upande wa shetani(tayari binadam wanamshutumu shetani kwa habari ya kuambiwa, one sided story, hivyo shetani anahukumiwa kua ni mbaya bila kusikilizwa).

Dini haisemi kwa nini shetani aliasi na ilikuaje akaasi. Dini inasema mungu anajua kila kitu, all knowing lakini haisemi mungu alishindwaje kujua kua shetani atakuja kuasi ili asimuumbe. Na kama alijua shetani atakuja kuasi kwa nini alimuacha aasi. Mbaya zaidi huo mgogoro wao umetuingiza na sisi binadam ambao hatujui chanzo cha mgogoro. Yaani mungu anarecruit binadam washirikiane nae mwenye mgogoro wake na shetani huku binadam hawajui chanzo cha mgogoro wao. Na mungu anatishia kua yoyote ambae hatashirikiana nae kwenye mgogoro huo atampanish vikali. Unajiuliza hakuaje involved kwenye mgogoro nisioujua chanzo chake na natishiwa adhabu kali kama sitashiriki huo mgogoro ambao in fact haupo kwa sababu mungu hajaonyesha kuwepo, hivyo watu waoga na wajinga wanalazimika kushiriki mgogoro blindly ili kuogopa adhabu.

Kama Mungu anawapenda wanadamu kama dini inavyosema alipaswa kurekebisha kasoro zilizojitokeza kabla ya kumuumba mwanadam, lakini pia alipaswa kujua in the first hand kua shetani atakuja kuasi kabla hajamuumba, vinginevyo hajui kila kitu kinyume na inavyosemekana kua anajua kila kitu.

Tukubali tukatae, maovu yote duniani kama mauaji, wivu, kifo, husda, wizi, matetemeko ya ardhi, tsunami, vimbunga, ukame, magonjwa yote chanzo chake ni mungu. Mungu ameshindwa kabisa kutuonyesha kua kweli anatupenda kama anavyosemwa, ameshindwa kuonyesha kweli kua anajali Mbaya zaidi ameyatengeneza alafu ameshindwa kuyaondoa.

Hii mada inaendelea.

Nyongeza ya mjumbe.
Kwanza unakosea mno kuandika neno mungu ukimaanisha Mungu. Hilo ni kosa kuu mno maana linaharibu maana yako nzima.

Pili, inabidi usome vitabu vya dini vizuri, ili uelewe kwanini mgogoro uliopo wa Mungu na shetani unamuingizaje mwanadamu.

Tatu, unamkosoa Mungu kwa jambo ambalo haulifahamu vizuri, na sidhani kama umedhamiria kufahamu mengi zaidi.

Nne, vitabu vya dini vimeelezea kila kitu, ingawa kwa ufupi mno, kwanini shetani alitokea, tangu enzi za mwanadamu wa kwanza, hadi kipindi cha Adamu na Hawa, mpaka kufukuzwa edeni na mambo ya Kizazi cha kaini.

Soma vizuri, biblia utapata majibu ya maswali yako.

Pia, sio kila jambo Mungu alilijua kabla kuwa Malaika atakosea, la hasha. Ndio maana zipo adhabu zinatolewa kwa kila kiumbe. Mf. Majabali na majitu enzi za nuhu.

Hata shetani kuasi kwake kuna sababu kubwa inayotokana na mwanadamu, na ndio maana anashirikishwa kwenye dhambi hii.

Mwanadamu anapendwa sana na Mungu kuliko unavyodhani.

Soma sana, utaelewa kila kitu, na vyote vipo wazi.
 
Mimi hiyo pia niliifikiria sana nikajiuliza;

Kwanini Mungu kabla ya kumuumba mwanadamu hakumfungia shetani huko kuzimu mpaka siku ya kyama?

Kwanini Mungu pale Bustani ya Edeni akaweka ule mti wenye yale matunda ambao Adamu na mkewe waliyala na kupata dhambi?

Na kwanini Mungu alipoona Adamu na mkewe wamekula lile tunda na kulikuwa na mti mwingine pale wa uzima wa milele, Mungu akawazuia wasile matunda yake wasije wakasamehewa makosa waliyofanya kwa kula ule wa mema na mabaya?

SIJAPATA JIBU, mwisho nikasema, Mungu anampenda binadamu sana, hivyo hakuna atakayechomwa moto, wote tutaenda peponi siku ya mwisho.
Hahahahaaa...Mungu anampenda sana Mwanadamu, ndio. Ila wapo ambao hawampendi Mungu.
Unadhani Mungu atawafanyeje watu hao? Ni kuni tuu
 
Kwanza unakosea mno kuandika neno mungu ukimaanisha Mungu. Hilo ni kosa kuu mno maana linaharibu maana yako nzima.

Pili, inabidi usome vitabu vya dini vizuri, ili uelewe kwanini mgogoro uliopo wa Mungu na shetani unamuingizaje mwanadamu.

Tatu, unamkosoa Mungu kwa jambo ambalo haulifahamu vizuri, na sidhani kama umedhamiria kufahamu mengi zaidi.

Nne, vitabu vya dini vimeelezea kila kitu, ingawa kwa ufupi mno, kwanini shetani alitokea, tangu enzi za mwanadamu wa kwanza, hadi kipindi cha Adamu na Hawa, mpaka kufukuzwa edeni na mambo ya Kizazi cha kaini.

Soma vizuri, biblia utapata majibu ya maswali yako.

Pia, sio kila jambo mungu alilijua kabla kuwa Malaika atakosea, la hasha. Ndio maana zipo adhabu zinatolewa kwa kila kiumbe. Mf. Majabali na majitu enzi za nuhu.

Hata shetani kuasi kwake kuna sababu kubwa inayotokana na mwanadamu, na ndio maana anashirikishwa kwenye dhambi hii.

Mwanadamu anapendwa sana na Mungu kuliko unavyodhani.

Soma sana, utaelewa kila kitu, na vyote vipo wazi.
Soma hapo kwenye bold.

Ndio maana tunasema Mungu hajui kila kitu, hajui kesho itatokea nini na wala hana ufahamu na mambo yajayo. Ile ya kusema Mungu anajua kila kitu, mwanzo hadi mwisho ni uongo.

Sasa kama Mungu hajui kila kitu na hajui kesho ama wiki ijayo kitatokea nini, hua mnamuomba ili awasaidie nini? Maana yake ni kua hana msaada wowote ule na wala hawezi kubadilisha chochote.

Ndio maana tunasema hizi dini ni utapeli kama utapeli mwingine, Mungu hayupo.
 
Utajisemesha hapa uzuri Mungu alivyotuumba alituwekea sauti kakumtambua na kila binadamu kapo tu utake ni hivyo na usitake ni hivyo...
 
Turudi kwenye mada Mungu mwenyewe ndio alitaka shetani aasi na ili aje kua Mtihani kwa watu wake kupima imani zao na alijua. Kama ata asi before shetani alikua kiumbe ana sali kuliko malaika wote na yeye aliishi duniani kabla na sio kama wengi wanavyohisi kua ni malaika noo shetani ni kizazi cha majini kwa kua aliumbwa kwa moto na hakuumbwa kwa light kama ilivyo malaika..so kwanini Mungu anajua yajayo?

Mungu alipomuumba Adam shetani alipatwa na wivu balaa na kuanza kukomplaini chini chini kipindi iko hata adama ajapuliziwa pumzi yani yupo tu kawekwa kama sanamu na alikaa hivyo kwa muda wa miaka kama 200 hivi bila kupuliziwa pumzi ya Mungu shetani wivu unamshika kwakua dunia anenda kukabidhiwa adam akawa anatoa madhaifu kiumbe gani yeye anaweza kupitia mdomoni akatokea upande wa pili yaani una tundu juu na chini.

Sasa Mungu alijua kua shetani hata afiki ndio maana aliwaambia malaika wote wamsjudie Adam na wakafanya hivyo isikua huyo ibilisi..kwanini alikataa na hapo ndio uthibitisho kua yeye sio malaika hakuna malaika anayeweza kupinga amri ya mwnyezi Mungu..wameumbwa hivyo hawapingi. Kwa hio ana kazi maalum hapa dunian so isikupe taabu..
Reffernce fuatlia katka Quran na hadith
 
Alafu kuna amri inayosema "USITAMANI MKE ASIYE MKE WAKO" mbona kama ime base upande mmoja....yaani wanaume tukimtamani mke wa mtu ni dhambi, ila wao😂😂😂
 
Soma hapo kwenye bold.

Ndio maana tunasema Mungu hajui kila kitu, hajui kesho itatokea nini na wala hana ufahamu na mambo yajayo. Ile ya kusema Mungu anajua kila kitu, mwanzo hadi mwisho ni uongo.

Sasa kama Mungu hajui kila kitu na hajui kesho ama wiki ijayo kitatokea nini, hua mnamuomba ili awasaidie nini? Maana yake ni kua hana msaada wowote ule na wala hawezi kubadilisha chochote.

Ndio maana tunasema hizi dini ni utapeli kama utapeli mwingine, Mungu hayupo.
Hizi ni busara za kibinadamu ambazo zilishazungumziwa kuwa ni Upumbavu mbele za Mungu. So, usijaribu.

Alafu, pale waliozungumziwa ni Malaika, na si Binadamu.

Mungu anamjua binadamu kabla hajatungwa na wazazi wake. Ipo mifano mingi mno kwenye dini ya Kikristo. Maana sijui hata nianze na upi. Hata watu wa dini ya kiislamu wakikuadithia, jinsi Mungu anavyomjua mwanadamu, utastaajabu mengi na kusadiki.

My point is..mwanadamu amepewa mamlaka na ukuu wa duniani na Mungu mwenyewe, na ndio maana uumbaji wake, ni mfano wa Mungu. So, huez pingana na creator coz kakuumba wewe, anajua kila kitu hata kabla hujaanza kufikiria
 
Back
Top Bottom