Kwanini Mungu hakurekebisha kilichosababisha shetani akaasi kabla ya kumuumba binadamu?

Vitabu vya Mola ni Injili (Hii haipo tena), kadhalika Taurati (Hii pia haipo) Zaburi (Hii kadhalika haipo) kilichopo kwa sasa ni Qur'aan. Anza kuihoji Qur'aan.
We una akili Sana lakini hili linanishangaza sana. hebu tufafanulie vilikopotelea na kwanini nikuamini wewe unayepiga chenga kuelezea majestic plural na kuleta uongo uongo tu na usanii. hivi nani anayewafundisha hizo mambo?
 
Ukiangalia katika zile sheria kumi alizompa mussa, Mungu ameonekana kuzivunja baadhi sheria hizo kwa kwenda kinyume nazo

Amesema usiue lakini yeye kaua watu kwa kuwachoma moto kwenye sodoma "naskia baada ya hukumu hiyo alijilaumu akasema hatotoa hukumu ya moto tena kwa binadamu, lakini tunaona anazidi kuongeza magogo kuchochea moto wa jehanamu dhidi ya watenda dhambi hapa duniani" (hapa mungu anajaribu kututangazia amani halafu nyuma kashika sime)

Sent using unknown device
Mkuu sio tu sodoma na gomola hata kwenye gharika ta Nuhu Aliua watu mamilion kwa mamilion na akajiraumu tena kama kawaida yake na kujiapiza kuwa hataua watu tena kwa gharika au maji yaani huyu Mungu ni kigeugeu gata hajifunzi kutokana na makosa yake sasa mtu jama huyu tunaanzaje kumwamini anayosema na yanayosemwa juu yake??
 
We una akili Sana lakini hili linanishangaza sana. hebu tufafanulie vilikopotelea na kwanini nikuamini wewe unayepiga chenga kuelezea majestic plural na kuleta uongo uongo tu na usanii. hivi nani anayewafundisha hizo mambo?
Kwanza kabisa nakukumbusha ya kuwa suala la jina la taadhima nilishalimaliza, na ubainifu katika sura ya 113 niliuweka bali zipo ithibati nyingi. Kwahiyo usilete uongo usio kuwa na msingi wowote.

Hivyi vingine kuna sababau kadha wa kadha zilizopelekea kupotea, ipo sababu ya hila za watu za makusudi kubadilisha maandiko na ipo sababu ya kihistoria ambayo ilitokana na watu kutokuandika ujumbe kipindi cha uhai wa nabii husika wakaja kuandika baada ya kufa kwa nabii husika kwa miaka kadhaa, hapa rejea uandishi wa Injili.
 
Mkuu sio tu sodoma na gomola hata kwenye gharika ta Nuhu Aliua watu mamilion kwa mamilion na akajiraumu tena kama kawaida yake na kujiapiza kuwa hataua watu tena kwa gharika au maji yaani huyu Mungu ni kigeugeu gata hajifunzi kutokana na makosa yake sasa mtu jama huyu tunaanzaje kumwamini anayosema na yanayosemwa juu yake??
Tuwekee andiko analo jilaumu.
 
Wewe una matatizo sana. unajiamini kuwa unajua sana kuliko unaozungumza nao. ondoa hilo blanketi la udini ujifunze.bkatadute mwenyewe hizo maana zote mbili uzilete hapa and then we can talk
Maana ya Ushirikina nimeshakupa. Mkiwa mnatoa maana za maneno kwanza mzisome na mjue asili ya maneno husika. Mfano tamko Ushirikina hili ni jina kwalo lina asili ya Kiarabu lenye kusomeka "Shirki" , kufata mjengeko wa sarufi ya Kiswahili, jina hilo likatoholewa na kuwa hivi lilivyo.

Kwahiyo hapa nimehitimisha ya kuwa hujui maana ya Ushirikina, kasome.
 
Nacheka sana, maneno yangu yako wazi sana.

Ngoja nikuulize,unakubali au kuamini juu ya Utatu ?

Hamna jibu la swali hilo.
auferet dominus said:
usilete heresy hapa mzee. lete hoja zilizo makini. umenisikia mimi nikisema habari ya utatu? utatu umeuleta wewe na kupiga chenga kwako. mimi siuamini utatu. utatu kwa nilivosikia ni mungu walio watatu. mimi namwamini Mungu mmoja tu, mmoja tu, ambaye kwa uwezo wake aliamua kufanyika nafsi tatu. sikuogopi wewe hata nifiche hoja zangu.
Nacheka sana, maneno yangu yako wazi sana.

Ngoja nikuulize,unakubali au kuamini juu ya Utatu ?
#№######
Hapo juu niliandika hivi "mimi siuamini utatu. utatu kwa nilivosikia ni mungu walio watatu. mimi namwamini Mungu mmoja tu, mmoja tu, ambaye kwa uwezo wake aliamua kufanyika nafsi tatu. sikuogopi wewe hata nifiche hoja zangu.
 
Halafu unakataa ya kuwa unaamini mungu mmoja. Kadhalika nipe tofsuti kati ya Utatu na nafsi tatu kivitendo.

Nipe ushahidi wapi alijifanyia nafsi tatu, na hizo nafsi tatu mmezijuaje na zinatambulika kama nani na kazi zao ni zipi na linawezekana vipi hili ?

Angalizo usilete habari za vijiweni.
 
Kwanza kabisa nakukumbusha ya kuwa suala la jina la taadhima nilishalimaliza, na ubainifu katika sura ya 113 niliuweka bali zipo ithibati nyingi. Kwahiyo usilete uongo usio kuwa na msingi wowote.

Hivyi vingine kuna sababau kadha wa kadha zilizopelekea kupotea, ipo sababu ya hila za watu za makusudi kubadilisha maandiko na ipo sababu ya kihistoria ambayo ilitokana na watu kutokuandika ujumbe kipindi cha uhai wa nabii husika wakaja kuandika baada ya kufa kwa nabii husika kwa miaka kadhaa, hapa rejea uandishi wa Injili.

1. Hukutoa sababu yoyote yenye msingi ya majestic plural ya we.umesema tu kuwa waliopokea hao makuraishi hawakubali ujumbe wote. Hukueleza kama pia hawakutambua kuwa anayewapa ujumbe alikuwa katika nafsi tatu. Pia umejitengenezea sababu za Mungu kutokuwa na washirika.

Nakukubalia kuwa hana washirika lakini nakufundisha kuwa anazo nafsi zaidi ya moja kwa sababu anao uwezo wa kuwa katika nafsi tatu kwa sababu yeye ni Mungu. Wewe hutaki eti kwa sababu kuwa nafsi tatu ni kuonyesha udhaifu mpaka kuita wa kumsaidia, sababu ya ovyo kiasi gani hii. Ukasema hakuzaliwa, nakukubalia kuwa hakuna aliyemuumba Mungu lakini ana uwezo wa kuumba kiumbe chochote kama atakavyo hata akitaka kumzlisha bibi wa miaka 90 au kumzalisha bikira bila mwanaume, anaweza kwa sababu yeye ni Mungu.

Wewe hutaki halafu unasema amejiharamishia kufanyika nafsi zaidi ya moja. Sijui anakufundisha nani huyo kafr mkubwa asiyeamini UWEZO wa Mungu. Kama hawezi kwa nini unaendelea kujidanganya kuwa unamwamini? Huo ndo ushirikina usioujua.
2. Sababu za kupotea kwa vitabu huna. Ni hisia zako tu na wenzio kwa na kwa sababu vitabu wanavyotumia kwenye imani zingine havikubaliani na vyenu basi unarule kuwa hivi sio. Nakukubalia kuwa yawezekana kuna hila ya kuvipoteza vitabu hivyo na mwenye nia hiyo ni shetani mwenyewe.

Lakini nikuhakikishie Mungu hashindwi kirahisi hivyo. Vitabu hivyo vipo vitabu ambavyo ninyi waislamu mnashauriwa kuwauliza wale wenye hivyo vitabu pindi mnapokwama kwenye mambo mbali mbali kama hilo la we. Hakuna cha majestic plural hapo. Mungu alikuwa anazungumza na nafsi yake kuwapa ujumbe wowote aliokusudia.

Hili la vitabu kupotea likwambie tu value ya hivyo vitabu. Unaweza kufikiria utavipoteza kabisa lakini hauwezekani. Kitabu kisiposhambuliwa ikupe fununu tu kama ni kitabu kinachowatisha wenye hila au ni kitabu cha kawaida tu. Vitabu vya kawaida haviwindwi.
 
Halafu unakataa ya kuwa unaamini mungu mmoja. Kadhalika nipe tofsuti kati ya Utatu na nafsi tatu kivitendo.
Huo utatu mimi siujui. Muulize aliyekuambia Habari ya utatu. Kuhusu Mungu, kwanza unapoandika Mungu tafadhali tumia herufi kubwa mwanzoni. Au labda nikusamehe tu kwa sababu una vinasaba vya ukafr.
Sasa kuhusu Mungu kufanyika nafsi tatu alichagua mwenyewe toka mwanzo aliposema na tuumbe mtu kwa mfano wetu na kwa sura yetu Mwa 1:26. Hapa Mungu anasema na tuumbe mtu kwa mfano wetu na sura yetu. Huyu ni Mungu mmoja anayezungumza na nafsi zake kama vile unapojishauri ngoja nichote majinna una mikono na macho na miguu na mgongo. Unajishauri na unafanya kwa kutumia your members. Tunapokuja kuona ni nafsi zipi hizo anazozungumza nazo ni Mathayo 28:18-20. Kasome
Nipe ushahidi wapi alijifanyia nafsi tatu, na hizo nafsi tatu mmezijuaje na zinatambulika kama nani na kazi zao ni zipi na linawezekana vipi hili ?
Kabla ya ushahidi unaoutaka nipe wewe ushahidi wa haya yafuatayo:
1. umezaliwa na mama huyo unayemfahamu
2. umezaliwa na baba huyo unayemfahamu
Ukileta huo uthibitisho bila kumquote mtu mwingine.
Angalizo usilete habari za vijiweni.
Kijiweni ndio nini?
 
hii ni sababu ya kijinga iliyopata kutokea..
kina jahal waliuliza kuhusu Jua kuzama kwenye tope?vipi kuhusu manii kutoka mgongoni hayo mambo waquraysh waliyajua?
kwasababu watu fulani hawakuona tatizo haimaanishi halikuwepo.
kipindi hiko utumwa ilikuwa jambo la kawaida.kwahyo hamna aliyemhoji mtume kumiliki watumwa ila sasaivi tunaona ilikuwa ufala...

By the way sijasema matumizi ya wingi yanamfanya Allah awe wengi..ila yanamfanya aoneshe kuwa Mungu wengi ni bora kuliko mmoja...hajiamini na umoja wake.
Hahahaha ! ujinga ni kutokujua kitu, inaonyesha ufikiri wako umekoma kwenye ideology mlizomezeshwa. Ukitaka kufahamu kitu hasa vitabu vya dini ni lazima uwe mbobezi wa lugha asili iliyoandikwa katika vitabu hivyo. Tatizo lenu mnasoma hivyo vitabu vilivyotafsiriwa kwa kiswahili halafu mnakuja kuleta hoja za kipuuzi kabisa, hebu soma hayo maandiko "Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika checmchem yenye matope meusi" hiyo ni tafsiri ya Quran 18:86, nani aliyeona jua linatua katika chemchem yenye matope meusi? Je ni kweli Mungu anasema ya kuwa jua linazama kwenye matope meusi?

Ile picha yako iliyokuwa imeandikwa maneno ya kipuuzi ulikuwa una maanisha nini? (refer to your post #1230)

Mungu anajiamini sana kwa upekee wake, ndiyo maana kama ukisoma Qurani huo uwingi anautumia katika kuonyesha utukufu wake kwa kusema "SISI" na mwanadamu ukiona sentensi inayosema sisi basi lazima uzingatie ujumbe wake. Katika aya zote za Qurani zinazoelezea mambo ya itikadi na ibada, Mungu ametumia umoja.
 
1. Ni Mungu ndie aliyesema kuwa anaposema we basi sisi tujuwe ni majestic plural? Au umepata wapi dhana hiyo?
2. Yako maeneo aliyojiita I au Me au my. Nini kigezo chake cha hapa kujiita we na huku I?
3. Unakubali au unakataa kuwa Mungu anao kila uwezo wa kujifanya nafsi moja, mbili au zaidi kwa yeye Mungu mwenye kuweza?
1. Huo uwingi ni uwingi wa taadhima, na Mungu aliteremsha kitabu chake Quran kwa lugha ya kiarabu na wao ndiyo wenye kujua nini maana ya uwingi wa taadhima, na hiyo siyo dhana bali ni kanuni ya lugha ya kiarabu ya kutumia uwingi wa taadhima. Ndiyo maana hakuna mwarabu yoyote toka Qurani inashushwa mpaka mtume anafariki aliyeweza kuhoji matumizi ya uwingi katika aya zilizotaja utukufu wa Mungu.

2. Kama ukisoma Quran, uwingi umetumika katika aya za kuonyesha utukufu wa Mungu katika yale aliyoyaumba. Na anatumia umoja katika masuala ya ibada na itikadi.

3. Mungu ametakasika na kila sifa za upungufu, hivyo siwezi kukubali kuwa Mungu anaweza kujifanya nafsi mbili au zaidi, kwani ukishafikiria hivyo utafunguliwa milango ya kuwa na fikra za kuwa na nafsi nyingi za Mungu, kitu ambacho hakuna kitabu cha dini chenye kufafanua hivyo.
 
Huo utatu mimi siujui. Muulize aliyekuambia Habari ya utatu. Kuhusu Mungu, kwanza unapoandika Mungu tafadhali tumia herufi kubwa mwanzoni.
Haya alikwambia Yesu au ?
Au labda nikusamehe tu kwa sababu una vinasaba vya ukafr.
Kwanza rekebeisha hapo,tamko Kafiri ni kwa wasio kuwa Waislamu peke yao. Kwahiyo usipoteze maana ya tamko, sababu asili yake iko wazi na maana yakw kadhalika iko wazi.
Sasa kuhusu Mungu kufanyika nafsi tatu alichagua mwenyewe toka mwanzo aliposema na tuumbe mtu kwa mfano wetu na kwa sura yetu Mwa 1:26.
Hii maana haiko sawa, na haya maneno unatakiwa untuthibitishie ya kuwa nani ameyasema, na hiki kitabu cha mwanzo amekiandika nani ?
Hapa Mungu anasema na tuumbe mtu kwa mfano wetu na sura yetu.
Tamko hili au kauli hii, haionyeshi wingi wa Mola kadhalika haionyeshi ya kuwa kuna kufanana kwa Mola na viumbe wake wala hakuonyeshi hizo nafsi nyingi, mpaka uweke andiko linalothibitisha jambo hilo.
Huyu ni Mungu mmoja anayezungumza na nafsi zake kama vile unapojishauri ngoja nichote majinna una mikono na macho na miguu na mgongo. U
Hii bado ni nafsi moja mzee. Hili gumu sana kwako naona unalazimisha jambo lisilo wezekana.
Tunapokuja kuona ni nafsi zipi hizo anazozungumza nazo ni Mathayo 28:18-20. Kasome
Kwanza ya kusoma andiko hilo, naomba unithibitishie ukweli wa kile kilichoandikwa humo katika Mathayo.
 
Kabla ya ushahidi unaoutaka nipe wewe ushahidi wa haya yafuatayo:
1. umezaliwa na mama huyo unayemfahamu
2. umezaliwa na baba huyo unayemfahamu
Ukileta huo uthibitisho bila kumquote mtu mwingine.
Itifaji lazima izingatiwe.

Pili, jambo nililo kutaka ufanye ni tofauti kabisa na haya maswaki uliyouliza, yaani ni maswali ya kitoto mno.
 
1. Huo uwingi ni uwingi wa taadhima, na Mungu aliteremsha kitabu chake Quran kwa lugha ya kiarabu na wao ndiyo wenye kujua nini maana ya uwingi wa taadhima, na hiyo siyo dhana bali ni kanuni ya lugha ya kiarabu ya kutumia uwingi wa taadhima. Ndiyo maana hakuna mwarabu yoyote toka Qurani inashushwa mpaka mtume anafariki aliyeweza kuhoji matumizi ya uwingi katika aya zilizotaja utukufu wa Mungu.
2. Kama ukisoma Quran, uwingi umetumika katika aya za kuonyesha utukufu wa Mungu katika yale aliyoyaumba. Na anatumia umoja katika masuala ya ibada na itikadi.
3. Mungu ametakasika na kila sifa za upungufu, hivyo siwezi kukubali kuwa Mungu anaweza kujifanya nafsi mbili au zaidi, kwani ukishafikiria hivyo utafunguliwa milango ya kuwa na fikra za kuwa na nafsi nyingi za Mungu, kitu ambacho hakuna kitabu cha dini chenye kufafanua hivyo.
Will come back to you tomorrow. Huyo sijui jurjani naona ananipotezea muda tu.
 
Shetani anaweza kuwa wewe Na Mungu Anaweza kuwa wewe mwenyewe,

ila Amini Usiamini au kubali kataa, wewe utakufa na ipo Nguvu Iliyosababisha haya yote ita kurenew nawe utakuw wew katka hali nyingine,

haijalishi kuwa alijua au hakujua ila muongozo ametoa, na haukinzani na akini za kibinadamu, .................
 
1. Huo uwingi ni uwingi wa taadhima, na Mungu aliteremsha kitabu chake Quran kwa lugha ya kiarabu na wao ndiyo wenye kujua nini maana ya uwingi wa taadhima, na hiyo siyo dhana bali ni kanuni ya lugha ya kiarabu ya kutumia uwingi wa taadhima. Ndiyo maana hakuna mwarabu yoyote toka Qurani inashushwa mpaka mtume anafariki aliyeweza kuhoji matumizi ya uwingi katika aya zilizotaja utukufu wa Mungu.
Asante kwa post hii. Naomba nifundishe jambo moja. Kwa mujibu quran au rejea nyingine wazo la kuwa Yuko Mungu liliwafikiaje walimwengu wa kiislam au wengine wowote? Je Hawa walimwona Mungu kwa sura yake au kumsikia kwa sauti yake? Kwa hili suala lililoko mezani la uwingi, nini kiliwafanya waimagine huyo aliekuwa akijiita 'sisi' alikuwa peke yake? Alipokuwa akizungumza nao hao wapokeaji alifafanua kuwa najiita we kwa sababu ya taadhima yake? Je ni kipi hasa cha kushikika kilichowaondoa mashaka kuwa huyu we alikuwa actually ni mmoja?

3. Mungu ametakasika na kila sifa za upungufu, hivyo siwezi kukubali kuwa Mungu anaweza kujifanya nafsi mbili au zaidi, kwani ukishafikiria hivyo utafunguliwa milango ya kuwa na fikra za kuwa na nafsi nyingi za Mungu, kitu ambacho hakuna kitabu cha dini chenye kufafanua hivyo.
Hii kwa hisia zangu (zinaweza kuwa si sahihi) ni madai tu ya wanazuoni au watu wengine. Zaweza kuwa sawa au kuwa na makosa. Kutakasika ni kweli, lakini kwa kuwa ana uwezo aweza kuamua kujifanya nafsi zaidi ya moja. Ni namna gani hilo linaondoa kutakasika kwake?
 
Habari ya jumapili.

Dini inasema shetani aliasi huko juu mbunguni mahala palipotukuka na palipoinuka juu anapoishi mungu. Baada ya shetani kuasi mungu akamtimua na kumshusha huku Duniani.

Dini inasema baadae mungu akamuumba mwanadamu na kumuweka Duniani, maana yake mwanadamu alipowekwa duniani tayari shetani alikua duniani muda mrefu tu anakula zake maisha.

Hadithi ya shetani kuasi iko one sided, yaani inaelezwa kutoka upande wa mungu, hakuna aliewahi kusikia upande wa shetani(tayari binadam wanamshutumu shetani kwa habari ya kuambiwa, one sided story, hivyo shetani anahukumiwa kua ni mbaya bila kusikilizwa).

Dini haisemi kwa nini shetani aliasi na ilikuaje akaasi. Dini inasema mungu anajua kila kitu, all knowing lakini haisemi mungu alishindwaje kujua kua shetani atakuja kuasi ili asimuumbe. Na kama alijua shetani atakuja kuasi kwa nini alimuacha aasi. Mbaya zaidi huo mgogoro wao umetuingiza na sisi binadam ambao hatujui chanzo cha mgogoro. Yaani mungu anarecruit binadam washirikiane nae mwenye mgogoro wake na shetani huku binadam hawajui chanzo cha mgogoro wao. Na mungu anatishia kua yoyote ambae hatashirikiana nae kwenye mgogoro huo atampanish vikali. Unajiuliza hakuaje involved kwenye mgogoro nisioujua chanzo chake na natishiwa adhabu kali kama sitashiriki huo mgogoro ambao in fact haupo kwa sababu mungu hajaonyesha kuwepo, hivyo watu waoga na wajinga wanalazimika kushiriki mgogoro blindly ili kuogopa adhabu.

Kama mungu anawapenda wanadamu kama dini inavyosema alipaswa kurekebisha kasoro zilizojitokeza kabla ya kumuumba mwanadam, lakini pia alipaswa kujua in the first hand kua shetani atakuja kuasi kabla hajamuumba, vinginevyo hajui kila kitu kinyume na inavyosemekana kua anajua kila kitu.

Tukubali tukatae, maovu yote duniani kama mauaji, wivu, kifo, husda, wizi, matetemeko ya ardhi, tsunami, vimbunga, ukame, magonjwa yote chanzo chake ni mungu. Mungu ameshindwa kabisa kutuonyesha kua kweli anatupenda kama anavyosemwa, ameshindwa kuonyesha kweli kua anajali Mbaya zaidi ameyatengeneza alafu ameshindwa kuyaondoa.

Hii mada inaendelea.

Nyongeza ya mjumbe.
kitabu kinasema hivyo maana biblia haisemi hivyo
 
Asante kwa post hii. Naomba nifundishe jambo moja. Kwa mujibu quran au rejea nyingine wazo la kuwa Yuko Mungu liliwafikiaje walimwengu wa kiislam au wengine wowote? Je Hawa walimwona Mungu kwa sura yake au kumsikia kwa sauti yake? Kwa hili suala lililoko mezani la uwingi, nini kiliwafanya waimagine huyo aliekuwa akijiita 'sisi' alikuwa peke yake? Alipokuwa akizungumza nao hao wapokeaji alifafanua kuwa najiita we kwa sababu ya taadhima yake? Je ni kipi hasa cha kushikika kilichowaondoa mashaka kuwa huyu we alikuwa actually ni mmoja?

Hii kwa hisia zangu (zinaweza kuwa si sahihi) ni madai tu ya wanazuoni au watu wengine. Zaweza kuwa sawa au kuwa na makosa. Kutakasika ni kweli, lakini kwa kuwa ana uwezo aweza kuamua kujifanya nafsi zaidi ya moja. Ni namna gani hilo linaondoa kutakasika kwake?
Kwa sisi wanadamu elimu na maarifa huyapata baada ya kufundishwa, hivyo basi Mungu huchagua katika viumbe vyake wajumbe (mitume) ambao ndiyo watakuwa wabeba muongozo kwa watu wao. Quran 10:47 ( Na kila umma una Mtume. Alipo wajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu, wala hawakudhulumiwa). Quran 16:36 (Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa MwenyeziMungu. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha.)

Kwa hakika Mungu hawezi kuonwa, Quran 6:103 (Macho hayamfikilii bali Yeye anayafikilia macho. Naye ni Mjuzi, Mwenye khabari). Hata mtume Musa alitaka kumuona Mungu lakini ilishindikana, Quran 7:143 (Na alipo kuja Musa kwenye miadi yetu, na Mola wake Mlezi akamsemeza, alisema: Mola wangu Mlezi! Nionyeshe nikutazame. Mwenyezi Mungu akasema: Hutoniona. Lakini utazame huo mlima. Ukibaki pahala pake basi utaniona. Basi alipo jionyesha Mola Mlezi wake kwa mlima, aliufanya uvurugike, na Musa akaanguka chini amezimia. Alipo zindukana alisema: Subhanaka, Umetakasika! Natubu kwako, na mimi ni wa kwanza wa Waumini).

Ama mwenyezi Mungu alizungumza na mitume wake kama aya niliyoitoa hapo nyuma ya kuwa Musa alizungumz na Mungu. Hivyo ukiangalia katika hiyo aya Q7:173 Musa anataka kumuona Mungu si kwamba anataka kuwaona miungu, na jibu Mungu analitoa kuwa huwezi "kuniona" siyo huwezi "kutona".

Hivyo hii ni dalili ya kuwa Mungu ni mmoja. Uwingi wa taadhima ni mfumo uliyotumika katika vitabu mbalimbali vya dini hasa katika semitic languge, kwa idadi Mungu ameshajipambanua ya kuwa yeye ni mmoja hana mshirika, Quran 4:171 (Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msimseme Mwenyezi Mungu ila kwa lilio kweli. Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neno lake tu alilo mpelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu.

Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka Yeye na kuwa na mwana. Ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha).

Na kama utakuwa na wakati unaweza ukapitia link hiyo hapo chini unaweza kupata mambo mengi yanayohusu uwingi wa taadhima yalivyojadiliwa kwa kirefu.
 
Kwa sisi wanadamu elimu na maarifa huyapata baada ya kufundishwa, hivyo basi Mungu huchagua katika viumbe vyake wajumbe (mitume) ambao ndiyo watakuwa wabeba muongozo kwa watu wao. Quran 10:47 ( Na kila umma una Mtume. Alipo wajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu, wala hawakudhulumiwa). Quran 16:36 (Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa MwenyeziMungu. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha.)
Kwa hakika Mungu hawezi kuonwa, Quran 6:103 (Macho hayamfikilii bali Yeye anayafikilia macho. Naye ni Mjuzi, Mwenye khabari). Hata mtume Musa alitaka kumuona Mungu lakini ilishindikana, Quran 7:143 (Na alipo kuja Musa kwenye miadi yetu, na Mola wake Mlezi akamsemeza, alisema: Mola wangu Mlezi! Nionyeshe nikutazame. Mwenyezi Mungu akasema: Hutoniona. Lakini utazame huo mlima. Ukibaki pahala pake basi utaniona. Basi alipo jionyesha Mola Mlezi wake kwa mlima, aliufanya uvurugike, na Musa akaanguka chini amezimia. Alipo zindukana alisema: Subhanaka, Umetakasika! Natubu kwako, na mimi ni wa kwanza wa Waumini). Ama mwenyezi Mungu alizungumza na mitume wake kama aya niliyoitoa hapo nyuma ya kuwa Musa alizungumz na Mungu. Hivyo ukiangalia katika hiyo aya Q7:173 Musa anataka kumuona Mungu si kwamba anataka kuwaona miungu, na jibu Mungu analitoa kuwa huwezi "kuniona" siyo huwezi "kutona". Hivyo hii ni dalili ya kuwa Mungu ni mmoja. Uwingi wa taadhima ni mfumo uliyotumika katika vitabu mbalimbali vya dini hasa katika semitic languge, kwa idadi Mungu ameshajipambanua ya kuwa yeye ni mmoja hana mshirika, Quran 4:171 (Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msimseme Mwenyezi Mungu ila kwa lilio kweli. Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neno lake tu alilo mpelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu. Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka Yeye na kuwa na mwana. Ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha).
Na kama utakuwa na wakati unaweza ukapitia link hiyo hapo chini unaweza kupata mambo mengi yanayohusu uwingi wa taadhima yalivyojadiliwa kwa kirefu.

hapa sasa tunapata mahali pazuri pa kuendelea na mazungumzo. Heko. Nitakuja tena.
 
Back
Top Bottom