Kwanini Mungu hakurekebisha kilichosababisha shetani akaasi kabla ya kumuumba binadamu?

Jamani imefikia huku hata salamu kuitikia ni shida..!
Salamu gani tena ? Sasa kama salamu ina makosa vipi unataka niunge mkono kosa ?

Rekebisha kiti chako kwanza kisha ukipambe. Numekukumbusha juu ya umakini kwanza.
 
Safi kabisa na hapa ndipo unapo ona ukamilifu wa Mola kwamba yeye hakosei,na vipi likatokea hilo jambo utasemaje ? Kwamba ulimlazimisha au utasema huo ni uhuru wa bendera kama unavyouita ?

Ndio maana nasema ya kuwa kujua kwake kwako hakukuzuii wewe kutofanya unalotaka,huelewi wapi ?

Ungekuwa unajibu maswali yangu lazima ungeona ujinga wako uko wapi.

Tuendelee ...
1. Ukamilifu wake ndio huo kwamba kama kapanga jambo lake ata kabla ujazaliwa mfano kwamba bwana A aende motoni , wewe bwana A ata ufanyaje utaenda motoni maana alishapanga hilo jambo , wewe ni bendera fuata upepo

2. Kujua kwake ndio jambo la msingi kwasababu wewe usiejua ndio unaangaika lakini Mungu wako matokeo anayo ata kabla ujaanza huko kuangaika , ndio maana nikasema wewe umepewa uhuru wa bendera ,
 
Nakusahihisha ya kuwa sio kupanga bali ni kujua,unatakiwa uwe makini.

Mimi na wewe hatujui ni wa motoni au wa peponi,kama hatujui ni wa motoni na ni wa peponi,na inajulikana uovu ni wa motoni na wema ni wa peponi kwanini tusifanye wema ili tuingie ? Hili swali naomba ulijibu,maana unakimbia sana maswali yangu.
2. Kujua kwake ndio jambo la msingi kwasababu wewe usiejua ndio unaangaika lakini Mungu wako matokeo anayo ata kabla ujaanza huko kuangaika , ndio maana nikasema wewe umepewa uhuru wa bendera ,
Ndio maana nakwambia zaidi ya mara mbili sasa kujua kwake yeye Allah aliye juu hakuja kuzuia wewe usifanye wema wala usifanye mabaya,kwahiyo haya unayo yauliza ni ubishi na kuleta utoto katika mambo ya kielimu.
 
Nakusahihisha ya kuwa sio kupanga bali ni kujua,unatakiwa uwe makini.

Mimi na wewe hatujui ni wa motoni au wa peponi,kama hatujui ni wa motoni na ni wa peponi,na inajulikana uovu ni wa motoni na wema ni wa peponi kwanini tusifanye wema ili tuingie ? Hili swali naomba ulijibu,maana unakimbia sana maswali yangu.

Ndio maana nakwambia zaidi ya mara mbili sasa kujua kwake yeye Allah aliye juu hakuja kuzuia wewe usifanye wema wala usifanye mabaya,kwahiyo haya unayo yauliza ni ubishi na kuleta utoto katika mambo ya kielimu.
Umeingia pazuri kweli , mimi na wewe hatujui kuwa ni watu wa motoni au peponi , je Mungu wako anajua au hajui kuwa mimi na wewe ni watu wa motoni au peponi ? kama anajua amejuaje wakati bado tupo hai na fursa ya kutubu tunayo
 
Salamu gani tena ? Sasa kama salamu ina makosa vipi unataka niunge mkono kosa ?

Rekebisha kiti chako kwanza kisha ukipambe. Numekukumbusha juu ya umakini kwanza.
Haya nifundishe mufti ili kesho nisikosee
 
je Mungu wako anajua au hajui kuwa mimi na wewe ni watu wa motoni au peponi ?
Hili nilishakwambia anajua na kujua kwake hakukuzii wewe kufanya unalo taka.

Unajua mpaka muda huu hujajibu hata swali moja,ila mimi najibu kila swali ninalo kuuliza,sasa huu utoto unatakiwa kuuacha.

Baada ya swali hili usiulize swali lingine kabla hujajibu maswali yangu niliyo kuuliza.
kama anajua amejuaje wakati bado tupo hai na fursa ya kutubu tunayo
Kuuliza amejuaje kunaonyesha ni namna gani humjui Mola wetu na ajabu ujasiri wa kumzungumzia usie mjua unaupata wapi ?

Swali la kujua amejuaje halistahiki kwake sababu yeye ndio ameumba kila kitu.

Nakukumbusha ujibu maswali yangu niliyo kuuliza huko nyuma na ninayo kuuliza.

Tuendelee ....
 
Hili nilishakwambia anajua na kujua kwake hakukuzii wewe kufanya unalo taka.

Unajua mpaka muda huu hujajibu hata swali moja,ila mimi najibu kila swali ninalo kuuliza,sasa huu utoto unatakiwa kuuacha.

Baada ya swali hili usiulize swali lingine kabla hujajibu maswali yangu niliyo kuuliza.

Kuuliza amejuaje kunaonyesha ni namna gani humjui Mola wetu na ajabu ujasiri wa kumzungumzia usie mjua unaupata wapi ?

Swali la kujua amejuaje halistahiki kwake sababu yeye ndio ameumba kila kitu.

Nakukumbusha ujibu maswali yangu niliyo kuuliza huko nyuma na ninayo kuuliza.

Tuendelee ....
Huwezi kujibu utaishia kuzunguka tu , Mungu wako anajua leo hii wapi wewe Zuri utaenda kama ni peponi au ni motoni anajua kabisaa , tena kabla ata wewe ujafa lakini ashajua sasa wewe una uhuru gani ? wewe rukaruka wewe lakini Mwisho wako Mungu wako anajua kabla ata huo mwisho wenyewe ujaufikia ndio hapo tunapokaa na kucheka pale unapojitangazia uhuru wa bendera
 
Utatulia tu , Kama Mungu ameshaamua kuwa wewe Zuri utaingia motoni kabla ajakuumba , wewe Zuri ndio ujui kuwa utaingia motoni au peponi , kwako wewe Zuri ndio jambo jipya likitokea, lakini kwa Mungu wako ni jambo alilolifahamu kabla ajakuumba sasa wewe una uhuru gani kama sio vichekesho
Mfano kama huu mungu amemuumba MTU ili awe mweusi lakini yeye anataka kuwa mwarabu si ukichaa huu
 
Inakuwaje?

Swali lingine linalofanana na hili ambalo sijajibiwa ni, kwa nini Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote kaamua kuumba ulimwengu ambayo mabaya yanawezekana (pamoja na shetani kuwezekana kuwepo) wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kuwepo (pamoja na shetani kutowezekana kuwepo)?

Mpaka leo sijajibiwa swali hili.
 
Mfano Mungu alimuumba Lusifa na mpango wake ulikuwa kwamba Lusifa aishi vizuri na Mungu lakini hilo likavurugika. Ikaja tena Mungu akamuumba mwanadamu akiwa na mpango kwamba nae aishi bila kutenda dhambi lakini huo mpango ukavurugika baada ya shetani kumrubuni mwanadamu na kula tunda. Mifano ya hiyo mipango "mizuri mizuri" iliyokuja kuvurugwa ipo mingi.
Inasemekana kuwa Mungu anamjua mtu tangu anamuumba, yaani tangu mtu anazaliwa Mungu anajua kila kitu chake maisha yake yote. Iweje amuumbe shetani halafu asijue kuwa huyu atakuja kuniasi?
Pia alishindwaje kumteketeza apotee kabisa Kama ni kweli aliona hafai tena?
Shetani huko aliko sidhani Kama anapata adhabu ambazo sisi binadamu tunazipata tukiwa hai
 
Kitabu cha Mwanzo sura ya 2 fungu la16-17: Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, 17. walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

(HILI ONYO ALIPEWA ADAM KABLA YA HAWA KUUMBWA MAY BE NDIO MAANA HAWA ALIOPKULA HILI TUNDA HAKUNA KILICHOTOKEA MPAKA PALE ADAM NAYE ALIPOKULA. INAONEKANA HAWA ALIAMBIWA NA ADAM MAANA WAKATI MUNGU ANATOA HILI AGIZO KWA ADAM HAWA ALIKUWA BADO HAJAUMBWA)

Kitabu cha Mwanzo sura ya 2 fungu la 18: Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
Nini hasa lilikuwa lengo la kuuweka huo mti wa mema na mabaya? Inaonyesha wazi kuwa Mungu alicreate mazingira ya kumfanya bidadamu atende dhambi. Mti Kama huo aliuumba wa kazi gani Kama sio kutafutiana lawama?
 
Mungu alimuumba binadamu ili amwabudu na kuabudu ni pamoja na kuweka masharti na vigezo vitakavyoonyesha kwamba kwali Mungu anaabudiwa. Hivyo hilo sharti la kutokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya lilikuwa ni sehemu ya mwanadamu kumwabudu Mungu. Hata malaika ambao ni viumbe walioumbwa na mungu pia humwabudu muumba wao.

Hata sisi binadamu tunapozaa watoto wetu na kuwalea huwa tunawapa masharti kwa nia njema kabisa ya kumfanya mtoto aenende katika mstari mnyoofu katika maisha yake hapa duniani. Na pindi mtoto/watoto wanapokataa kufuata yale masharti au kanuni tulizowawekea mara nyingi huwa tunawaadhibu kama sehemu ya kuwafundisha!
 
Na ulaaniwe, mwenyez mungu anasema watu walio viziwi kusia haya zake naye anawazidishia ugumu zaidi ili ukija kuzinduka mda ushapita utabaki na majuto tu. Inaonesha dhahiri watu humu wanavuta bangi kwanza ndo wanakuja kujadili habari za dini na pia inaonesha mtu amelelewa maisha kama ngurue tu .Hv mtu aliolelewa na wazaz wenye kujielewa kwel anashindwa kujifunza kwa nn kuna vitu akifanya anapigwa ,Jibu c lipo wazi kwasababu mzazi kaweka sheria zake ukizivunja ndo anakuchapa sasa utasema kosa LA mama yako au baba yako kwanini alikukataza usifanye kitu fulani. Kuna vitu unaweza ukaona unafanya sifa ili uonekane ila utakuja kujuta quran inasema utumie vizur ulimi wako pia hata sheria za kidunia zinasema hivyohivyo ulimi unaponza .
Acha matusi na ujikite kwenye hoja mkuu au ndiyo mungu wako anakufundisha matusi..
 
Back
Top Bottom