Kwanini Mungu hakurekebisha kilichosababisha shetani akaasi kabla ya kumuumba binadamu?

  • Thread starter Hakimu Mfawidhi
  • Start date
Hakimu Mfawidhi

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Messages
860
Points
1,000
Hakimu Mfawidhi

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined Oct 30, 2018
860 1,000
Habari ya jumapili.

Dini inasema shetani aliasi huko juu mbunguni mahala palipotukuka na palipoinuka juu anapoishi mungu. Baada ya shetani kuasi mungu akamtimua na kumshusha huku Duniani.

Dini inasema baadae mungu akamuumba mwanadamu na kumuweka Duniani, maana yake mwanadamu alipowekwa duniani tayari shetani alikua duniani muda mrefu tu anakula zake maisha.

Hadithi ya shetani kuasi iko one sided, yaani inaelezwa kutoka upande wa mungu, hakuna aliewahi kusikia upande wa shetani(tayari binadam wanamshutumu shetani kwa habari ya kuambiwa, one sided story, hivyo shetani anahukumiwa kua ni mbaya bila kusikilizwa).

Dini haisemi kwa nini shetani aliasi na ilikuaje akaasi. Dini inasema mungu anajua kila kitu, all knowing lakini haisemi mungu alishindwaje kujua kua shetani atakuja kuasi ili asimuumbe. Na kama alijua shetani atakuja kuasi kwa nini alimuacha aasi. Mbaya zaidi huo mgogoro wao umetuingiza na sisi binadam ambao hatujui chanzo cha mgogoro. Yaani mungu anarecruit binadam washirikiane nae mwenye mgogoro wake na shetani huku binadam hawajui chanzo cha mgogoro wao. Na mungu anatishia kua yoyote ambae hatashirikiana nae kwenye mgogoro huo atampanish vikali. Unajiuliza hakuaje involved kwenye mgogoro nisioujua chanzo chake na natishiwa adhabu kali kama sitashiriki huo mgogoro ambao in fact haupo kwa sababu mungu hajaonyesha kuwepo, hivyo watu waoga na wajinga wanalazimika kushiriki mgogoro blindly ili kuogopa adhabu.

Kama mungu anawapenda wanadamu kama dini inavyosema alipaswa kurekebisha kasoro zilizojitokeza kabla ya kumuumba mwanadam, lakini pia alipaswa kujua in the first hand kua shetani atakuja kuasi kabla hajamuumba, vinginevyo hajui kila kitu kinyume na inavyosemekana kua anajua kila kitu.

Tukubali tukatae, maovu yote duniani kama mauaji, wivu, kifo, husda, wizi, matetemeko ya ardhi, tsunami, vimbunga, ukame, magonjwa yote chanzo chake ni mungu. Mungu ameshindwa kabisa kutuonyesha kua kweli anatupenda kama anavyosemwa, ameshindwa kuonyesha kweli kua anajali Mbaya zaidi ameyatengeneza alafu ameshindwa kuyaondoa.

Hii mada inaendelea.

Nyongeza ya mjumbe.
Naongezea

Kwanini baada ya adam na hawa kula lile tunda walijikuta wapo uchi, halafu akaagiza malaika wawafukuze akihofia wanaweza wakala tunda la mema wakaja kua kama yeye?

Kwanini adam na hawa baada ya kula lile tunda ambalo walishawishiwa na shetani mungu alitoa hukumu ya vifo kwa adamu na hawa tu halafu shetani akamuacha ale bata tu?

Kwanini yesu atoe pepo ahamishie kwenye nguruwe badala ya kuyaua? Huoni kama nguruwe ilifanyiwa fitna kwa serikali ya sasa hivi yesu angehukumiwa kwa kufanya ukatili dhidi ya wanyama na taasisi za haki za wanyama

Kwanini wachungaji wanatoa mapepo badala ya kuyaua? Wangekua wanayaua kulikua na uwezekano mkubwa yakawa yamepotea kwenye uso huu wa dunia, lakini kwanini wayatoe je wameshindwa kuyaua?

Kwanini vitabu vya mungu vinadai kua sisi niwadhambi sana kiasi kwamba hatuwezi kufanya mawasiliano physically na mungu, halafu tunaona huyo huyo mungu anakutana na shetani na wanapiga stori kama ni marafiki wasiokua na uadui?? Je inamaana siye ni wadhambi sana kuliko shetani mwenyewe??
 
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Messages
8,216
Points
2,000
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2018
8,216 2,000
Acheni kujifariji vijana ,hakuna jambo wewe Zuri utalifanya Mungu wako akulijua kabla , yote anayajua kabla ayajatokea na baada ya kutokea , wewe ni bendera fuata upepo
Hili liko wazi na hakuna aliye kataa na kujua kwake hakunizuii mimi nisifanye ninacho taka na hili mpaka kwako na mfano wako.
 
ielewemitaa

ielewemitaa

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Messages
1,140
Points
2,000
ielewemitaa

ielewemitaa

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2014
1,140 2,000
Chanzo cha kufanya dhambi au kuumba dhambi ? Unatakiwa uweke wazi hapa.
Hayo weka wewe , ila mimi ninachojua chanzo cha dhambi ni Mungu mwenyewe , hayo mengine kama unataka kusema ruksa
 
ielewemitaa

ielewemitaa

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Messages
1,140
Points
2,000
ielewemitaa

ielewemitaa

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2014
1,140 2,000
Hili liko wazi na hakuna aliye kataa na kujua kwake hakunizuii mimi nisifanye ninacho taka na hili mpaka kwako na mfano wako.
Unachokifanya kilishajulikana na Mungu wako kabla ujakifanya , na bahati nzuri huwezi kubadilisha , hii ndio maana ya kujitekenya na kucheka mwenyewe
 
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Messages
8,216
Points
2,000
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2018
8,216 2,000
Mifano unayotoa inachekesha sana mimi kama baba naweza kujua jambo lakini lisitokee( hakuna ajabu ),
Safi kabisa na hapa ndipo unapo ona ukamilifu wa Mola kwamba yeye hakosei,na vipi likatokea hilo jambo utasemaje ? Kwamba ulimlazimisha au utasema huo ni uhuru wa bendera kama unavyouita ?
tofauti na Mungu wako analolijua ndio linalotokea ,
Ndio maana nasema ya kuwa kujua kwake kwako hakukuzuii wewe kutofanya unalotaka,huelewi wapi ?

Ungekuwa unajibu maswali yangu lazima ungeona ujinga wako uko wapi.

Tuendelee ...
 
ielewemitaa

ielewemitaa

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Messages
1,140
Points
2,000
ielewemitaa

ielewemitaa

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2014
1,140 2,000
Hili nilishakujibu huko awali,sasa sijajua unalirudia kwa misingi gani ?
Jibu lako ni dhaifu ndio maana hiyo kauli imeendelea na itaendelea kutamba humu ndani
 
ManchoG

ManchoG

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Messages
1,183
Points
2,000
ManchoG

ManchoG

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2017
1,183 2,000
Jamani imefikia huku hata salamu kuitikia ni shida..!
 
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Messages
8,216
Points
2,000
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2018
8,216 2,000
Jamani imefikia huku hata salamu kuitikia ni shida..!
Salamu gani tena ? Sasa kama salamu ina makosa vipi unataka niunge mkono kosa ?

Rekebisha kiti chako kwanza kisha ukipambe. Numekukumbusha juu ya umakini kwanza.
 
ielewemitaa

ielewemitaa

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Messages
1,140
Points
2,000
ielewemitaa

ielewemitaa

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2014
1,140 2,000
Safi kabisa na hapa ndipo unapo ona ukamilifu wa Mola kwamba yeye hakosei,na vipi likatokea hilo jambo utasemaje ? Kwamba ulimlazimisha au utasema huo ni uhuru wa bendera kama unavyouita ?

Ndio maana nasema ya kuwa kujua kwake kwako hakukuzuii wewe kutofanya unalotaka,huelewi wapi ?

Ungekuwa unajibu maswali yangu lazima ungeona ujinga wako uko wapi.

Tuendelee ...
1. Ukamilifu wake ndio huo kwamba kama kapanga jambo lake ata kabla ujazaliwa mfano kwamba bwana A aende motoni , wewe bwana A ata ufanyaje utaenda motoni maana alishapanga hilo jambo , wewe ni bendera fuata upepo

2. Kujua kwake ndio jambo la msingi kwasababu wewe usiejua ndio unaangaika lakini Mungu wako matokeo anayo ata kabla ujaanza huko kuangaika , ndio maana nikasema wewe umepewa uhuru wa bendera ,
 
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Messages
8,216
Points
2,000
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2018
8,216 2,000
1. Ukamilifu wake ndio huo kwamba kama kapanga jambo lake ata kabla ujazaliwa mfano kwamba bwana A aende motoni , wewe bwana A ata ufanyaje utaenda motoni maana alishapanga hilo jambo , wewe ni bendera fuata upepo
Nakusahihisha ya kuwa sio kupanga bali ni kujua,unatakiwa uwe makini.

Mimi na wewe hatujui ni wa motoni au wa peponi,kama hatujui ni wa motoni na ni wa peponi,na inajulikana uovu ni wa motoni na wema ni wa peponi kwanini tusifanye wema ili tuingie ? Hili swali naomba ulijibu,maana unakimbia sana maswali yangu.
2. Kujua kwake ndio jambo la msingi kwasababu wewe usiejua ndio unaangaika lakini Mungu wako matokeo anayo ata kabla ujaanza huko kuangaika , ndio maana nikasema wewe umepewa uhuru wa bendera ,
Ndio maana nakwambia zaidi ya mara mbili sasa kujua kwake yeye Allah aliye juu hakuja kuzuia wewe usifanye wema wala usifanye mabaya,kwahiyo haya unayo yauliza ni ubishi na kuleta utoto katika mambo ya kielimu.
 
ielewemitaa

ielewemitaa

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Messages
1,140
Points
2,000
ielewemitaa

ielewemitaa

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2014
1,140 2,000
Nakusahihisha ya kuwa sio kupanga bali ni kujua,unatakiwa uwe makini.

Mimi na wewe hatujui ni wa motoni au wa peponi,kama hatujui ni wa motoni na ni wa peponi,na inajulikana uovu ni wa motoni na wema ni wa peponi kwanini tusifanye wema ili tuingie ? Hili swali naomba ulijibu,maana unakimbia sana maswali yangu.

Ndio maana nakwambia zaidi ya mara mbili sasa kujua kwake yeye Allah aliye juu hakuja kuzuia wewe usifanye wema wala usifanye mabaya,kwahiyo haya unayo yauliza ni ubishi na kuleta utoto katika mambo ya kielimu.
Umeingia pazuri kweli , mimi na wewe hatujui kuwa ni watu wa motoni au peponi , je Mungu wako anajua au hajui kuwa mimi na wewe ni watu wa motoni au peponi ? kama anajua amejuaje wakati bado tupo hai na fursa ya kutubu tunayo
 
ManchoG

ManchoG

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Messages
1,183
Points
2,000
ManchoG

ManchoG

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2017
1,183 2,000
Salamu gani tena ? Sasa kama salamu ina makosa vipi unataka niunge mkono kosa ?

Rekebisha kiti chako kwanza kisha ukipambe. Numekukumbusha juu ya umakini kwanza.
Haya nifundishe mufti ili kesho nisikosee
 
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Messages
8,216
Points
2,000
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2018
8,216 2,000
je Mungu wako anajua au hajui kuwa mimi na wewe ni watu wa motoni au peponi ?
Hili nilishakwambia anajua na kujua kwake hakukuzii wewe kufanya unalo taka.

Unajua mpaka muda huu hujajibu hata swali moja,ila mimi najibu kila swali ninalo kuuliza,sasa huu utoto unatakiwa kuuacha.

Baada ya swali hili usiulize swali lingine kabla hujajibu maswali yangu niliyo kuuliza.
kama anajua amejuaje wakati bado tupo hai na fursa ya kutubu tunayo
Kuuliza amejuaje kunaonyesha ni namna gani humjui Mola wetu na ajabu ujasiri wa kumzungumzia usie mjua unaupata wapi ?

Swali la kujua amejuaje halistahiki kwake sababu yeye ndio ameumba kila kitu.

Nakukumbusha ujibu maswali yangu niliyo kuuliza huko nyuma na ninayo kuuliza.

Tuendelee ....
 
ielewemitaa

ielewemitaa

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Messages
1,140
Points
2,000
ielewemitaa

ielewemitaa

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2014
1,140 2,000
Hili nilishakwambia anajua na kujua kwake hakukuzii wewe kufanya unalo taka.

Unajua mpaka muda huu hujajibu hata swali moja,ila mimi najibu kila swali ninalo kuuliza,sasa huu utoto unatakiwa kuuacha.

Baada ya swali hili usiulize swali lingine kabla hujajibu maswali yangu niliyo kuuliza.

Kuuliza amejuaje kunaonyesha ni namna gani humjui Mola wetu na ajabu ujasiri wa kumzungumzia usie mjua unaupata wapi ?

Swali la kujua amejuaje halistahiki kwake sababu yeye ndio ameumba kila kitu.

Nakukumbusha ujibu maswali yangu niliyo kuuliza huko nyuma na ninayo kuuliza.

Tuendelee ....
Huwezi kujibu utaishia kuzunguka tu , Mungu wako anajua leo hii wapi wewe Zuri utaenda kama ni peponi au ni motoni anajua kabisaa , tena kabla ata wewe ujafa lakini ashajua sasa wewe una uhuru gani ? wewe rukaruka wewe lakini Mwisho wako Mungu wako anajua kabla ata huo mwisho wenyewe ujaufikia ndio hapo tunapokaa na kucheka pale unapojitangazia uhuru wa bendera
 
pwiro

pwiro

Member
Joined
Nov 3, 2018
Messages
92
Points
125
pwiro

pwiro

Member
Joined Nov 3, 2018
92 125
Utatulia tu , Kama Mungu ameshaamua kuwa wewe Zuri utaingia motoni kabla ajakuumba , wewe Zuri ndio ujui kuwa utaingia motoni au peponi , kwako wewe Zuri ndio jambo jipya likitokea, lakini kwa Mungu wako ni jambo alilolifahamu kabla ajakuumba sasa wewe una uhuru gani kama sio vichekesho
Mfano kama huu mungu amemuumba MTU ili awe mweusi lakini yeye anataka kuwa mwarabu si ukichaa huu
 
Forum statistics

Threads 1,326,267
Members 509,458
Posts 32,216,552
Top