Kwanini Mungu anaitwa Mungu na hakuitwa jina lingine? Kama Shetani ni mharibifu kwanini aliachwa hai?

Waarabu na Wazungu hakuna kitu walipatia Africa kama kuleta dini zao,
Ni vurugu mechi ambazo sio rahisi kuzishinda.
Wafia DINI ni watu wenye matatizo ya akili waliochangamkJehovah Mungu
Jehovah Mungu hakumuumba Shetani; labda useme Allah ndiye aliyemuumba Shetani(Allah siyo Mungu wa kweli). Tafadhali soma Ezekiel 28:13-19 utaona kuwa Shetani alikuwa Malaika mzuri kabisa na inadokeza kuwa alipewa pia jukumu fulani ktk Bustani ya Eden. Baada ya kuona uzuri na fahari aliyopewa akapata kiburi na hatimaye akamsingizia Jehovah kwa Hawa na baadae kwa Adam kuwa yeye Jehovah hakusema ukweli kuhusu TUNDA LA MTI WA KATI. Yesu alipokuwa hapa Duniani alizungumzia hilo ktk John 8:44 "Shetani hakusimama imara ktk kweli..." akaamua kusema uwongo. MANENO HAYO YAONESHA KUWA HAPO MWANZO ALIKUWA MALAIKA MZURI. Nikupe mfano: Baba na Mama wanapata mtoto mchanga matarajio yao ni mtoto huyo kuwa mtu mzima mwenye maadili mema. Endapo itatokea mtoto huyo akawa mwizi, wakulaumiwa si wazazi bali ni huyo mtoto kuwa alijiachia mazingira/marafiki wabaya/ au TAMAA ZAKE zikamfanya mwizi.
KWANINI JEHOVAH AKAMUACHA SHETANI MPAKA SASA?
Kwanza kabisa jukumu yake ilitangazwa siku ile Ile kwamba UZAO WA MWANAMKE UTAMPONDA KICHWA (unapoua nyoka ili afe kabisa unaponda kichwa) Yesu ndyo angefanya jukumu hiyo.
PIA FIKIRIA KUWA HAYO YAKITOKEA palikuwepo MALAIKA wengine (NB Mungu aliumba viumbe wake wakiwa na free will) hivyo kama angemuua Shetani mara Moja hao Malaika wengine wangetokeza maswali kuwa labda anachosema Shetani ni kweli.
Kiujumla Shetani aliwaambia Adam na Hawa kuwa kuwa chini ya UONGOZI WA Jehovah hakuwafaidishi- muwe nchini ya miongozo Tangu. Hivyo Jehovah aliwafukuza Toka Bustani ya Eden waende huko wakawe chini ya miongozo ya Shetani, ili wao wenyewe wajionee kama watafaidika. Hilo lilihitaji miaka mingi ipite ili sisi wanadamu tujithibitishie wenyewe kuwa nani kati ya Jehovah na Shetani apaswa kuwa mtawala wetu. Pia kumbuka vilio hivi unavyo toa kuwa " KWANINI MUNGU ANASHINDWA KUMUONDOA SHETANI ILI WANADAMU WAWE SALAMA?" yanawapa pia majibu wale Malaika wengine kuwa "Kumbe Jehovah ndiye alisema ukweli"
Ndyo maana Yesu ktk John 16:11 Shetani ni MTAWALA wa Ulimwengu huu. Hata hivyo akasema AMEHUKUMIWA
UKISOMA UFUNUO kitabu Cha mwisho kabisa
unaona kuwa hatimaye Utawala wa Ulimwengu huu unawekwa chini ya Yesu Ufunuo 11:15 (hii itatokea hivi KARIBUNI, kwanza NB 2029 ndiyo inatimia MIAKA 2000 Tangu Ulimwengu umjue MESIHA). UKISOMA UFUNUO 20:10 Shetani atupwa ziwa la moto; UFUNUO 20:14 Inasema ni kifo Cha MILELE.
Baada ya hayo sasa ndiyo Jehovah ktk Ufunuo 21:3 inasema ndiyo Ile hali ya mwazo itarudi" Jehovah atakuwa pamoja na Wanadamu, yaani watakuwa chini ya utawala wake" MATOKEO yatakuwa- wanadamu hawatakuwa na maombolezo, maumivu na kakutakuwa na KIFO tena😀😀 soma Ufunuo 21: 4
NB NINAYOSEMA HAYA YOTE YAKO KWENYE BIBLIA JAMANI SOMENI HIKI KITABU, KWANI TUNAISHI (on borrowed times) na mambo yaliyotabiriwa kwenye biblia yanatimia kwa kasi isiyoyakawaida
 
Miongoni mwa maswali najiuliza kila uchwao ni kwanini Mungu aliitwa Mungu na sio jina lingine?,Ni nani alimpatia hilo jina? Na kama yupo alikuwa nani?

Kwanini Mungu hakummaliza shetani hukohuko kama kweli ni muharibifu? kiasi kwamba anatuletea tabu ambazo tunaamini yeye ni chanzo? na anashindwaje kumuangamiza hata sasa ili hali hakuna anachondwa?
Unajiuliza kuhusu jina la Mungu!?
Ubongo ndio kiungo kinachoratibu shughuli zote za mwili wa mwanadamu. Hata jina unalojiita (AIMENTER) ni matokeo ya utendaji kazi wa Ubongo.. Unajua kuwa UBONGO wenyewe ndio uliamua uitwe UBONGO?
 
Jibu simple sana mkuu. Baba hawezi kushindana na mtoto wake ata akiwa mwizi au tabia mbaya au hawezi kumuua kisa kafanya kitu flaan inakuwa anajishushia hadhi yake ya ubaba na kuwa dikteta flaani kama ataweza kumuua mtoto wake zaidi anampa tu adhabu na badae anaweza hata mkataa akumuacha tu hata kama ni kero vipi kwake na majirani. Mungu hawezi kushindana na kitu alichokiumba lakini pia hapangiwi nini afanye na mwanadamu ila yeye anampangia mwanadamu nini afanye.
 
Mungu ni sifa ya mtu ama kiumbe cha kiroho chenye uwezo juu ya viumbe wenzake, pia hata mwanadamu akiwa juu ya wenzie huyo hutambulika kama MUNGU japo kizazi cha sasa kinaficha sana kuhusu hili jambo, haswa hao walioleta hizi dini wanatuaminisha Mungu ni mmoja na binadamu hawezi kuwa MUNGU.

Kama dini ya kikristo iko tofaut na dini ya kiislam basi hata MUNGU wao si mmoja bali tofaut, hapo tyr tunapata idadi ya MIUNGU wawili.

Kama dini ya ubudha ni tofaut na dini ya uhindu pia ni tofauti na dini ya Rastafarian hapo tyr tunapata idadi ya MIUNGU mingine ambayo si MUNGU mmoja, je nyie mnaosema Mungu ni mmoja mmetumia kigezo gani?

Kiuhalisia dunia ina Miungu wengi sana kimwili na kiroho, na hata huyo mnaemuita shetan nae ni Mungu wa hii hii dunia pia ndie huyo huyo Mungu wa ulimwengu wa Rohoni ambaye anatawala kiroho hii dunia.

Hata hao miungu wa dini zenu wote wapo chini ya Nguvu ambayo nguvu hiyo ndiyo iliyowaumba wao wawe juu ya viumbe vilivyo vidogo kinguvu kuwaliko wao.

Mungu ni cheo cha juu kwa viumbe wanao tawala maisha ya mwilini na Rohoni, lkn Nje ya Uungu kuna chanzo kilichozifanya hizo Nguvu na chanzo hichi sio Mungu, na hiki chanzo ndicho kilipaswa kuabudiwa na wanadamu+watu hapa dunian, lkn baada ya uhaini wa Miungu kujigeuza na kufanya uharamia wa kuwapotosha wanadamu kuwa wao/Miungu ndie wakuu wa kila kitu kumbe sio kweli.

Unachotakiwa kujua ni kwamba Kuna viumbe wenye nguvu zaid ya cheo cha Allah, Yesu, Elishadai, Elohim na majina mengi ya hovyo hovyo mliyodanganywa ni matakatifu, kumbe uongo mkubwa, hao wote ni aina ama jamii ya malaika ambao kiuhalisia ni wakubwa kiumri kuliko binadamu ndiomaana wametuzidi nguvu na maarifa wakaamua kututawala kupitia uongo na uchawi.

Binadamu ndie kiumbe wa mwisho ktk rank ya uumbwaji wa viumbe, maajabu Elimu hii haifundishwi huko makanisan na misikitini kwasababu hizo dini zipo chini ya ushawishi wa hivyo viumbe vinavyowadanganya.

Mungu Yesu ama Mungu Elohim ama Mungu Allah hawezi kumuangamiza Shetan kwakuwa hawa wote kicheo ni wamoja wote ni waungu ambao wameumbwa na Nguvu iliyo KUU kuwazidi.

Amkeni.
 
Yesu, MUNGU ama jina limetumika kama kiwakilishi fulani lakini uhalisia ama kitu kinachowakilishwa kina uhalisia ndani ya mtu mwenyewe, mfano ukisema Mungu ndani yako unakuana fikra ya roho, ama mtu ama kitu vyovyote utavyoita chenye uwezo na nguvu zaidi kuliko vyote.

Kwa hio jina hilo sio tatizo aitwe seba, kyala, jehova, jesus, deus. Haina tija lakini ni nini msemaji wa jina hilo anawakilisha moyoni mwake.

Realitu only exist inside you, huyo Mungu ama shetani ni kiwakilishi tu lakini image ya kinachowakilishwa unayo wewe na umeijenga hio conection kuelekea unachomaanisha sio!..

Ndio maana utakuta kuna neno aina fulani lina maana fulani kwenye hii jamii, sehemu nyingine ni matusi ama ni marufuku kutaja hilo neno, tatizo sio hilo neno ni maana ya watu husika na jinsi wanavyotumia.
 
hizi ni swaga,kumbuka katuumba na akili kwa mantiki,kama ndivyo kwanini asimuache huko akabiliane naye ili asisumbue watu huku
 
umenijibu kifalsafa umenishawishi,bado nina maswali,je hiyo nguvu asiliina jina ama haina?
 
Yesu, MUNGU ama jina limetumika kama kiwakilishi fulani lakini uhalisia ama kitu kinachowakilishwa kina uhalisia ndani ya mtu mwenyewe, mfano ukisema Mungu ndani yako unakuana fikra ya roho, ama mtu ama kitu vyovyote utavyoita chenye uwezo na nguvu zaidi kuliko vyote.

Kwa hio jina hilo sio tatizo aitwe seba, kyala, jehova, jesus, deus. Haina tija lakini ni nini msemaji wa jina hilo anawakilisha moyoni mwake.

Realitu only exist inside you, huyo Mungu ama shetani ni kiwakilishi tu lakini image ya kinachowakilishwa unayo wewe na umeijenga hio conection kuelekea unachomaanisha sio!..

Ndio maana utakuta kuna neno aina fulani lina maana fulani kwenye hii jamii, sehemu nyingine ni matusi ama ni marufuku kutaja hilo neno, tatizo sio hilo neno ni maana ya watu husika na jinsi wanavyotumia.
kwanini ilikuwa hivyo na sio tofauti ili kumaanisha hiki kinachomaanishwa?
 
Unajiuliza kuhusu jina la Mungu!?
Ubongo ndio kiungo kinachoratibu shughuli zote za mwili wa mwanadamu. Hata jina unalojiita (AIMENTER) ni matokeo ya utendaji kazi wa Ubongo.. Unajua kuwa UBONGO wenyewe ndio uliamua uitwe UBONGO?
Hoja yako nini?,ikiwa unanizungumzia mimi kama binadamu kamili kwa mfano zidi ya kile ambacho hatujui kama ni binadamu,ama nini,kina ubongo ama hakina,na hilo jina ni chanzo cha ubongo wake ama nini?,weka clear hoja yako
 
Jehovah Mungu hakumuumba Shetani; labda useme Allah ndiye aliyemuumba Shetani(Allah siyo Mungu wa kweli). Tafadhali soma Ezekiel 28:13-19 utaona kuwa Shetani alikuwa Malaika mzuri kabisa na inadokeza kuwa alipewa pia jukumu fulani ktk Bustani ya Eden. Baada ya kuona uzuri na fahari aliyopewa akapata kiburi na hatimaye akamsingizia Jehovah kwa Hawa na baadae kwa Adam kuwa yeye Jehovah hakusema ukweli kuhusu TUNDA LA MTI WA KATI. Yesu alipokuwa hapa Duniani alizungumzia hilo ktk John 8:44 "Shetani hakusimama imara ktk kweli..." akaamua kusema uwongo. MANENO HAYO YAONESHA KUWA HAPO MWANZO ALIKUWA MALAIKA MZURI. Nikupe mfano: Baba na Mama wanapata mtoto mchanga matarajio yao ni mtoto huyo kuwa mtu mzima mwenye maadili mema. Endapo itatokea mtoto huyo akawa mwizi, wakulaumiwa si wazazi bali ni huyo mtoto kuwa alijiachia mazingira/marafiki wabaya/ au TAMAA ZAKE zikamfanya mwizi.
KWANINI JEHOVAH AKAMUACHA SHETANI MPAKA SASA?
Kwanza kabisa jukumu yake ilitangazwa siku ile Ile kwamba UZAO WA MWANAMKE UTAMPONDA KICHWA (unapoua nyoka ili afe kabisa unaponda kichwa) Yesu ndyo angefanya jukumu hiyo.
PIA FIKIRIA KUWA HAYO YAKITOKEA palikuwepo MALAIKA wengine (NB Mungu aliumba viumbe wake wakiwa na free will) hivyo kama angemuua Shetani mara Moja hao Malaika wengine wangetokeza maswali kuwa labda anachosema Shetani ni kweli.
Kiujumla Shetani aliwaambia Adam na Hawa kuwa kuwa chini ya UONGOZI WA Jehovah hakuwafaidishi- muwe nchini ya miongozo Tangu. Hivyo Jehovah aliwafukuza Toka Bustani ya Eden waende huko wakawe chini ya miongozo ya Shetani, ili wao wenyewe wajionee kama watafaidika. Hilo lilihitaji miaka mingi ipite ili sisi wanadamu tujithibitishie wenyewe kuwa nani kati ya Jehovah na Shetani apaswa kuwa mtawala wetu. Pia kumbuka vilio hivi unavyo toa kuwa " KWANINI MUNGU ANASHINDWA KUMUONDOA SHETANI ILI WANADAMU WAWE SALAMA?" yanawapa pia majibu wale Malaika wengine kuwa "Kumbe Jehovah ndiye alisema ukweli"
Ndyo maana Yesu ktk John 16:11 Shetani ni MTAWALA wa Ulimwengu huu. Hata hivyo akasema AMEHUKUMIWA
UKISOMA UFUNUO kitabu Cha mwisho kabisa
unaona kuwa hatimaye Utawala wa Ulimwengu huu unawekwa chini ya Yesu Ufunuo 11:15 (hii itatokea hivi KARIBUNI, kwanza NB 2029 ndiyo inatimia MIAKA 2000 Tangu Ulimwengu umjue MESIHA). UKISOMA UFUNUO 20:10 Shetani atupwa ziwa la moto; UFUNUO 20:14 Inasema ni kifo Cha MILELE.
Baada ya hayo sasa ndiyo Jehovah ktk Ufunuo 21:3 inasema ndiyo Ile hali ya mwazo itarudi" Jehovah atakuwa pamoja na Wanadamu, yaani watakuwa chini ya utawala wake" MATOKEO yatakuwa- wanadamu hawatakuwa na maombolezo, maumivu na kakutakuwa na KIFO tena😀😀 soma Ufunuo 21: 4
NB NINAYOSEMA HAYA YOTE YAKO KWENYE BIBLIA JAMANI SOMENI HIKI KITABU, KWANI TUNAISHI (on borrowed times) na mambo yaliyotabiriwa kwenye biblia yanatimia kwa kasi isiyoyakawaida
Hata biblia yenyewe haipaswi kuaminika,i have a reason,so whenever we say GOD we mean yehova?
 
Miongoni mwa maswali najiuliza kila uchwao ni kwanini Mungu aliitwa Mungu na sio jina lingine?,Ni nani alimpatia hilo jina? Na kama yupo alikuwa nani?

Kwanini Mungu hakummaliza shetani hukohuko kama kweli ni muharibifu? kiasi kwamba anatuletea tabu ambazo tunaamini yeye ni chanzo? na anashindwaje kumuangamiza hata sasa ili hali hakuna anachondwa?
Mbona ana majina mengi tu mkuu
 
Mungu anayo majina mengine mengi kulingana na lugha, tamaduni na kabila.. Hivyo Mungu hana jina MOJA

1. ADONAI-Mungu Mwenye Enzi Yote Mwanzo 15:2-8

2. EL – SHADAI-Mungu ututoshelezae/Mungu mtoshelezi
Mwanzo 17:1

3.EL-OHEENU- Bwana Mungu Wetu Zaburi 99:5,8,9

4. EL- GIBBOR- Mungu Mwenye Nguvu, Isaya 9:6-9

5. EL-OHEEKA- Bwana Mungu Wako Kut 20:2,5,7

6. EL-ELYON -Mungu Aliye Juu Sana Mwanzo 14:18

7. EL-OHIM- Muumbaji wa Milele Mwa 1:1

8. YEHOVA- SABAOTH Bwana wa Majeshi 1Samwel 1:3

9. JEHOVA TSIDKEMU -Bwana ni Haki Yetu Yeremia 23:6

10. JEHOVA RAPHA- Mungu Atuponyae,kutoka 15:26

11. JEHOVA MEKADDISHKEM- Mungu atutakasaye Kutoka 31:13

12. JEHOVA ROHI-Bwana Mchungaji Wangu Zaburi 23:1

13. JEHOVA JIREH- Mungu Atupaye /Atoaye Mwanzo 22:14

14. JEHOVA HOSEENU -Bwana Aliyetuumba Zaburi 95:6

15. JEHOVA NISSI- Bwana ni Beramu (Bendera)
yangu
Kutoka17:15

16. JEHOVA SHALOM -Bwana ni Amani, waamuzi 6:24

17. JEHOVA SHAMMAH -Bwana Yupo Hapa, Ezekiel 48:35

18.El-hai-Mungu aliyehai,Joshua 3:10,1 Samwel 17:26

19.El-elohe-israel-Mungu wa Israel, Mwanzoh 33:20

20.El-Olam-Mungu wa milele,Ufunuo 4:8,kutoka 3:14

Majina haya yapo katika Lugha za kiebrania

Shetani sio mwili ni roho na roho ikizaliwa haifi
Mshana Jr kwa mtiririko huu wewe ni Mganga wa kienyeji kweli?
Au umekopi huu mtiririko mahali?
 
Miongoni mwa maswali najiuliza kila uchwao ni kwanini Mungu aliitwa Mungu na sio jina lingine?,Ni nani alimpatia hilo jina? Na kama yupo alikuwa nani?

Kwanini Mungu hakummaliza shetani hukohuko kama kweli ni muharibifu? kiasi kwamba anatuletea tabu ambazo tunaamini yeye ni chanzo? na anashindwaje kumuangamiza hata sasa ili hali hakuna anachondwa?
Na mimi nasubiri jibu kwanini shetani aliachwa?
 
Miongoni mwa maswali najiuliza kila uchwao ni kwanini Mungu aliitwa Mungu na sio jina lingine?,Ni nani alimpatia hilo jina? Na kama yupo alikuwa nani?

Kwanini Mungu hakummaliza shetani hukohuko kama kweli ni muharibifu? kiasi kwamba anatuletea tabu ambazo tunaamini yeye ni chanzo? na anashindwaje kumuangamiza hata sasa ili hali hakuna anachondwa?
Mungu yupo nje ya time dimension.

So kifupi haeleweki na hatokaa aeleweke.

Ukitakaa uwe kichaa endelea kutaka kumwelewa.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom