Kwanini mume akifa ndugu wanadai maliza marehemu na si ndugu wa mke??je hawana haki ya kudai nao??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini mume akifa ndugu wanadai maliza marehemu na si ndugu wa mke??je hawana haki ya kudai nao???

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jan 24, 2012.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,485
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  KWANINI MWANAMUME AKIFA NDUGU WA MWANAMUME WANADAI MALI ZA MTOTO WAO HATA KAMA ANA WATOTO KWA NINI NDUGU WA MWANAMKE HAWANA HAKI YA KUDAI?
  Mimi ni mwanamke niliyeolewa nimekuwa nikiona matukio mengi hasa upande mmoja wao anapoitwa mbele za haki na Baba yetu wa Mbinguni. Nitaongelea upande wa mwanamume mara nyingi nimekuwa nikiona tofauti sana na kujiuliza ni kwanini inakuwa hivyo?

  Ikitokea mwanamume akafa utakuta ndugu wa waupande wa mwanamume wanaanza kudai mali alizochuma ndugu yao hata kama ana watoto na mke aliyebaki hawaangalii hilo wao ni mali tu sababu mtoto wao ndo alikuwa mtafutaji. Hawakumbuki kuwa wakati wanatafuta hizo mali alikuwa na mke wake wanashauliana saa nyingine wanajima vitu Fulani Fulani ili wawe na maendeleo kama watu wengine. Chakushangaza mke athaminiwe tena hasa akiwa na watoto wadogo ndo basi make wakiwa wakubwa kunakuwa na hofu kidogo lakini maneno hayatakosa, utakuta wakati wanaoana walikuwa hawana kitu hata kimoja lakini wakajibana wakapambana na maisha wakawa na kitu kidogo lakini walijibanaje wanajua wao hasa mama na baba sasa kwa nini inapotokea baba akaondoka kunakuwa na vurugu hasa kuhusu mali?
  Niongelee tena upande wa mwanamke inapotokea mama ameitwa mbele ya haki kwanini ndugu upande wa mwanamke hawana haki ya kudai mali ya mtoto wao aliyochuma na mume wake? Sababu mali alizobaki nazo mwanamume zilitafutwa na wote wawili sasa kwa nini haki iende upande mmoja? Naomba kujua hilo toka kwa wadau. Ikumbukwe mwanamke anapokufa baba ana haki ya kuoa mke mwingine na kumuolea kwenye nyumba aliyojenga na mke wa kwanza na wakaendelea na maisha lakini anapokufa baba mwanamke haruhusiwi kumiliki tena mali za mume wa kwanza kwa nini? Na tujue asilimia ya wengi hasa mama akifa wa kwanza watoto huwa wanapata shida sana na utakuta matunzo ya watoto yanaegemea upande wa mama tofauti na upande wa baba na utakuta watoto wanadhulumiwa hasa na upande wa baba ni kwanini?
  Mimi nashauri wanapotunga katiba nahili waliangalie hasa upande wa mwanamke wawe na haki ya kudai mali endapo mtoto wao ametangulia
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  kwani africa mtafutaji wa nyumbani ni nani?
  Au wewe ni mgeni wa Yerusalemu hii??
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,485
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  Na wale wanaume wanaoishi nyumba za wanawake wako jehanum mpwa??
  Aisee embu watake radhi wanaume aiseee
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ni tabia za kijinga sana, nakumbuka nikiwa mdogo baba yangu alipofariki, shangazi zangu na baba wadogo wakawa wanagombania mali zetu na mdingi wangu mdogo akawa anamng'ang'ania mama amrithi, nilishuhudia mama akitandika wifi zake makonde ya nguvu na kuwaburuza mahakamani.
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,485
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  heri ya wewe
  mjomba wangu alikufa ati msiban mamazangu wadogo wakachukua madaraka ya kudai mali za kkakayao
  nikwambie malipo hapa hapa duniani..wakamsumbua sana sana mama alikuwa shirika mpoja la haki za binadamu
  akawasakazia wanasheria wakasimama na shangazi mpaka akashinda walivyo wajinga wakamfwata wakamwomba msmaha
  ati wakamtumia babu yetu kwamba anaomba gari moja haata asipate shida kule moshi
  Najua wengine wangewatoa resi ..mjomba alikuwa na gari 7//benzi 3 na mengineyo
  akamwambia mamayangu wacha nimpe gari huyu babayenu aakasema bado wanakufwata akasema wamekuja nae wanaomba gari la kutembelea..akamwomba maza na ndugu wengine waje jumapili...unajua alichofanya ..akapika safiiiiiiiii akawekakwaya yake akaweka
  tv zake mbili yaani ya sebulen na chumban ..akawa anaonyesha movie ya msiba wa mjomba walipojaa wengi akaomba utulivu akasema mumewe amekuwa na msaada kwa babake na mamake tangu akiwa ajanioa..akasema na hili nitaendeleza mpaka mungu atakapomchukua...aunt akaamka akaomba babu na wengineo wafwatane akasema mahakamani wameandika magari 7 labda mliemtuma
  kuja kuangalia akujua ama akutaka hesabu nzuri kutoka kwangu ziko nane...naomba babamkwe chagua unayotaka kuanza kushoto mpaka kulia moja...ama kutoka kulia kwenda kushoto...mumy akaita lawyers wakakaa sawa mzee wetu akaenda kwenye Benzi..ndugu wengine wakaanza kupiga keleleee yeye akasema mi si ndio nimehalalalishwa mahakamani .mi sindie nimewaita ,mi sindienimemwomba aende kuchagua naomba chaguo la babu liheshimiwe........

  Ndugu zanguni yule babu akapelekwa kwa ndege Moshi..muda akaaambiwa gari linakuja linakuja kumbe watoto wakaanza kutafuta mteja ....yule babu akaanza kupiga kelele kwa aunt naomba waambie hao wattoto walete hiyo gari akasema mzee huko nishatoka waambie wao ndio waliochukua...Mzee akatangaza isipofika sisku fulan yaani babamkwe analaani mtu akatokea mtoto mmoja alikuwa kishelu kweliiiiikweliiiiiiiiii kwenye kudai mali Mungu amrehemu alipo uko..akachukua kuipeleka MOSHI
  Aliishia pale same ..kabla ujafika same kabisa kuna sehemu kuna kaupepo kweli kweli jamaa akapigwa ikazunguka ile gari kama chapati
  kuitoa waanagalie bima imeisha jana yake yaani siku iliomzunguka

  Kama mwana JF OGOPA SANA KUDAI ZA MAREHEMU ALIEACHA WATOTO LOH
   
 6. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Yani mijitu mingine haitaki kujishughulisha inasubiri ndugu afe ikadai mali, PUMBAVU ZAO
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Ukikubali vya kurithi basi ukifa vyako vitarithiwa..........muhimu wanaume kuwashirikisha wake zao....wengi wetu hupenda ku-share info za mali na ndugu zeo wakati mwingine hata mke au watoto hawajui kitu....ukifa wanazijua na wanajua zilipo..kina mama na nyie muwache mbwembwe wakati waume zenu wako hai
   
 8. MWAMUNU

  MWAMUNU JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 661
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mi nafikiri hii inasababishwa na ndoa isiyo thabiti !
  Hapa namaanisha nini unakuta katika ndoa mume na mke wanaishi kama paka na panya ( they don't trust each other ) mwisho wa wa siku baba anakufa bila kuacha mwongozo mzuri.Kumbe kuna baadhi ya ndoa zenye furaha na upendo unakuta baba akiwa bado hai anahakikisha kila kitu kinakuwa writen,kiasi kwamba hata hao ndugu wanashindwa kuingilia.
  Pia kuna kitu ambacho huwatia hofu wanaume wengi ,unakuta jamaa amekufa hata miezi sita haijapita
  Bi mkubwa anaanza mahusiano mapya, hii huchangia wanandugu kupata mwanya wa kujisogeza kwa mgongo wa kutunza mali zisipotee !!!
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Akina marioo ni wanamme????

   
 10. M

  MUMY A JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 234
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  halafu hiyo mindugu ya mwanaume haina hata haya,wengine hawajui hizo mali mmezipataje,ndo mana huwa mara nyingi zinawatokeaga puani..................
   
 11. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Qumbe Pdidy wamekuwowa? Nilikuwa sijui ati...
   
 12. piper

  piper JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kama mke alimtolea mume mahari basi ndugu wa mke wadai mali ndugu yao akifariki, makabila mengi Tanzania ni Patrilineal (upande wa baba) na siyo mama, kwasababu nafikiri jina lako la ukoo litakuwa la upande wa baba na siyo ujombani (unless u'r matrilineal) anyway kabila langu hatuchukui hata kijiko labda mfiwa awape.
   
 13. Anita Baby

  Anita Baby JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 1,203
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  Co ndugu wa mwanaume 2! Mama angu alifariki ha2jaambulia hata sent moja ya mirathi wala ki2 hata kimoja kati ya alivyokua navyo. Na ma2si ju 2kapewa.
   
Loading...