Kwanini mtuibie?

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,737
5,438
Kwa nini utuibie?

Rais. Unalipwa mshahara mkubwa kuliko mtumishi yeyote wa umma, unalipwa marupurupu kibao; ukistaafu utaendelea kutibiwa bure ndani na nje ya nchi, utalipwa 80% ya mshahara wa rais kipindi chote cha uhai wako na au mwenzi wako, utalipwa kiinua mgongo kinono mno baada ya kuondoka madarakani.

Kwa nini utuibie? Kwa nini utuingize kwenye mikataba ya hovyo ya kimagumashi?

Waziri. Unalipwa mshahara mnono kuliko watumishi wote ndani ya wizara yako. Unalipwa posho za vikao na per diem za kutosha unapofanya ziara ndani na nje ya nchi, unalipwa posho ya shilkingi laki 3 kila siku unspokuwa Bungeni. Utalipwa kiinua mgongo cha kutosha kama mtumishi wa umma na ukiwa kama mbunge utalipwa 200m baada ya miaka 5 (maana yake unalipwa kiinua mgongo mara mbili).

Kwa nini utuibie? Kwa nini utuingize kwenye mikataba ya kimagumashi na ya hovyo na hivyo kulitia hasara taifa letu?

Mbunge. Unalipwa mshahara na marupurupu kibao kila mwezi yapata 12m. Unalipwa posho ya shilingi laki 3 kila siku uwapo kwenye kikao cha Bunge. Unalipwa kiinua mgongo cha shilingi milioni 200 baada ya miaka 5 cha ubunge, kiwango ambacho hakuna mtumishi yeyote wa umma anapata hata baada ya utumishi wake wa miaka 30!

Kwa nini utuibie? Kwa nini hutimizi wajibu tuliokutuma wa kuisinamia serikali isiingie mikataba ya hovyo na kuthibiti matumizi mabaya ya fedha zetu? Kwa nini mtuibie?

Vv
 
IMG-20220108-WA0017.jpg
 
Bora hata wangetuibia wao wenyewe tungejua ni tamaa tu ya pesa. Yan wanapanga kabisa na wazungu/ wachina kutuibia. Yaan baba anapanga na majirani jinsi ya kuwaibia watoto wake. Huwa nasema siku zote kwamba sio kwamba wazungu wote wanaakili sana Bali wapo wachache wanaochaguliwa viongozi wanajitoa kwa ajili ya wengine. Hapa Africa tunakuchagua tupo hukoo namtumbo ukiniambia huko kwa waarabu pipa Moja la mafuta ni usdolaar kadhaa, Yan hata ukubwa wa hilo pipa hatujui ni kiasi gan Sasa kwann mnashindwa kujitoa kwa ajili yetu tusiojua na tumewaamini?
 
Tatizo ni 10%..

Kitu ambacho huwa kinaniacha na maswali viongozi wa idara, wakurugenzi hawawezi tumia gari tofauti na v8 katika shughuli zao
 
Shida hawaridhiki na walivyonavyo,ubinafsi umewajaa sanaa ndio maana mwanasiasa akipata nafasi kubwa anaanza kuangalia kwao kwanza.

Tizama wanavyojiwekea kinga kila mahali kulinda maslahi yao,wanajua nje ya ulingo wa siasa hawana lolotee.
Angalia wanasiasa waliovuliwa vyeo vyako,wakirudi mtaani wanageuka ombaomba.
 
Tena wanashindana kuiba na kupiga deal ndefu. Kwa nje na suti zao wanaonekana wa maana sana, lakini behind doors ni zaidi ya mashetani wanyonya m@&%*i.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom