Kwanini mtu akiwa hana hela anakuwa na mipango mingi mikubwa lakini akipata hela mipango huyeyuka ghafla?

Fantastic boy

Member
May 10, 2022
15
15
Hivi ni kwanini binadamu wengi wao, wakiwa hawana pesa huwa na ndoto za kila aina na zenye kuonyesha mtu huyu future yake ni sahihi na kubwa zaidi...!!

Lakini 'mfano' baada ya kuipata pesa ndoto zile hutoweka kwa kasi sana bila ya kutimizwa kama ilivyokuwa awali akifikiria?

Naombeni mnisaidie wanafamilia
#i'm fantastic boy
 
Hivi ni kwanini binadamu wengi wao, wakiwa hawana pesa huwa na ndoto za kila aina na zenye kuonyesha mtu huyu future yake ni sahihi na kubwa zaidi...!!

Lakini 'mfano' baada ya kuipata pesa ndoto zile hutoweka kwa kasi sana bila ya kutimizwa kama ilivyokuwa awali akifikiria?

Naombeni mnisaidie wanafamilia
#i'm fantastic boy
Baada ya kazi ngumu lazima tujipongeze,hapo ndipo tunaposahau malengo yetu tukipata.
 
Andika malengo yako yote hata kabla ya kutokuwa na kitu na baada ya kupata HAKIKISHA uliyo yaandika unayatimiza kama ulivyo yaandika mwanzo.

Usiingize visingizio vyovyote vile mpaka uhakikishe umeyatimiza.

Tengeneza mazingira ya kuona bado kuna vitu unavikosa katika maisha mpaka pale malengo yako ya mwanzo yote yatapotimia.

Ukishindwa kufanya hivyo, basi malengo hayo hayakutoka ndani ya moyo ila zilikuwa ni hisia zako tu kwasababu ya upweke wako.

Malengo dhabiti yaliyo ndani ya moyo wa mtu huwa ni ngumu kulala kwa amani kabla hajayatimiza.

Lakini katika yote kumbuka kadiri ya unavyo panda juu kimaisha ndivyo unavyokutana na ulimwengu mpya wenye mambo tofauti na ulimwengu uliokuwa mwanzo, hivyo unahitaji jitiada zaidi ili kuunganisha malengo uliyojiwekea katika ulimwengu wa mwanzo ili kuyatimiza katika ulimwengu mpya uliopo.

New level, New devil.
 
Hivi ni kwanini binadamu wengi wao, wakiwa hawana pesa huwa na ndoto za kila aina na zenye kuonyesha mtu huyu future yake ni sahihi na kubwa zaidi...!!

Lakini 'mfano' baada ya kuipata pesa ndoto zile hutoweka kwa kasi sana bila ya kutimizwa kama ilivyokuwa awali akifikiria?

Naombeni mnisaidie wanafamilia
#i'm fantastic boy
Tafuta maarifa ya kupanga,

kupanga siyo tu kuwaza nitauza magari, nitauza kompyuta, nitalima nyanya, nitafuga kuku.

ukiwa na mpango uliokamilika, ukipata hela unatekeleza lakini usipokuwa na mpango uliokamilika ndipo ukipata hela kila unachojaribu kushika unaona hakishikiki.

kama ni mpango wa kufuga kuku,
jiulize unataka kufuga ili iweje, labda ujasiliamali, sasa jiulize unalenga kupata pesa kiasi gani kwa mda gani? labda unataka laki 5 kwa mwezi, jiulize soko la kuku utalipata wapi? hapa anza kuuliza masoko ya kuku na utagundua ni kuku wa aina gani ufuge. Jiulize kwa aina hiyo uliyochagua je ufuge kuku wangapi ili kupata faida ya laki 5?

hapa utafanya mahesabu kulingana na ulivyoambiwa sokoni bei na gharama za kufuga.

hapo utajiuliza je unahitaji mtaji kiasi gani kufanya huo mradi, utapiga gharama za banda, kununua kuku wenyewe, matunzo kama chakula na madawa na mengineyo.

hapo utajiuliza je unaweza kupata pesa hiyo na kwa njia gani?

huo ndo mpango wa kufuga kuku unajua kila kitu.

sasa ukiwa na kitu kama hicho alafu ukapata pesa hiyo na usifanye basi utakuwa na matatizo.

ila kwa wengi kitu tunachokiita mipango siyo mipango na ndiyo maana tukipata pesa tunakosa cha kufanya.

tunachokiita mipango ni kusema nitafuga kuku nasikia kuku wanalipa, hujui gharama, hujui masoko, hujui mahitaji na sasa unapopata pesa ndipo unaanza kufanya mchanganuo na kugundua pesa uliyo nayo ama haitoshi au unaogopa changamoto.

KAJIFUNZE JINSI YA KUPANGA NDIPO UKIPATA PESA UTAPATA CHA KUFANYA
 
Yeah this real happen ndo maskin hua tunajiona tuna malengo ya maana kushnda walionazo the way wanavyozitumia mfano ukimwangalia diamond ana push ride ya 2.2Bil (milion 2000 na milion 200) kwa harak harak haikuingii wew akilin kufany huo ujing hata kama ukipew hio hela unaona kuna vitu ving vya maana vya kufanyia io pesa but ndo ivo huez jua ukiipata inakuaje ndo kama ivo unajikuta inayeyuka

inshort kua na mipango na msimamo kabla hujaitia mkononi
Eti uishke mkonon ndo uanze kupanga umekwisha.. uliza walioshnda bet 🥹
 
Back
Top Bottom