Kwanini mto Wami na Ruvu maji hayakauki?

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
4,291
2,466
Wala Sioni Yakipungua. Ukitazama Mikoa Ya Kaskazini Ambayo Miaka 10 Iliyopita Mito Yake Ilijaa Maji, Tena Yale Masafi. Leo Yamebaki Mabonde Makubwa Na Mawe Kibao Na Maji Kiduchu Kama Ya Mfereji. Hii Mito Ya Huku Pwani Inanishangaza Maana Haina Jiwe Hata Moja, Na Maji Yake Yamejaa Udongo Kiasi Huoni Kina Cha Maji. Sababu Ya Hii Mito Kutokauka Ni Nini? Na Ile Mingine Ifanyweje Isikauke?
 
Mito iyo ina connection nyingi yaani inaanzia mbali. Inatoka ktk milima na misitu mikubwa.... Inakusany maji toka mito midogo na inamwaga baharini...
 
Baadhu ya sehemu mito inakauka sababu watu wanalima ndani ya mita 60 toka vyanzo vya maji afu wakiambiwa waache wanatetewa kuwa wanazuiwa kwa sababu za kisiasa ngoja ikauke afu wasingizie mito imekaushwa
 
Ngoja siku utakayoshuhudia nayo imebaki michanga magogo yaliyooza, ndipo utakapoanza kulia kwa masikitiko.

Ni swala la muda tu.
 
Labda sababu inapokea maji kutoka vyanzo vingi vya maji na pia wingi wa misitu.
 
Pwani ndio mwisho wa mito mingi kwa sababu ndipo inapoingilia baharini.

Mito mingi inakuwa midogo midogo inapokuwa huko mbali lakini inapokaribia kuingia baharini huungana na kuwa mito mikubwa na kutengeneza mikondo isiyokauka.

Mto kama Rufiji huwa unapungua sana maji wakati wa kiangazi na bonde linabai tupu sana, ila wakati wa masika huwa unajaa kweli kweli mpaka unaweza kuogopa kupita pale, lakini ukiuchunguza Rufiji mwanzo kabisa unakotokea kama mto Ruaha utaukuta unaanzia mbali kweli kweli ukiwa mdogo ila kadri unavyosogea ndivyo unazidi kuunganisha mifereji mingine na kutengeneza mto mmoja unaoonekana mkubwa sana kwa kadri unavyosogea baharini.

Vivyo hivyo kwa mito mikubwa kama Kagera na mto Mara inayomwaga maji yake ziwani Victoria.
Mito hii ikiwa mbali na ziwa huwa midogo sana na maji yake huwa si mengi, ila kadiri inavyokaribia ziwani huwa mikubwa sana kwa sababu ya mito midogo midogo kuunga tera na kutengeneza mto mmoja mkubwa kabla ya kuingia ziwani.
 
Wala Sioni Yakipungua. Ukitazama Mikoa Ya Kaskazini Ambayo Miaka 10 Iliyopita Mito Yake Ilijaa Maji, Tena Yale Masafi. Leo Yamebaki Mabonde Makubwa Na Mawe Kibao Na Maji Kiduchu Kama Ya Mfereji. Hii Mito Ya Huku Pwani Inanishangaza Maana Haina Jiwe Hata Moja, Na Maji Yake Yamejaa Udongo Kiasi Huoni Kina Cha Maji. Sababu Ya Hii Mito Kutokauka Ni Nini? Na Ile Mingine Ifanyweje Isikauke?
Umefuatilia vyanzo vyake?
 
Kione hiki nacho mxiuuuu

Qur'an 2:25
Na wabashirie walio amini na wakatenda mema kwamba watapata mabustani yapitayo mito kati yake; kila watapo pewa matunda humo, watasema: Haya ndiyo kama tuliyo pewa mbele. Na wataletewa matunda yaliyo fanana; na humo watakuwa na wake walio takasika ; na wao humo watadumu.
Maelezo
 
Wala Sioni Yakipungua. Ukitazama Mikoa Ya Kaskazini Ambayo Miaka 10 Iliyopita Mito Yake Ilijaa Maji, Tena Yale Masafi. Leo Yamebaki Mabonde Makubwa Na Mawe Kibao Na Maji Kiduchu Kama Ya Mfereji. Hii Mito Ya Huku Pwani Inanishangaza Maana Haina Jiwe Hata Moja, Na Maji Yake Yamejaa Udongo Kiasi Huoni Kina Cha Maji. Sababu Ya Hii Mito Kutokauka Ni Nini? Na Ile Mingine Ifanyweje Isikauke?
Kama ulisoma Jiografia basi ndio maana yule dada Faiza anasema shule mlienda kusoma ujinga.

Unajua wazi Ruvu na Wami zimekusanya vijito hivyo vidogo vyote inapeleka baharini unafananisha na sehemu ya miinuko
 
Wala Sioni Yakipungua. Ukitazama Mikoa Ya Kaskazini Ambayo Miaka 10 Iliyopita Mito Yake Ilijaa Maji, Tena Yale Masafi. Leo Yamebaki Mabonde Makubwa Na Mawe Kibao Na Maji Kiduchu Kama Ya Mfereji. Hii Mito Ya Huku Pwani Inanishangaza Maana Haina Jiwe Hata Moja, Na Maji Yake Yamejaa Udongo Kiasi Huoni Kina Cha Maji. Sababu Ya Hii Mito Kutokauka Ni Nini? Na Ile Mingine Ifanyweje Isikauke?
Kijiografia, mto wami na ruvu almost inaanzia sehemu moja na inaenda kumwaga maji karibu karibu kabisa baharini

Hii mito yote ipo kwenye mamlaka ya bonde la ruvu

Mito hii huanzia kwenye milima ya uluguru, morogoro

Asilimia kubwa ya maji yanayotumiwa dar kwa matumizi ya viwandani na majumbani yanatoka mto ruvu, nadhani hapa utapata ni sababu gani zinazofanya bonde la mto ruvu litunzwe vizuri
 
Nakubaliana na faizafoxy huwa mnaenda shule kusomea ujinga utaulizeje swali la namna hii aisee?
 
Back
Top Bottom