MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,801
kwanza kimaadili tu ya kiuandishi wa habari huyu mtangazaji wa efm maulid kitenge huwa anakiuka kila siku au kila kukicha hasa katika uendeshaji wa vipindi vyake vya michezo awapo redioni. kwa wabobezi wa masuala ya media watanielewa nasema nini. huyu mtangazaji siku zote amekuwa akipenda sana kutafuta taarifa za habari za kiuchochezi zinazoihusu klabu ya Simba Sports Club tu pekee kana kwamba katika vilabu vingine ( tena hasa ile anayoipenda kupita kiasi ya Yanga F.C ) hakuna matatizo. Mtangazaji huyu tunajua kuwa ni mnazi wa kutupwa wa klabu ya Yanga F.C lakini mara kwa mara huwa anakwenda kinyume sana na maadili au taratibu za kiutangazaji na kama asiporekebishwa naogopa ipo siku atakuja kuleta uchochezi mkubwa utakaopelekea chuki baina yake yeye na wana Simba S.C au hata baina ya hizi timu mbili kubwa.
mfano mdogo tu tokea wiki iliyopita huyu mtangazaji amekuwa akihangaika kutafuta taarifa ya nia ya bilionea mo dewji kutaka kuinunua Simba S.C na jana tu amekuja na taarifa ya kupika yeye mwenyewe na akaitengeneza kuwa tajiri mo dewji ameipa Simba S.C ULTIMATUM ya kuamua kama watamuuzia klabu au hapana kitu ambacho kimeleta sana sintofahamu hasa kwa mustakabali wa suala lenyewe. kinachosikitisha kama siyo kushangaza wengi ni kwamba huyu huyu mtangazaji maulid kitenge anajua fika kuwa kuna mchezo mchafu tena wa kikatiba unafanyika ndani ya klabu yake ya pendwa ya Yanga F.C na yapo " madudu " chungu nzima yanaendelea ndani ya klabu hiyo ya Yanga lakini hata hathubutu kujishughulisha kutaka kuileta hiyo habari kwa walaji wake lakini amkekuwa na tabia za " kipashkuna " tu dhidi ya klabu ya Simba S.C.
kama vipi basi uongozi wa efm watuambie kuwa hiyo redio yao ni mali ya Yanga F.C tu na kwamba 75% ya maudhui yake ni kuisema kama siyo kuisimanga tu klabu ya Simba S.C. maulid kitenge asipojirekebisha ataiathiri sana efm na kuishusha thamani mbele ya walaji. moja wa kanuni kuu ya mtangazji yoyote wa redio au runinga ni kuwa " objective " au " neutral " lakini si kwa kitenge na ukitaka kulithibitisha hili tegea akiwa anawasilisha taarifa mbaya ya kuihusu klabu ya Simba S.C utagundua kuwa huwa na furaha na uchangamfu usio na kifani lakini kukiwa na taarifa mbaya ya kuihusu klabu yake pendwa ya Yanga F.C utaona anavyokosa raha na kuhangaika kuwatafuta sources mbali mbali wa Yanga huku akiwauliza maswali elekezi ambayo yataleta " harmony " ndani ya Yanga F.C.
nina mengi ila kwa kuanzia leo naomba niishie tu hapa na huyu mtangazaji maulid kitenge anatakiwa apigwe msasa upya aendane na utangazaji wa kisasa uliojaa ueledi na aachane na " utoto " na ushabiki wa " maji tope " kwani hautamsaidia zaidi tu ya kumshusha thamani kwa wenye ueledi na hiyo tasnia yake.