Kwanini Mtangayika haruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar wakati Mzanzibari anamiliki ardhi Tanganyika?

Nyie watu hamchoki na mijadala feki? Mtanzania yoyote anaweza kuwa Mzanzibari akiamua inatakiwa akae Zanzibar kwa miaka 5 tu atapata Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi. Maraisi 3 wa Zanzibar wana uhusiano wa moja kwa moja na Tanganyika. Mhe. Aboud Jumbe kwao ni Mji mwema na maekuwa Rais wa Zanzibar 1972 hadi 1984, Mhe Mwinyi wazazi wake wote wamezali Tanzania Bara na amekuwa Rais wa Zanzibar 1984 na Rais wa sasa Baba yake hakuwa Mzanzibar wa kuzaliwa na Rais wa Zanzibar. Hata wewe ulieleta hii mada ukuhamia Zanzibar leo upo uwezekano na kuwa Rais miaka 10 ijayo. Ikiwa uraisi unawezekana ardhi ni nini?. Wacheni fitina na uchonganishi
 
Aliyekua anahtaji muungano alikua Tanganyika(nyerere)
Sidhani kama karume(Zanzibar)alimfata Tanganyika(nyerere) kutaka muungano pengine hiyo ilipelekea makubaliano uchwara kama hayo
 
Muungano hatuvunji, tutawashikilia hivi hivi mpaka kakisiwa kazame. Tukihakikisha kamezama tuna wagawana tutawapeleka Mara, Shinyanga, Tabora,Morogoro, Kyela mkapigishwe kazi mpaka UN na Uarabuni waingilie kati. Hao walio nunua vi-Ardhi huku bara tutawakamata wote na kuwaunganisha huko utumwani mkapige kazi za kulima na kufuga kwa ujira duni. Mtakubali tu kudadeki
 
Ukisema wengi sidhani kama utakuwa sahihi na pengine Haujawahi kutafuta ardhi Zanzibar ukiwa umetokea bara au bongo kama wao wanavoita. Unaweza kuwa na hela na kila kitu na kuna MTU tayari ameamua kukuuzia kiwanja, umefuata taratibu zote na ukamilikishwa subiri siku utakapoanza kujenga hapo ndo utaijua unguja na waunguja.
Naamini wapo waliojenga lakini bado wanachangamoto haziishi, kuna jamaa alijenga nyumba na Mhaya baada ya kuamia kila siku ikawa majirani wanakuja mara huyu kaja kuomba kiberiti, mara chumvi, mara sabuni nk. Na akiangalia hao watu wanaokuja kuomba hawana sababu ya kufanya hivo, akaamua kujenga ukuta ikawa Shida pia.
Zanzibar mzanzibar anaweza kuwa anamiliki bar au club lakini wewe ukijenga pembeni yake utaambiwa hii ni nchi ya kiislamu.
Zanzibar tafuta hela kajenge Dar hata kama utafanikiwa kujenga huwezi kuishi Kwa Amani.
Hata kama sheria itakuruhusu hawa jamaa wanavitimbi kuliko kawaida Mimi nimeishi Sana Zanzibar ni Bora MTU yeyote kutoka nje ya Tanzania anaweza kufanya vitu Kwa wepesi kuliko ww wa kutoka bara
Itakua uliishi mitaa ambayo iko kama buza, nakwambia tena wapo ambao wamejenga na wanafamily na wanaishi fresh tu hakuna tatizo, labda ww mwenyewe ulikua mbaguzi kutokana na dini yako, hakuna sehemu yyte yenye amani kama znz, hakuna sehem yyt tz yenye watu wakarimu kama znz
 
Tanganyika tunafaudika nini na huu Muungano?..kuna mtu alisema ni kwa ajili ya kiusalama..lakini kwangu mimi bado haiku-make sense.
 
Itakua uliishi mitaa ambayo iko kama buza, nakwambia tena wapo ambao wamejenga na wanafamily na wanaishi fresh tu hakuna tatizo, labda ww mwenyewe ulikua mbaguzi kutokana na dini yako, hakuna sehemu yyte yenye amani kama znz, hakuna sehem yyt tz yenye watu wakarimu kama znz
Wadanyanye wasiyojua naijua Unguja Kwa zaidi ya unavodhani, anzia kitope, kinyasini, mfenesini, pwani mchangani mpaka Nungwi, njoo stone town, magomeni, kisiwani, uwanja WA ndege, kariakoo, mwembe Radu, Amani, kwerekwe, Kwa ndundu, Fuoni, tunguu, Pete, Unguja ukuu, jozani, kizimkazi, makunduchi, paje, bwejuu, michamvi.
Kutaja chache nambie hiyo Unguja ambayo mbongo atamiliki ardhi bila zengwe ni ipi? Wapo wanamiliki lakini wanamiliki kibishi tofauti na waunguja na wapemba wanamiliki ardhi bara. Kuna watu kibao na marafiki zangu wameamua kusalimu amri na kuacha uwekazaji WA mamilioni. Chukuwa hata mche bara kama utaingia nao Zanzibar kirahisi, chukuwa hata ndizi mbivu kama utaingia nayo Zanzibar. Lakini hivo nikivovitaja chukuwa znz kuja bara kama kuna MTU atakuuliza.
Jutetee kivingine lakini ni ninyi ni wabaguzi, mkikosa WA bara utasikia huyu wa mbambi, huyu wa mtende, huyu wa bwejuu, huyu wa michamvi. Niambie kama MTU wa kizimkazi anaweza kwenda via jambiani, au bwejuu, michamvi na kinyume chake akarudi salama kesho yake? Njoo huku bara kama unachombo kavue popote ili mradi Una leseni na nyavu sahihi.
Zanzibar ukanda wote wa mahotel ya kitalii nimeishi. Mfano mwingine MTU wa bara anunue Costa aiweke barabarani kama daladala aone kama atafanya biashara, njoo Dar wanzanzibar wangapi wanamiliki daladala?
Mkuu Bora unyamaze Tu muendelee kuufaidi muungano
 
Wakuu waliotunga Sheria ya Mtanganyika kutoruhusiwa kumliki ardhi Zanzibar wakati wazanzibar wanarusiwa kumliki ardhi Bara waliwaza nini?

Kuna jamaa amekaa Zanzibar miaka miwili na kapata kiasi kadhaa akataka anunue eneo ajenge kibanda chake nje ya mji, amechoka maneno ya wenye nyumba. Cha ajabu kakosa kwa sababu za kijinga na ikanipelekea kujiuliza maswali mengi kwa kujua au kutojua swala yanayohusu Muungano.
  • Mtanganyika harusiwi kumiliki ardhi Zanzibar kisheria
  • Mtanganyika harusiwi kuwa na kitambulisho cha Mzanzibar mkazi
  • Pamoja na harufu ya kiubaguzi wa kidini ,inawekwa kwenye sababu ya kukosa ardhi (Jirani wa eneo alilotaka kununua jamaa katoa kauli ya kiubaguzi wa kidini nanukuu !! "huyu kafiri atajenganje karibu na sie").
Nimejiuliza kwanini Bara wazanzibari wanamliki ardhi bila vikwazo ?,nini maana ya Muungano,na hii kwa asilimia kubwa wazanzibari wanaofanyia kazi kwenye taasisi yanayohusu Muungano wanamliki ardhi Bara pamoja wafanya biashara.

Wanaojua Sheria watusaidie hapa naona Leo nitalala mabusu kwa haya sababu, na sanasana hiyo ya kiubaguzi,kwa kweli kauli ya kiubaguzi kinauma kuliko matusi.

Wazanzibari waliona mbali katka suala hili na ndio suala linalo waangaisha wapalestina kwa wayahudi.walona utamu wa kuuza ardhi yao kwa wayahudi sasa linawatokea puani.
Weka akilini kua kitu Muungano iko siku utavunjika siku ukivunjika na watanganyika kwa wingi wao wamehodhi Ardhi zazinbari itakuaje? wawe kama wapelestina ktk nchi yao?
 
Mimi nafikiri hayo yalikuwa mawazo ya Nyerere akifikiri kwa kuwapa upendeleo wazanzibar watakubali Serikali Moja!
 
Itakua uliishi mitaa ambayo iko kama buza, nakwambia tena wapo ambao wamejenga na wanafamily na wanaishi fresh tu hakuna tatizo, labda ww mwenyewe ulikua mbaguzi kutokana na dini yako, hakuna sehemu yyte yenye amani kama znz, hakuna sehem yyt tz yenye watu wakarimu kama znz

huyu itakua kaishi uswahilini halafu analeta lawama
 
Kwasababu Zanzibar ina katiba yake, pili ardhi kwao siyo jambo la muungano, tatu eneo la zanz ni dogo hivyo si vyema wasiyo wazanzibar kumiliki maana anaweza tokea bwege mmoja akainunua yote! Wapemba akawatimua wakaishi kwenye mitumbwi
Ha ha ha ha! Imebidi nicheke
 
Kwasababu Zanzibar ina katiba yake, pili ardhi kwao siyo jambo la muungano, tatu eneo la zanz ni dogo hivyo si vyema wasiyo wazanzibar kumiliki maana anaweza tokea bwege mmoja akainunua yote! Wapemba akawatimua wakaishi kwenye mitumbwi
Dah mkuu umenichekesha japo unapoint eti kwny mitumbwi kkkkk!!
 
Kuna pahala niliona ufafanuzi kuwa ardhi ya Znz ni ndogo, so Wadanganyika kwa kuwa ni wengi, wakiruhusiwa kumiliki huko wataimaliza yote fasta
Sheria huwa ni msumeno, hukata kuwili.

Iweje hiyo marufuku iwe kwa Zanzibar pekee na isiwe kwa bara kupiga marufuku waZanzibari kumiliki aridhi?

...'wataimaliza yote'..! Tafakuri za kijinga sana hizi.

Maana ya uhuru ni nini na lini ulisikia kila mTanganyika ana nia ya kwenda kununua aridhi na kuishi Zanzibar?

Sheria za hovyo na kibaguzi namna hii ambazo ni kero ndiyo zinazostahili kuangaliwa upya na kufumuliwa.
 
Population ya zanzibar hadi leo hii milion 3 hawajafika hapo ukijumlisha hadi na mbuzi. Wakiruhusu watu wa bara tununue tu wale jamaa watakosa pa kuishi. Sisi bara li nchi likubwa acha waje, ila uzur wazanzibar wengi viwanja wanamiliki kigamboni, ununio, msasani. Sehemu zenye bahar. Bado hawana effect
Hivi sijui kwanini watu huwa hatuwazi nje ya box!
 
Sheria huwa ni msumeno, hukata kuwili.

Iweje hiyo marufuku iwe kwa Zanzibar pekee na isiwe kwa bara kupiga marufuku waZanzibari kumiliki aridhi?

...'wataimaliza yote'..! Tafakuri za kijinga sana hizi.

Maana ya uhuru ni nini na lini ulisikia kila mTanganyika ana nia ya kwenda kununua aridhi na kuishi Zanzibar?

Sheria za hovyo na kibaguzi namna hii ambazo ni kero ndiyo zinazostahili kuangaliwa upya na kufumuliwa.
Mkuu, ndiyo maana tunataka Katiba mpya SASA
 
Wakuu waliotunga Sheria ya Mtanganyika kutoruhusiwa kumliki ardhi Zanzibar wakati wazanzibar wanarusiwa kumliki ardhi Bara waliwaza nini?

Kuna jamaa amekaa Zanzibar miaka miwili na kapata kiasi kadhaa akataka anunue eneo ajenge kibanda chake nje ya mji, amechoka maneno ya wenye nyumba. Cha ajabu kakosa kwa sababu za kijinga na ikanipelekea kujiuliza maswali mengi kwa kujua au kutojua swala yanayohusu Muungano.
  • Mtanganyika harusiwi kumiliki ardhi Zanzibar kisheria
  • Mtanganyika harusiwi kuwa na kitambulisho cha Mzanzibar mkazi
  • Pamoja na harufu ya kiubaguzi wa kidini ,inawekwa kwenye sababu ya kukosa ardhi (Jirani wa eneo alilotaka kununua jamaa katoa kauli ya kiubaguzi wa kidini nanukuu !! "huyu kafiri atajenganje karibu na sie").
Nimejiuliza kwanini Bara wazanzibari wanamliki ardhi bila vikwazo ?,nini maana ya Muungano,na hii kwa asilimia kubwa wazanzibari wanaofanyia kazi kwenye taasisi yanayohusu Muungano wanamliki ardhi Bara pamoja wafanya biashara.

Wanaojua Sheria watusaidie hapa naona Leo nitalala mabusu kwa haya sababu, na sanasana hiyo ya kiubaguzi,kwa kweli kauli ya kiubaguzi kinauma kuliko matusi.
ni kweli Mkuu.kumbe ukitaka ardhi zenji lazima uoe kule na kuishi miaka mitano huko huko mfululizo.au uwe na partneship na mzenji. ukijichangaja kuepuka masharti unaweza kupata ardhi ila pia ni rahisi kuipoteza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom