Kwanini Mtangayika haruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar wakati Mzanzibari anamiliki ardhi Tanganyika?

PAND PIERI

Senior Member
Jul 30, 2020
183
270
Wakuu waliotunga Sheria ya Mtanganyika kutoruhusiwa kumliki ardhi Zanzibar wakati wazanzibar wanarusiwa kumliki ardhi Bara waliwaza nini?

Kuna jamaa amekaa Zanzibar miaka miwili na kapata kiasi kadhaa akataka anunue eneo ajenge kibanda chake nje ya mji, amechoka maneno ya wenye nyumba. Cha ajabu kakosa kwa sababu za kijinga na ikanipelekea kujiuliza maswali mengi kwa kujua au kutojua swala yanayohusu Muungano.
  • Mtanganyika harusiwi kumiliki ardhi Zanzibar kisheria
  • Mtanganyika harusiwi kuwa na kitambulisho cha Mzanzibar mkazi
  • Pamoja na harufu ya kiubaguzi wa kidini ,inawekwa kwenye sababu ya kukosa ardhi (Jirani wa eneo alilotaka kununua jamaa katoa kauli ya kiubaguzi wa kidini nanukuu !! "huyu kafiri atajenganje karibu na sie").
Nimejiuliza kwanini Bara wazanzibari wanamliki ardhi bila vikwazo ?,nini maana ya Muungano,na hii kwa asilimia kubwa wazanzibari wanaofanyia kazi kwenye taasisi yanayohusu Muungano wanamliki ardhi Bara pamoja wafanya biashara.

Wanaojua Sheria watusaidie hapa naona Leo nitalala mabusu kwa haya sababu, na sanasana hiyo ya kiubaguzi,kwa kweli kauli ya kiubaguzi kinauma kuliko matusi.
 
Huu muungano unawafaidisha sana wa zanzibar kuliko wa bara... yaani hata uwe tajiri kama mzee mengi zanzibar haruhusiwi kununua ardhi ajenge nyumba yake ya kuishi hata chumba kimoja
Mambo Kama haya yanakera Sana, imagine wanzanzibari wanaruhusiwa kumlika ardhi Bara lkn Wabara hawarusiwi, Mambo yote yanayohusu Muungano serekali ya Bara ndio inagharamia kuanzia mshara, uendeshaji na kila kitu.

Hapa nikianza kuangalia Waziri wa Katiba wa Sasa, nikiangalia clips zake za nyuma kabla hajawa Waziri"kutolewa kwenye dampo ya takataka kwa mjibu wa kauli yake mwenyewe na baada ya kuteuliwa na Magufuli . Watanganyika lazima wafanye kitu ili kuweka swala la Muungano sawa.
 
Kwasababu wana utindio kutokana na kubanwa kichwa wakizaliwa ili wasiwe na visogo
 
Kuna pahala niliona ufafanuzi kuwa ardhi ya Znz ni ndogo, so Wadanganyika kwa kuwa ni wengi, wakiruhusiwa kumiliki huko wataimaliza yote fasta
Sababu hiyo haina mashiko hata kidogo, kwani Watanganyika hawazaliani ili badae wajaze eneo lao wanaokaliwa na wazanzibari?, kwa hiyo hao wazanzibari hawazaliani kuja kujaza eneo lao bila wanao hofia Watanganyika watayamaliza ?
 
Kwasababu Zanzibar ina katiba yake, pili ardhi kwao siyo jambo la muungano, tatu eneo la zanz ni dogo hivyo si vyema wasiyo wazanzibar kumiliki maana anaweza tokea bwege mmoja akainunua yote! Wapemba akawatimua wakaishi kwenye mitumbwi
Kama hizo ndio sababu , ni lazima marekebisho yafanyike, inaonekana waliohusika ku suggest maoni /kuandaa Sheria na kupitisha walikosea kwa kiasi kikubwa. Kama ni hivyo kwa sababu hayohayo ni bora wazanzibari wasinunue ardhi Bara.
 
Kama hizo ndio sababu , ni lazima marekebisho yafanyike, inaonekana waliohusika ku suggest maoni /kuandaa Sheria na kupitisha walikosea kwa kiasi kikubwa. Kama ni hivyo kwa sababu hayohayo ni bora wazanzibari wasinunue ardhi Bara.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom