Kwanini Mtanganyika hawezi kugombea urais Zanzibar?

Wakuu habari

Nipo hapa natafakari huu muungano wetu ambao binafsi nauona umekosa usawa kabisa

Kuna hili suala la urais na umiliki wa mali katika muungano huu.

N rahis kwa mzanzibar kumiliki ardhi TANGANYIKA kuliko MTANGANYIKA kumiliki ardhi Zanzibar

Kama muungano huu n wa usawa mbona unaubaguzi ndani yake nayasema haya nikiwa Zanzibar hapa kiutafutaji toka wiki iliyopita nikajaribu kufuatilia taratibu za umiliki wa ardhi kiukwel n ngumu mno kupata ardhi yaaan watoto wa mjin wanasema kwa mbinde Sana

SUALA LA URAIS. nalo naona n kizungumkuti Sana kwann watu wabara au Watanganyika hawatakiwi KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR lakn mzanzibar anaruhusiwa kugombea urais TANGANYIKA

RAIS SAMIA amewatoa mashekhe wanuamsho mahabusu lakn ameshindwa kuwatoa mashekhe mbalimbali ambao wapo magereza au mahabusu maeneo mablimbli Tanzania je Rais huyu yupo kwa maslah ya wazanzibar pekee Kama haki angetenda kwa wote

Tumeona pesa za covid zilizokopwa zimepelekwa had Zanzibar kujenga shule hospitali je mikopo wanayo kopa wenzetu wa Zanzibar lini ililetwa huku bara na sisi tukajenga shule na zahanati?

Huu muungano n wakuangaliwa kwa jicho la pili umekuwa wa kuwadekeza wazanzibar huku TANGANYIKA ikinyonywa
Yooote hayo siyo tatizo

Tatizo ni kwamba pia hatuwezi kuuvunja hata tukitaka🤣🤣🤣
 
1. Aboud Jumbe Mwinyi kutoka Mji Mwema.
2. Ali Hassan Mwinyi (Nzasa) kutoka Mkuranga
3. Hussen Ali Mwinyi nusu Mzanzibari na Nusu Mtanganyika.
4. Abeid Amani Karume - Malawi
5. Amani Abeid Karume nusu Mzanzibari
Hii inaonyesha mtanganyika yeyote anaweza kuwa rais Zanzibar.
 
Huu muungano kwa taarifa yako we wa kunyumba tunaulazimisha sisi wa bara.
Sisi kuwalalamikia wa Zanzibar ni kuwaonea tu. Tukilalamika Sana watatuambia tuuvunje.

We wakunyumba umeongea point kabisa wakunyumba.
 
Zanzibar ni nchi kamili kwa 100%, lakini ipo kwenye 'shirikisho' linaloitwa Tanzania.

Tanganyika ni shamba la bibi ambalo kila mgeni anaweza kuingia na kuvuna chochote. Sisi wazanzibar, wengine warundi, warwanda, wakongo, wakenya, waganda, waarabu, wahindi, wachina, wazungu nk. kila siku tunavuna kwenye hilo shamba la bibi.

Watanganyika msitegemee kuna mtu kutoka nje atakuja kuwapigania, unganeni pamoja muipiganie Tanganyika yenu. Mjiandae kulipa gharama. Woga wenu ndio unawagharimu sasa.
Hakuna watu wabaguzi kama hawa wazanzibar. Huyu bibi akimaliza muda wake atoke tu.
 
Zanzibar ikiwa chini ya waarabu itaendelea kwa kac sana,,,ili ipae kiuchumi na watu wake wawe na maendeleo solution ni kuvunja muungano. Muungano hauna faida kwa wazanzibari
Kumbe mnawaza kutawaliwa na mwarabu sio kujitawala ?
 
Hakuna watu wabaguzi kama hawa wazanzibar. Huyu bibi akimaliza muda wake atoke tu.
Hata katiba inasema hivyo
Akimalia miaka kumi haruhusiwi kugombea tena
Labda kama aliyetangulia angefanikiwa kuchange katiba na akakaa unlimited
Sidhani kama kuna mtu angetia nano humu
 
Pole ya nini?? Mnaumia mno mukickia neno "waarabu" hivi kuna jamii yoyote duniani watu wake wakarimu kama waarabu? Tusemeni ukweli bila kutia chuki mzehe. Wewe kama wanakukera kaa kimya mzehe
Kuna msaada wowote wa maana dunia hii umewahi toka nchi hizo ?
Kati ya wazungu na waarabu ni jamii ipi inayoongoza kutoa misaada hata kuwekeza Africa?
Wazungu wanamapungufu yao lakini wanamambo mazuri mengi
 
Kuna msaada wowote wa maana dunia hii unawahi toka nchi hizo ?
Kati ya wazungu na waarabu ni jamii ipi inayoongoza kutoa misaada hata kuwekeza Africa?

Unataka wajitangaze dunia nzima wajuwe kama wametoa msaada kama ilivyo kwa ndugu zako wacokuthamini a.k.a mabeberu?
 
Unataka wajitangaze dunia nzima wajuwe kama wametoa msaada kama ilivyo kwa ndugu zako wacokuthamini a.k.a mabeberu?
Mabeberu ni smart aiseee.
Huoni mataifa yao yalivyo na maandeleo ,usalama,uhuru (quality of life in general).
Usifananishe mabeberu na nchi za ajabu ajabu tafadhali
 
Wazanzibar asili yao Tanganyika, na Oman. Lengo la muungano lilikuwa kuilinda Unguja isichukuliwe na wageni. Kwa hiyo ni suala la majadiliano na kuondoa kero za huu muungano. Nakumbuka huko nyuma bila pasipoti huendi Unguja. Mambo hatua kwa hatua, pole pole ndiyo mwendo.
 
Mabeberu ni smart aiseee.
Huoni mataifa yao yalivyo na maandeleo ,usalama,uhuru (quality of life in general).
Usifananishe mabeberu na nchi za ajabu ajabu tafadhali
Smart kwako wewe wanaekutambuwa "SOKWE"
Kwani nchi za kiarabu hazina maendeleo? Kuna mataifa mengi ya ulaya yamepigwa gep kubwa mno na nchi za kiarabu kiuchumi/kimaendeleo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom