Kwanini Mtaa wa Congo umekuwa maarufu sana toka mwaka 1920?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Mtaa wa Congo upo Kariakoo Jijini Dar es Salaam Mtaa huu umekuwa Maarufu sana kwa Wingi wa Watu toka Mwaka 1920 mpaka leo.

Je, UMAARUFU wa Mtaa huo ni NINI?

Kwanini Muda wote una Watu Wengi Tofauti na Mitaa Mingine?

Je, kuna Biashara gani kwenye Mtaa huo inayokusanya Watu wengi kiasi hicho?

20210908_100222.jpg
 
Duh!, palikuwa na minazi back then na nyumba za udongo, mtu alieishi mwaka huo leo umfufue ukamuoneshe mtaa wake ataumwa kichwa kwa yale magorofa atakayoyaona, yamekuwa mengi kama idadi ya hiyo minazi nayoiona kwenye picha, itakuwa ni mambo ya kibiashara tu.
 
Wakati mi nipo mdogo, huo mtaa ulikuwa hauna umaarufu wowote

Msimbazi na Uhuru labda

Hapo palikuwa na wauza nyanya tu

1980s
 
Lord
Soma makala hiyo hapo chini:

MASAHIHISHO PICHA TAWI LA TANU: DUA NYUMBANI KWA ALI MSHAM SAFARI YA UNO 1955

Hapo chini ni picha ya Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa nyumbani kwa Ali Msham ambako alifungua tawi la TANU mwaka wa 1955.

Huo si Mtaa wa Congo mwaka wa 1920.

Siku hii ni February 1955 Nyerere alikuwa anakwenda UNO kwa mara ya kwanza na huo umma uliofurika hapo ni kuwa hapo nyumbani kwa Ali Msham lilipo tawi la TANU palifanyika dua ya kumuombea Nyerere salama katika safari ile.

Ukiangalia vizuri hii picha mkono wa kulia nyumba ya kwanza kuna watu wamevaa kanzu na koti wamekaa barazani wanafanya kisomo.

Wanae Ali Msham wamenieleza historia ya baba yao na uhusiano wake na Mwalimu Nyerere na Mama Maria walipohamia Magomeni uhusiano uliodumu hadi Tanganyika ilipopata uhuru wake mwaka wa 1961.

Naishukuru familia hii kwa kunipa picha nyingi za baba yao wakati anapigania uhuru wa Tanganyika na kuniruhusu nizitumie nipendavyo.

Screenshot_20210908-205114_Facebook.jpg


Screenshot_20210908-205330_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom