Kwanini Msemaji wa Serikali anadanganya Umma juu ya Mikataba ya Madini?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Na Thabit Jacob

Nimeangalia mahojiano kati ya @TZMsemajiMkuu na Salym wa @bbcswahili Jioni hii. Msemaji Amesema serikali ya awamu ya tano imeboresa sana uwazi kwenye sekta ya madini na mikataba. Huu ni upotoshaji na naomba niweke ufafanuzi na ukweli halisi. Thread

Kwanza kabisa, wananchi wengi hawafahamu mkataba wa Barrick na Serikali una nini ndani yake hasa. Mkataba wa Mwaka 2019, unajumuisha jumla ya Mikakata Tisa kusuhu vitu mbalimbali. @TZMsemajiMkuu amesema mikataba iko kwenye mjadala, sio sawa, Mikataba imeshasaniwa tayari.

Kwa faida ya wananchi wote, hii dio mikataba 9 ambayo serikali imesaini na Barrick.

1. Framework agreement
2. Management and administrative services
3. Twiga shareholders agreement
4. North Mara shareholders agreement
5. Buly shareholders agreement.

6. Buzwagi shareholders agreement

7. North Mara development agreement

8. Buly development agreement

9. Pangea development agreement

Mikataba hiyo yote ilisainiwa Ikulu, wabunge hawakupata nafasi yotote kuipitia, imebaki kuwa siri na wananchi hawajui chochote. Serikali inayo sema inajali uwazi kumbe inapenda usiri. Kama ni mikataba mizuri unaficha nini hasa! Kwa faida ya nani!

Lakini hili swala la usiri nilianza kabla hata ya Mkataba ma mwaka 2019. Mwaka 2018, Kamapuni ya Tanzanite one ilifikia makubalino ya kulipa serikali kiasi cha pesa kwa madai ya madini ya Tanzanite. Serikali ilikataa kabisa kuweka wazi kiasi cha fedha. Angalia hapa https://t.co/sDTRkNz3C5
Kuhusu hiyo ya Tanzanite One unaweza kusoma zaidi hapa (lugha ya mabeberu lakini) Prof Kabudi says Tanzanite One paid compensation following

Mwaka Jana, Waziri wa Madini akishiriki mkutano wa @EITIorg aliahidi Tanzania itaweka mikataba yote ya madini na gesi wazi. Lakini ahadi imekuwa Porojo. https://t.co/SDrR09wt5x

More than half of EITI countries have disclosed oil, gas and mining contracts! That is actually a big deal. Doto Biteko, Minister of Minerals from #Tanzania 🇹🇿 , and Minister Trotman of #Guyana 🇬🇾 announce that their governments will follow suit! at #EITI2019 @IsabelMunilla 👏 https://t.co/TvOhSL2YPh

Unaweza kusoma zaidi kusuhu ahadi hiyo ya kuweka mikataba wazi hapa. Ni muda sasa kwa wananchi kuuliza mikataba itawekwa wazi Lini?
Tanzania now set to disclose mining contracts

Kwenye mradi wa Bomba la Mafuta la Uganda-Tanzania, serikali imetoa misamaa mbalimbali kwa Uganda katika maeneo ya kodi, fidia na kazalika. Kuna mengine mengi lakini mkataba ni siri. Uganda walifurahi

https://t.co/gZo4Vz2uLA

I thank Tanzania for giving us concessions to use the Tanga route for the pipepline. In some areas, they allowed the pipeline to pass through road reserves thus cutting costs of compensation. https://t.co/WaOX1lwADf

Kipindi kile nilisema hilo ni tatizo la Kusaini mikataba nyuma ya pazia, bila bunge ambalo bahati mbaya limetekwa Prof Assad alivyosema. Waingereza wanasema Backroom Concessions.
https://t.co/e8ZmL7Pxmg

Transit fee, VAT and now compensation. Day by day details are emerging about backroom concessions. #EACOP https://t.co/aThhqeSRKX
 
Huyo anayesema kweli ni nani?

Yaani unajadili mikataba ya madini bila kuongelea sheria mpya ya bunge inayotamka Rasilimali zetu kuwa ni za Serikali!! hapo ndipo propaganda zenu zinapofeli.

Kwenye Madini: Mapato na kodi zitokanazo vimeongezeka.
Thamani imeanza kuongezwa humu humu nchini.

Tatizo wakati Bunge linajadili madini Chadema mlikimbia Bungeni.
 
Huyo anayesema kweli ni nani?...
Serikali ni kikundi cha watu sio nchi na serikali sio tanzania. Nchi ni ya wananchi na nchi ni wananchi. Serikali ni chama ni kakikundi ka watu.

Haki kakikundi sio kwamba ndio kenye haki wenye haki ni wananchi wanaotakiwa kujua mali zao zinaliwaje na wanapata nini. Huo ni wizi na ufisadi unaofishwa kwa niaba ya ccm na mabeberu mnao walinda na ccm inakuwa kibalaka wa mabeberu
 
Toka lini serikali ya ccm ikawajali watanzania?

Miaka 60 ya ufukara, ujinga, maradhi, miundombinu mibovu, ukosefu wa maji na kadhalika.

Nothing good is going come from ccm government, nothing.

Kuna mtu ana akili timamu anategemea ccm itatuletea maendeleo Tanzania?
 
Kwani wewe ndo unatuambia ukweli au unatulisha matango pori. Wananchi wengi kutokujua kilichomo kwenye mikataba si kigezo cha kuharamisha mikataba hiyo, kwanza ni wananchi gani unaowaongelea wanaopaswa kujua kilichomo ndani ya mikataba?

Mwananchi yeye anachohitaji ni kujua matunda yatokanayo na mikataba hiyo basi na ukimuuliza leo Mtanzania mwenye akili timamu atakueleza kwamba kwa sasa madini yamekuwa yakiinufaisha Tanzania tofauti na miaka ya nyuma.

Leo akina Laizer wanapata Tanzanite zenye kilo nyingi ni kwa nini? Kwani huko nyuma hizo Tanzanite zenye ukubwa huo au zaidi zilikuwa hazipatikani?

Zilipatikana sana tu lakini kwa sababu ya udhaifu wa udhibiti uliokuwepo ilionekana nchi inayoongoza kwa uuzaji wa Tanzanite ni South africa ikifuatiwa na Kenya na Tanzania ilikuwa ya tatu lakini leo hii Tanzania ni ya kwanza kwa uuzaji wa Tanzanite na hatuhitaji kuitwa wa kwanza bali tuitwe TANZANIA NDO NCHI PEKEE DUNIANI INAYOUZA TANZANITE
 
Kwani wewe ndo unatuambia ukweli au unatulisha matango pori. Wananchi wengi kutokujua kilichomo kwenye mikataba si kigezo cha kuharamisha mikataba hiyo, kwanza ni wananchi gani unaowaongelea wanaopaswa kujua kilichomo ndani ya mikataba?

Mwananchi yeye anachohitaji ni kujua matunda yatokanayo na mikataba hiyo basi na ukimuuliza leo Mtanzania mwenye akili timamu atakueleza kwamba kwa sasa madini yamekuwa yakiinufaisha Tanzania tofauti na miaka ya nyuma.

Leo akina Laizer wanapata Tanzanite zenye kilo nyingi ni kwa nini? Kwani huko nyuma hizo Tanzanite zenye ukubwa huo au zaidi zilikuwa hazipatikani? Zilipatikana sana tu lakini kwa sababu ya udhaifu wa udhibiti uliokuwepo ilionekana nchi inayoongoza kwa uuzaji wa Tanzanite ni South Africa ikifuatiwa na Kenya na Tanzania ilikuwa ya tatu lakini leo hii Tanzania ni ya kwanza kwa uuzaji wa Tanzanite na hatuhitaji kuitwa wa kwanza bali tuitwe TANZANIA NDO NCHI PEKEE DUNIANI INAYOUZA TANZANITE
Umeiona hiyo mikataba? Imepita katika bunge lipi? Au ni siri? Inakuwa siri kwa maslai ya nani?
 
Huyo anayesema kweli ni nani?

Yaani unajadili mikataba ya madini bila kuongelea sheria mpya ya bunge inayotamka Rasilimali zetu kuwa ni za Serikali!!....hapo ndipo propaganda zenu zinapofeli.

Kwenye Madini:Mapato na kodi zitokanazo vimeongezeka.

Thamani imeanza kuongezwa humu humu nchini.

Tatizo wakati Bunge linajadili madini Chadema mlikimbia Bungeni.
Naona umepaniki badala ya kujibu hoja
 
Sasa hizi wamebadili gia angani eti 50/50 win iko kwenye muktadha Mara wa kodi, ajira sijui kwenye corporate social responsibility yaani chenga nyingi. Seems barrick walitoa chochote huko private room ili kuyamaliza. Hawa ndio wazalendo wa awamu ya 5
 
Huyo anayesema kweli ni nani?

Yaani unajadili mikataba ya madini bila kuongelea sheria mpya ya bunge inayotamka Rasilimali zetu kuwa ni za Serikali!!....hapo ndipo propaganda zenu zinapofeli.

Kwenye Madini:Mapato na kodi zitokanazo vimeongezeka.

Thamani imeanza kuongezwa humu humu nchini.

Tatizo wakati Bunge linajadili madini Chadema mlikimbia Bungeni.
Umeelewa lakini ndugu Mataga?
 
Acheni Uongo Watanzania wana Akili labda mkawadanganye Wanyonge weny wanaokunywa Maji ya Matope
 
I thank Tanzania for giving us concessions to use the Tanga route for the pipepline. In some areas, they allowed the pipeline to pass through road reserves thus cutting costs of compensation
 
Back
Top Bottom