Rais Magufuli ataja sababu kusitisha ujenzi bandari ya Bagamoyo kwa Mkopo wa Dola Bilioni 10

Na katika gesi alichelewa, akakuta maji yameishamwagika.

Halafu unakuta kuna mpumbavu anajisikia vibaya kisa magufuli haongei kiingereza fasaha, hapa ndio utajua kila binaadam ana kipaumbele chake.
Sasa hiyo Mikataba ameijuaje athari zake wakati lugha ya mabeberu haipandi??
 
Waliomshabikia Kikwete na mama Makinda siku Ile usiku, mswaada ulipo lazimishwa kupitishwa usiku wa manane ni pamoja na huyu anayelalamika leo. !!!

Ccm wote wanafki. Leo ndiyo wanajifanya wazalendo wa kuionea nchi huruma ?!.

Tatizo la Tz ni katiba. Imewafanya ma Rais mamiungu watu . Na ndiyo chanzo cha kuiuza nchi yetu kwa wanaitwa wawekezaji.
Hawa ni ukoo wa panya banaaa
 
Mtoe magu ktka mambo ya kipuuzi kama hayo, labda kama umemjua baada ya kuwa rais 2015.

Huyu mtu mna chuki naye, lakini isiwe sababu ya kumpaka ubaya kwa gharama,
Unataka kusema wakati haya yanapitishwa yeye alikua kijijini kwao Chato??
 
MK254, Tatizo la Tanganyika ni katiba inayowafanya ma Rais kuwa mamiunguwatu !!. Hawahojiwi na yeyote juu ya actions zao wawapo mamlakani au hata wakishatoka madarakani. Na hao hao ndiyo uendelea kutupangia nani wa kutuongoza na si wa kutuongoza !!. Ma Rais wa Tz ni mamiunguwatu

Kama si hivyo muswaada wa Gas na mafuta isingelazimishwa kupitishwa ilimradi anayetoka atoke ameshasaini na kuwa Sheria . Wapinzani walijitahidi hata kutumia nguvu bungeni , lakini waliishia kuitiwa police kuwaondoa ili muswaada upite. Na ile ilikuwa ni amri toka juu. Natamani tuwe na katiba kama ya S Korea , Brazil , France n.k. ili hawa watu wakitoka madarakani wawajibike kwa matendo yao ya aibu. Lakini hii tuliyonayo inalinda viongozi dhidi ya wananchi
Kenya na katiba nzuri kina Ruto na wachina wanazidi kupiga pesa kila uchao,,
Trust me, katiba pekee sio suluhu.
 
Kenya na katiba nzuri kina Ruto na wachina wanazidi kupiga pesa kila uchao,,
Trust me, katiba pekee sio suluhu.
Basi siyo nzuri !!. Katiba nzuri ni ile inayowawajibisha viongozi wabadhirifu . Angalia Brazil , France, S Korea , S Africa nk. nk. Si hizi zilizowageuza viongozi mamiunguwatu.
 
Basi siyo nzuri !!. Katiba nzuri ni ile inayowawajibisha viongozi wabadhirifu . Angalia Brazil , France, S Korea , S Africa nk. nk. Si hizi zilizowageuza viongozi mamiunguwatu.

Na inaweza ikawa nzuri wa kuisimamia asiwepo,kama haifuatwi kwa mambo madogo haiwezi fuatwa kwa mambo makubwa.
 
kwanini unataka kujilinganisha na nchi ambazo zimekuwa nchi kwa miaka 1000's Hizo nchi hapo mwanzo mwanzo huko enzi za kale zilikuwa Kingdoms/ Hakuna democrasia...Sasa nchi za afrika ziki ruka stages fulani hadi kuwa democracy hapo ndipo shida inatokezea. Sababu mwafrika bado hajui democrasy ni nini..Anafikiria democracy aidha ni uhuru wa makabila kujitawala ama ni uhuru wa kudhalilisha nchi yako, kutukana na kukosea heshima..
uendelevu wa kuelewa democrasy ni kitu gani bado upo chini sana, yaani tunaelewa democracy kama vile wazungu waliewa miaka ya 1500's
Nilikuwa off lakini naomba nikujibu hivi. Maisha ni haya tunayoishi leo. Huwezi kuniambia nisubiri miaka 1000 kupata haki na maisha mazuri ninayotaka leo. Africa haiwezi kuendelea kujificha kwenye kichaka cha uchanga kuhalalisha maovu ya viongozi wao kama haya yaliotokea Tz (Bagamoyo & Gas na mafuta) .

Tumeamua kuiga ustaarabu wa maisha ya watu wa dunia ya 1 (western). Basi na tuige jumla siyo nusu nusu . Hatuuwezi kuendelea kuishi kijima ati tu mataifa yetu bado ni machanga !!!.

Kinachowasumbua viongozi wa ki Africa ni ubinafsi, utemi wa kujiona watawala badala ya viongozi. Kiongozi mzuri hufuata wananchi wanataka je. Lakini mtawala hufuata nafsi yake inatakaje.

Usiku mwema
 
Hata hizo nchi unazoamini unaziiga,zimetokea kwenye msoto.
 
Rais Akisema hatuhitaji kusikia upande wa pili,
Besides, Kikwete was not Different from Uhuru Kenyatta and William Ruto.

Hii imekumbusha ya zamani yaani ya wakati wa awamu ya tatu na nne Mawaziri walikuwa wanakimbilia kuwaomba Wa Africa Kusini(Makaburi) na Uarabuni kuwaomba wachukue makampuni na mashirika aliyotuachia Mwl Nyerere kwa bei ya kutupa. Wala siyo kwa bei ya kutupa bali buuuure kabisa Mawaziri wa Mawasiliano wakati huo walihusika saaaana kuuza nchi! Asante Rais Dr Magafuli kwa kuyaoana hayo yote! Bado una mengi ya kufanya kwani nina imani kuwa 2021 utarudisha nyumba na plot zote za serikali na mashirika ya umma walizozichukia au kuuza bila huruma! Zote zitudishwe serikalini! Za Bandari zirudishwe, za Reli, Benki, Posta na Mawasiliano, TAZARA, EAC Arusha, Research Institutes, za Wizara, Mahakama na kadhalika!!
 
Pascal Mayalla umesoma habari hii
Mkuu Njinjo, no nilikuwa sijasoma makala hii, asante kuni tag, ngoja nisome.
Thanks
P
Update, nimeisoma na nimeguswa, kwa ruhusa yako naomba kuitumia makala hii kama mbegu ya kupandia kwa kupandisha bandiko langu fulani kuhusu SGR.
P
 
Nilikuwa off lakini naomba nikujibu hivi. Maisha ni haya tunayoishi leo. Huwezi kuniambia nisubiri miaka 1000 kupata haki na maisha mazuri ninayotaka leo. Africa haiwezi kuendelea kujificha kwenye kichaka cha uchanga kuhalalisha maovu ya viongozi wao kama haya yaliotokea Tz (Bagamoyo & Gas na mafuta) .

Tumeamua kuiga ustaarabu wa maisha ya watu wa dunia ya 1 (western). Basi na tuige jumla siyo nusu nusu . Hatuuwezi kuendelea kuishi kijima ati tu mataifa yetu bado ni machanga !!!.

Kinachowasumbua viongozi wa ki Africa ni ubinafsi, utemi wa kujiona watawala badala ya viongozi. Kiongozi mzuri hufuata wananchi wanataka je. Lakini mtawala hufuata nafsi yake inatakaje.

Usiku mwema
Mw Nyerere aliwaambia kwamba kuna democrasia bila vyama vingi, democrasia na kingozi wa kudumu...mkabisha hoja zake, yeye uelewa wake wa democrasia ulikuwa miaka 2000 mbele..Leo enda germany, angela merkel amekuwa kiongozi miaka 20 bila mpinzani, China inaenda na speed ya ndege huku ikuwa na chama kimoja..Uingereza na Japan bado wana wafalme wa kudumu...Canada mfalme wao ni Queen of england..
 
Mkuu Njinjo, no nilikuwa sijasoma makala hii, asante kuni tag, ngoja nisome.
Thanks
P
Update, nimeisoma na nimeguswa, kwa ruhusa yako naomba kuitumia makala hii kama mbegu ya kupandia kwa kupandisha bandiko langu fulani kuhusu SGR.
P
Mkuu, mimi siyo mwandishi zuri kama wewe endelea tu. Nilikutag ili ujaribu kusaidia wengine kwa kuweka bandiko kuonesha kuwa pamoja na mapungufu yake, Dunia nzima inaona jinsi anavyopigania nchi si tumbo lake. Nitakuletea na nyingine leo
 
Basi siyo nzuri !!. Katiba nzuri ni ile inayowawajibisha viongozi wabadhirifu . Angalia Brazil , France, S Korea , S Africa nk. nk. Si hizi zilizowageuza viongozi mamiunguwatu.
A reason I told you Katiba pekee sio Suluhu, It should begin with Leadership, kusimama kwenye haki sio lele mama kama unavyodhani. katiba are just pages my friend.
 
Rais wa Tanzania John Magufuli ameghairi mkopo wa China wenye thamani ya dola bilioni 10 akisema kwamba masharti ya makubaliano ya mkopo wa China yanaweza kukubaliwa tu na mtu mlevi.

Mkopo uliotajwa ulikuwa umesainiwa na mtangulizi wake Jakaya Kikwete kujenga bandari kwenye kijito cha Mbegani huko Bagamoyo.

Mtangulizi wake, Jakaya Kikwete alikuwa amesaini mkataba huo na wawekezaji wa China ili kujenga bandari hiyo kwa sababu watapata miaka 30 ya garantii juu ya mkopo huo na miaka 99 ya kukodisha bila kuingiliwa, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya ndani.

Iliyoitwa "mkopo wa kifo wa Wachina", mashirika kadhaa na raia wa Afrika walimtaka Rais wa wakati huo kufuta makubaliano.

Walikuwa wameonya kwamba hatua hiyo itakuwa na athari mbaya lakini wasiwasi wao ulipuuzwa na mpango huo ulisainiwa.

Lakini, baada ya kuingia madarakani, Rais Magufuli alianzisha mchakato wa kupitia upya mkataba na kushinikiza wawekezaji hao watoe kipindi cha kukodisha hadi miaka 33 badala ya miaka 99 iliyosainiwa na serikali iliyopita

Wawekezaji hao walishindwa kutimiza masharti yaliyowekwa mpaka tarehe ya mwisho iliyotolewa na serikali ya Magufuli na kwa sababu makubaliano yalifutwa.

Uchina mara nyingi imekuwa ikishutumiwa kwa kuziwekea nchi maskini za Afrika katika mtego wake wa deni kwa kuwapatia mikopo ya miradi ya miundombinu inayohitajika sana na kisha kuwadhibiti wanaposhindwa kulipa madeni.

======================================

Tanzania President John Magufuli has cancelled a Chinese loan worth $10 billion saying that the terms of the Chinese loan agreement could only be accepted by a drunken man.

The aforesaid loan had been signed by his predecessor Jakaya Kikwete to construct a port at Mbegani creek in Bagamoyo.

His predecessor, Jakaya Kikwete had signed the deal with Chinese investors to build the port on condition that they would get 30 years to guarantee on the loan and 99 years uninterrupted lease, according to local media reports.

Labeled as the “killer Chinese loan”, several organizations and African citizens had demanded the then President to cancel the agreement.

They had warned that the move would have dire consequences but their concerns were overlooked and the deal was signed.

However, after coming to power, President Magufuli initiated the renegotiation process and pressed the investors to bring down the lease period to 33 years instead of 99 years signed by the previous government

The investors didn’t meet the deadline issued by the Magufuli government as a result of which the agreement was canceled.

China has often been accused of luring the poor African countries in its debt-trap by providing them loans for much-needed infrastructure projects and then control them when they fail to pay off their debts.

Screenshot_20200424-225341.jpg

Source: Khabarhub
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom