Kwanini Serikali ilituficha kuugua kwa Dkt. Magufuli?

Definition ya Serikali ni group la watu waliochaguliwa na watu kwa ajili ya kutetea maslahi ya watu hao.(Government of the people, by the people, for the people)

Sasa hiki kikundi cha majambazi kinachoongoza watu hapa Tanzania kimekosa sifa zote kuu mbili:

1.Hiki kikundi cha ugaidi hakijatokana na watu.Hakina kibali cha wananchi.

2.Hakitetei maslahi ya wananchi.

Kwa sababu kikundi hiki cha ugaidi kimekosa sifa kuu mbili za kuitwa Serikali hakiwezi kuitwa ni Serikali.
Ndo maana nimekuambia as long as huna tatizo kwenye kuzitii sheria bila shuruti za hao majambazi hakuna tatizo. Endelea kuwa mwaminifu katika hilo.
 
Ndo maana nimekuambia as long as huna tatizo kwenye kuzitii sheria bila shuruti za hao majambazi hakuna tatizo. Endelea kuwa mwaminifu katika hilo.
Hakuna sheria yoyote ninayotii ya magaidi bali nafanya mambo yangu kwa utashi wangu.Dhamira ikiniambia kuwa hili ni baya sifanyi ni ikiniambia kuwa hili ni zuri nafanya.Mfano tozo silipi hata moja kwa sababu ni jambo baya.
 
Kama sikosei, mpaka sasa Rais Samia keshaongea na waandishi wa habari kama mara mbili hivi.

Ni zaidi ya mwezi sasa tokea alipoongea na wahariri wa vyombo vya habari/ waandishi wa habari toka ikulu ya Dar es Salaam.

Wiki moja au mbili zilizopita, akafanya mahojiano na Salim Kikeke wa BBC.

Katika nyakati zote hizo mbili, sikusikia kabisa akiulizwa ni kwa nini serikali yake ilituficha kuhusu kuugua kwa Rais Magufuli.

Wananchi hatukupata taarifa zozote zile zilizo rasmi hadi tukaishia kutegemea habari umbea na zisizo rasmi kupitia mitandao ya kijamii.

Kimya kilipozidi kutanda, tukaanza kudokezwa dokezwa kuwa hali si nzuri, mara sijui yupo anachapa kazi, mara sijui anafanywa nini…

Haikupendeza hata kidogo. Na hata vyombo vya habari vya kimataifa viliripoti kuhusu tetesi za kutoonekana kwa Magufuli.

Kwangu hili halikubaliki kabisa!

Wananchi kama waajiri wa hawa viongozi wetu, tuna haki ya kujua kuhusu afya za viongozi wetu.

Hapa simaanishi kila kitu kuhusu afya. Namaanisha tu ile kwa ujumla wake.

Kama mtu anaumwa, kalazwa, tuna haki ya kujua.

Mambo ya kuficha/ kufichwa halafu mnakuja tu kuambiwa mtu kaaga dunia, hayafai.
Hivyo, ningependa sana kujua kwa nini wananchi hatukupewa taarifa.

Na itokeapo fursa ingine ya Rais Samia au hata waziri mkuu Majaliwa kuongea na waandishi wa habari, ningependa kuona na kusikia wakiulizwa ni kwa nini hawakutufahamisha kilichokuwa kinaendelea.

Pascal Mayalla take note and spread the word.
Hayo ni mambo ya mauaji yatakuja siku zijazo bado yanaiva
 
Hakuna sheria yoyote ninayotii ya magaidi bali nafanya mambo yangu kwa utashi wangu.Dhamira ikiniambia kuwa hili ni baya sifanyi ni ikiniambia kuwa hili ni zuri nafanya.Mfano tozo silipi hata moja kwa sababu ni jambo baya.
Hahaha. Sawa sawa behaviourist.
Tozo hulipi hata moja na pia unafanya mambo kwa utashi wako na imetokea tu kuwa mambo yote ya utashi wako uyafanyayo si kinyume cha sheria za unaowaita majambazi.
 
Kama sikosei, mpaka sasa Rais Samia keshaongea na waandishi wa habari kama mara mbili hivi. Katika nyakati zote hizo mbili, sikusikia kabisa akiulizwa ni kwa nini serikali yake ilituficha kuhusu kuugua kwa Rais Magufuli.
Samia na marais wote waliopita huwa wanapelekewa maswali kwanza, may be 1-2 weeks before ili yaandaliwe majibu. Maswali huwa yanakuwa "censored" na swali lolote tatanishi huwa linaondolewa na ole wako uje ulichomekee siku ya interview ikfika.

Who knows? labda walishawahi kuuliza ila swali likatupwa kwenye dust bin
 
Hahaha. Sawa sawa behaviourist.
Tozo hulipi hata moja na pia unafanya mambo kwa utashi wako na imetokea tu kuwa mambo yote ya utashi wako uyafanyayo si kinyume cha sheria za unaowaita majambazi.
Kutokulipa tozo siyo kinyume cha sheria?Yaani kutokulipa kodi za majengo siyo kinyume cha sheria?!
 
We jamaa ukikuwa Na mutual interests Na mzee baba umejaribu kujificha wee finally umeshindwa kabisa Na sasa unaonesha feeling zako wazi wazi, Muache SASHA yeye ndo dereva nao tu naelewa nyie wa ukanda ule mna Mfumo dume sana, Habari ndo iyo sasa samia ni Amiri Jeshi mkuu Na Rais
 
Vice President hakujua kama President anaumwa?! Mkuu are you serious and well informed?!
Nini Vice mtaalam hicho cheo ni ceremonial tu mzee hata CDF anaweza kumvimbia VP ukitaka kuona hicho cheo hakina impact yoyote kimfumo angalia Uturn Alizopiga Bi mkubwa baada ya kushika cheo cha Urais
 
Ni wiki kadhaaa sasa tangu makamu wa Raisi ndugu philipo haonekani hadharani. Kuna taari fazinadai yuko mahututi,

Kama hizi taarifa ni za kweli Naona tabia ya kuficha maradhi na vifo vya viongozi wetu inaendalea
Whereabouts zitaanza sasa ivi twitter hawa activists uchwara watamsahau Gaidi mbowe waanze hashtag za whereabouts
 
Hi dunia kweli ni mapito. Rais mstaafu B. M. Mkapa, Balozi Mahiga, Balozi kijazi, maalimu Seif, Rais Magufuri Kama ndoto hivi lkn hatupo nao tena. Hakika ni kwa zamu zamu ni heri tukimcha Mungu.
 
Kama sikosei, mpaka sasa Rais Samia keshaongea na waandishi wa habari kama mara mbili hivi.

Ni zaidi ya mwezi sasa tokea alipoongea na wahariri wa vyombo vya habari/ waandishi wa habari toka ikulu ya Dar es Salaam.

Wiki moja au mbili zilizopita, akafanya mahojiano na Salim Kikeke wa BBC.

Katika nyakati zote hizo mbili, sikusikia kabisa akiulizwa ni kwa nini serikali yake ilituficha kuhusu kuugua kwa Rais Magufuli.

Wananchi hatukupata taarifa zozote zile zilizo rasmi hadi tukaishia kutegemea habari umbea na zisizo rasmi kupitia mitandao ya kijamii.

Kimya kilipozidi kutanda, tukaanza kudokezwa dokezwa kuwa hali si nzuri, mara sijui yupo anachapa kazi, mara sijui anafanywa nini…

Haikupendeza hata kidogo. Na hata vyombo vya habari vya kimataifa viliripoti kuhusu tetesi za kutoonekana kwa Magufuli.

Kwangu hili halikubaliki kabisa!

Wananchi kama waajiri wa hawa viongozi wetu, tuna haki ya kujua kuhusu afya za viongozi wetu.

Hapa simaanishi kila kitu kuhusu afya. Namaanisha tu ile kwa ujumla wake.

Kama mtu anaumwa, kalazwa, tuna haki ya kujua.

Mambo ya kuficha/ kufichwa halafu mnakuja tu kuambiwa mtu kaaga dunia, hayafai.
Hivyo, ningependa sana kujua kwa nini wananchi hatukupewa taarifa.

Na itokeapo fursa ingine ya Rais Samia au hata waziri mkuu Majaliwa kuongea na waandishi wa habari, ningependa kuona na kusikia wakiulizwa ni kwa nini hawakutufahamisha kilichokuwa kinaendelea.

Pascal Mayalla take note and spread the word.
Noted. This is very valid question ila hata ningepata chance kumuuliza Rais Samia, nisinge uliza swali hili, ni open ended question, nitajibiwa "Acha maswali ya chokochoko, umwache JPM apumzike kwa amani"
Usingeuliza kwa sababu unaogopa au kwa sababu unasadiki unajua utachojibiwa?
Nisinge uliza kwasababu mimi tayari ni black listed baada lile swali kwa JPM pale Ikulu, na najua the consequences za kuwa black listed, I wouldn't wish to ask any hard or tough questions, jina langu likarudishwa na kwenye kitabu cha Samia.
Better be safe than sorry.
P
 
42 Reactions
Reply
Back
Top Bottom