Kwanini Moyo Wa Rais Uwe Mgumu Kama Wa Pharao?

Thanda

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,915
596
Hivi jamani Huyu rais wetu "is his common sense common kweli"? hata Biblia inasema "Enyi wagalatia ni nani aliyewaloga? ikifanyika sensa watanzania tutakuwa Mil 48 and above, sasa anatuongozaje, Haya ndiyo maisha bora kwa kila mtanzania?Unawalinda mafisadi badala ya kuwatoa? Jamani mimi ni mpiga, namba ya kadi yangu Ni *45428905* kituo cha, Sekei, Jimbo la Arumeru Magharibi.(Ni mpiga kura halali na nitakuja kuitumia haki yangu kikatiba-kupiga kura kuwachagua watu watatu (Diwani, Mbunge, na Rais, period!!)

Sasa anatufikishia ujumbe gani kuhusu "Msamaha wa Mawaziri wake fisadi" wasing'oke? Ina maana wabunge wetu wote tuliowachagua wana "Taahira ya Ubongo?, Zitto Kabwe ni kichaa, au Tundu Lissu? Jamani mtasema hao ni CHADEMA, vipi kuhusu Deo Filikunjombe? Vipi hawa wabunge wengine wa CCM? Kwani pale bungeni hakukuwa na mawaziri wengine ambao wanayaona hayo madudu.

Tafakari Komavu: Maandamano yaliyotokea Uingereza unjua yalipoanzia? Watu waliji-mobilise vipi kama si huku kwenye mitandao?Hakuna somo lolote kwa mafarao wengine ambao leo hatunao?...Just 8 people unatoa kauli "NI UPEPO TU UTAPITA?" Unamtakia mema PM wako (Msemaji wa Serikali Bungeni)au unataka afe kabla ya siku zake? Mbona ulimchagua na tukamuunga mkono, tukashirikiana naye hata kwa Maombi, sala na dua zetu zote.....Haya Leo kapigiwa kura ya kutokuwa na imani naye...Inamng'oa yeye kwa lipi?.........Mheshimiwa rais naomba majibu kwani mimi ni mtanzania nina haki ya kuuliza na kujibiwa, na hapa sipigwi kofi kama lile la mwaka 1985.(rejea thread yangu:Nitaishitaki CCM Mahakamani).

PM akitaka kutoa maamuzi magumu UNAMZUIA, matokeo yake anakuja na kauli kuwa "NITATOA MSIMAMO KESHO" kwani usipokuwepo hana haki ya kufanya hayo maamuzi magumu?

Au ni Wagalatia sura ya 6, mstari wa 5 "Kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe?"

Mtakatifu Rais
Mtukufu Rais
Mheshimiwa Rais
Mwenyekiti wa CCM...Stoooooooooooooooooooooooooooooop, huo nao ni ufisadi unaoufanya.Kwa kauli yako ni kwamba unayapinga maoni, mawazo na ukweli ambao watanzania tunaujua, na Serikali ya CCM unayoiongoza itafia mikononi mwako kama ilivyokuwa U.S.S.R iliyofia mikononi mwa Mikhail Gorbachev mwaka 1991..akakimbilia kwa Bro. Bush

Namalizia kwa kuuliza kwa mantiki hii "Is our President Moralising Politics or Politisizing Morals?"

Wabunge wenzangu wa JF, naomba kuwasilisha hoja.
 
Kwa sababu serikali yake ni ya wahuni kuanzia wakurugenzi wa wilaya aliwachagua yeye hadi mawaziri ni kwamba anashindwa aanzie wapi kujitakasa. Serikali ya kikwete ni chafu kuanzia chini kwa sababu wakurugenzi hakuwachagua kufuata qualification bali alibase zaidi kwenye uswaiba, wengine ni maswaiba wake wengine ni wa mkewe, mfano hai ni mkurugenzi wa newala hana qualification mwenye hoja abishe. Mbunge wake mkuchika hawezi kumkataa kwa sababu na yeye alizawadiwa uwaziri
 
Ndugu yangu Moderator where are you, my Prompted comments on my thread to evacuate Mr.President, can you please reinstate "Rais Kikwete Should Undergo "VOTE OF NO CONFIDENCE"

IRUDISHE JAPO KWA MUDA KIDOGO TUJADILI HAPA.
 
Kwangu mimi, "RAIS TULIYE NAYE NDIYE NI JANGA LA TAIFA"
 
Kwa wemye masikio na kusikia wasikie , serikali yetu imeoza na kikwete asipoangalia atakuwa Gorbachof wa tanzania siku sio nyingi
 
Hata moyo wa Farao ulikuwa mgumu hivi hivi, pindi wana wa Israel walipokuwa wakitoka Misri kuelekea Nchi ya ahadi!

Huyu wa kwetu naye atapata mapigo yake ya mwisho na yako njiani muda si mrefu yatafika..... 'upepo huu ukimpita' itamjia gharika!
 
Swali jingine Mheshimiwa Rais nijibu, kwani najua uno muda wa kutosha sana kusoma mambo yanayokuhusu mtandaoni, muda wa kutosha kabisa kuchunguza kuna lipi jipya katika jamii forum. Kama si wewe "AKINA FULANI" wanakuletea yote;

SWALI: Kwanini hutaki ushauri kutoka vyama vya upinzani kwamba kuwe na serikali ya majimbo? Kwanini usiteue mawaziri kutoka vyama vyote vya upinzani kama rafiki yako George Bush? Ina maana ukifanya hivyo utakuwa umevunja sheria? ok weka reference ya sheria itakayokuwa imevunjwa....Kwani hao upinzani si watanzania, tena wenye uwezo mkubwa tu kuliko hao akina mjomba, wifi, shangazi na wengineo?
 
Kwangu mimi, "RAIS TULIYE NAYE NDIYE NI JANGA LA TAIFA"

kwa upande, wangu, Rais wetu ndio tatizo kwani hayupo kwa maslahi ya taifa! Yy yupo kwa maslahi yake binafsi...Na inawezekana kuna mgao anaopata kutokana na wizi unaofanywa na hao mawaziri.... Inauma mpaka leo mshahara wangu hautoshi hata kwa wiki mbili sembuse mwezi m1
 
Huyu JK aendelee kuwa na moyo mgumu kama wa Pharao alafu tutamtandika mapigo kumi kwa mda mfupi sana na yeye mwenyewe atasadiki.
 
Huyu JK aendelee kuwa na moyo mgumu kama wa Pharao alafu tutamtandika mapigo kumi kwa mda mfupi sana na yeye mwenyewe atasadiki.


Ndoto za mchana, soma historia ya JK- Mwanajeshi wa ukweli.
Haburuzwi yule mkuu, kiongozi wa dola na amiri jeshi mkuu lazima awe na maamuzi magumu.
 
Dalili ya mapigo kumi yameshaanza na Zito kupata indosimenti ya wabunge 71, lakini moyo wake ungali ngangari hadi mapigo kumi yakishakamilika ndo ataamini. Anawaamini washauri wake kumbe wanamfika kilemba cha ukoka tu.
 
Back
Top Bottom