Kwanini mnashangaa mafenesi, mapapai na mbuzi kukutwa na COVID-19/Corona?

Blackman

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
752
250
Mnachokiandika sio kile alichokisema Magufuli.
Lakini yupo kwa silimia 100% maana akiliza watanzania zimekuwa polluted na politics za kipumbavu.
Kongore Magufuli dunia inahitaji vichwa kama nyie
HVI KIWANGO KIPI ULICHOTUMIA KUPIMA MPAKA UKAONA ETI DUNIA INAHITAJ MTU KAMA MAGU
 

secret file

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
2,178
2,000
Interest, Unajua ulichooongea Lakini? Yaani watu wanatetea Lakini hawajui wanatetea nini masikini Kama huyu hajui lolote anataka tu kulazimisha kutetea, sasa Kama kirusi kinapatikana hadi kwenye mbao unasemaje kuwa Rais anashangaa kuonekana kwenye papai?

Au unatushangaaa vipi sisi Wakati kumbe kinaweza kupatikana hadi kwenye mti? Pole Sana Kwa kutojua unachoongelea na kutetea huyo rais ameleta maskitikito sana kwa kutowaaamini watumishi wake hadi anawapelekea mapapai na mafenesi, yeye Kama angekuwa mjanja angetafuta watu ambao hawajaambukizwa akawapima hata kule Uganda Halafu akawaletea watu wamaaabara sio kuwapelekea mapapai ni Aibu kubwa na pia haiwezekani tu kitaaalam

Sent using Jamii Forums mobile app
Inaelekea ukienda kushoto huwezi geuka kulia!!??
 

nabiidaniel

JF-Expert Member
Feb 25, 2014
763
1,000
Ja
SwalSwal he hao mbuz na mapapai yamekua contaminated saa ngap, kama ndo ivo basis mashine ndo IPO contaminated
We Jamaa unafurahisha, mashine ndio iko contaminated? Na mi najiuliza hivi kama yale manguo yao, sijui ndio PPE yapo contaminated hawawezi kuwaambukiza wagonjwa wanaowahudumia, au wanajipulizia dawa kila mara, au ukivaa Siku moja yanachomwa. Msaada tafadhari!!
 

mzee74

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
9,770
2,000
concern ya Raisi ni kwamba kuna uwezekano mkubwa taarifa zilizopo juu ya maambukizi ya COVID19 sii sahihi
Kwamba vile vifo 16 si vya Corona??

Kwamba zile case 480 zillizogundulika na Corona hazikuwa na Corona??

Kwamba huenda Tanzania kuna visa zaidi ya 480 ?

Toa ufafanuzi tafadhali?
 

hazard Don

JF-Expert Member
Oct 9, 2017
696
500
Mkuu nilichogundua watanzania wengi kwa sasa wana tatizo la ufahamu (comprehension) baada ya kusoma, au kusikia habari.
Sasa sijajua tatizo elimu yetu au kuna shida ya afya, au tunapoteza umakini sababu ya mihemko na hisia flani flani.

Huenda tunaongozwa na emotion bila reasoning.

Umeongea vizuri sana kwenye mada yako, tena angekuwa makini angeelewa wewe na huyo daktari aliye toa ufafanuzi mnapinga dhana ya hujuma katika vipimo na mnahalalisha matokeo aliyotilia shaka Mh. Raisi.

Kifupi unasema NDIYO inawezekana kupima uwepo wa virusi kwenye papai, mbuzi, fenesi na oil kisha vikakutwa na uwepo wa kirusi husika.
Yaani kisayansi hilo linawezekana na hakuna cha kushangaza kama alivyo shangaa Raisi au mimi na watanzania wengine.

Huyu mdau stella1975 hakukuelewa au alisoma ufafanuzi wako akiwa na mtazamo kwamba wewe umekuja kumtetea Magufuli. Kifupi na yeye alikuja na majibu yake mkononi kutokana na hasira au chuki zake kwa Magufuli.
Nimekuelewa vyema mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

mzee74

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
9,770
2,000
Wakati sample za wagonjwa zinawekwa pembeni kumbe tulikuwa tunasubri sample za mapapai na mafenesi kwa amri kutoka juu.

Tanzania tulimkosea nini Mungu?
Sampuli 652 tu zimepimwa Tz na hata hizo tuna mashaka na majibu yake. South Africa wamepima sampuli takribani laki mbili mpaka leo.
 

White party

JF-Expert Member
May 5, 2015
712
1,000
Sijui hata nilitaka kusema nini,..bandugu kila mtu ajilinde yeye na familia yake kivyake hii nchi haisomeki sahizi,. nngekua Ummy nngekua najifungia ndani naliaaaaa
 

Jerry Ekky

JF-Expert Member
May 6, 2018
783
1,000
Kwamba vile vifo 16 si vya Corona??

Kwamba zile case 480 zillizogundulika na Corona hazikuwa na Corona??

Kwamba huenda Tanzania kuna visa zaidi ya 480 ?

Toa ufafanuzi tafadhali?
Kila ulichotaja yawezekana kikawa zaid ama pungufu
 

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
14,806
2,000
Rais Magufuli ana matatizo yake. Watanzania nasi tuna yetu pia. Hatupishani sana.

Ukipita mitandaoni utaona kejeli zimetapakaa kuhusu mafenesi, mbuzi na mapapai. Kisa? Rais amesema walituma sample maabara kwa siri zikakutwa na maambukizi ya corona.

Yeye ameshangaa. Na wananchi wanashangaa. Mishangao isiyofanana.

Kwake Magufuli anashangaa kwanini sample hizo zimekutwa positive. Anadhani kuna udanganyifu. Watu wa Maabara wanatumika. Kaagiza wachunguzwe.

Wananchi wanashangaa. Wanasema Rais muongo. Inawezekanaje atume sample za mafenesi na mapapai maabara zisishitukiwe? Wanasema kipimo cha PCR kinapima sample kupitia DNA sijui RNA za binadamu.

Hakuna aliye sahihi hapo.

Kimsingi kinachopimwa maabara sio DNA wala RNA ya binadamu. Sample yoyote ikifika maabara, inapimwa RNA ya Kirusi (Viral RNA) kuthibitisha kwamba ipo kwenye hiyo sample husika au haipo.

Kupitia njia hii ya kupima samples tofauti tofauti, ndio maana kirusi cha corona kiligundulika kuwa kinaweza kupatikana kwenye mbao, ukuta, mlango, na sehemu mbalimbali nje ya mwili wa binadamu. Si ndio sababu tunanawa mikono kila mara?

Na hili liligundulika mapema kwa kuchukuliwa samples kutoka kwenye surface mbalimbali. Sasa kipi cha kushangaza kupatikana Corona kwenye sample za mapapai na mafenesi?

Nanukuu maneno ya daktari mmoja aliyetoa ufafanuzi kidogo mchana huu:

"The test (PCR) targets viral RNA not human DNA, it confirms the presence of the virus. How did they know about the virus being alive on surfaces eg. wood, metal? They swabbed the contaminated surfaces and tested. The virus lives inside and outside living things". Mwisho wa kunukuu.

I hope nimesaidia.
Zaidi ya comedy of errors ,Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
 

Jerry Ekky

JF-Expert Member
May 6, 2018
783
1,000
Huoni kwamba anajiumbua mwenyewe? Huoni kwamba yupo kinyume na waziri Mkuu .

If that is the point; Hilo swala si ni lakufanyiwa kazi internally na kurekebishwa. Kutuambia Sisi ni kuonesha udhaifu wa Serikali nzima.
Think


Mk54
Alieleza hayo sababu kiongozi wa upinzani alimtuhumu na kudai kuwa amelifanya hilo janga km lake peke yake na mwishowe anafukuza makamanda katikati ya vita
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom