Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,297
- 33,909
Kama Rais John Magufuli anasifiwa kwa kuchukua maamuzi ambayo watangulizi wake walishindwa kuchukua na pia anasifiwa kwa kufanya yale ambayo watangulizi wake walishindwa kufanya. NI kwa nini basi kina John Mnyika walipokuwa wanasema Kikwete ni dhaifu kwa kushindwa kuchukua hatua kwa uharibifu uliofanywa na Mtangulizi wake Mkapa walishutumiwa?
Kwa haya yanayofanywa na Magufuli kama vile kufukuza wafanyakazi hewa, kutaka kubadili mikataba ya madini, kufuta safari za nje, na mengine mengi si dalili kwamba mtangulizi wake alilea mambo yasiyofaa kwa nchi yetu? Wale waliokuwa wanamtetea Kikwete kwamba si dhaifu leo hii bado wanamtetea angalau kwa maneno tu? CCM ina watu wasio na msimamo kabisa!
Si kwamba kuwa Kikwete hana mambo mema alipokuwa Rais. Kwa mfano aliachilia watu wafanye walichoona kinafaa mradi hawavunji sheria, aliendesha siasa za uchangamano, alijenga haiba ya ushirika kitaifa na kimataifa. Bila shaka kwa haya wapo pia wanaomkumbuka!!