Kwanini mkulima hupangiwa namna ya kufanya biashara yake tofauti na wafanyabiashara wengine?

Mr.genius

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
1,369
1,169
Kwangu kilimo sio kujikimu, sio kulima kwaajili ya kula hiyo walishafanya ma babu zetu sasa hv tunazungumzia kilimo biashara maana yake pana mambo makubwa matatu.
1.) Mtaji
2.) Bidhaa na
3.) Soko.
Mtaji wote tunaelewa katika biashara yoyote ile mtaji ni lazima uwe umekopa, fedha yako binafsi umeingia ubia (patnership) whatever lakini mtaji ni lazima uanze nao na kwa biashara nzuri au mfanya biashara mzuri mtaji ni lazima urudi (kumbuka tunazungumzia biashara ya kilimo hapa).
Namba mbili bidhaa, hapa sasa ndio tunazungumzia zao husika mahindi, muhongo, mchele, mbaazi n.k na la mwisho kabsa (lilitakiwa kua la kwanza) ni soko sasa kuhusu hili la soko mambo mengine hapo juu yakiwa ok halaf soko likazingua bidhaa na mtaji wote unaenda na maji na kumweka mfanyabiashara katika hali ngumu.

Ndugu wana jamvi hasa wafanyabiashara wenzangu mimi nataka kuuliza kwa nini serikali yetu kwa miaka yoote hii haitaki kujifunza au kubadilisha mtazamo (sera) kuhusu kilimo na kukitambua hii ni biashara kubwa na inaweza kutupeleka onother one great step mbele? Kwanini haitaki kuangalia hii sekta ktk jicho la kibiashara zaidi badala ya kujikimu? Kwanini nasema hivi, nasema hivi kwa sabab msingi mzima wa biashara yoyote ile ni masoko. Soko ndio linaamua uuze nini sasa hivi (kipi / bidhaa / zao) gani linalipa. Soko ndio linaamua kwa kiwango gani zao lako linahitajika soko ndio linaamua bei ya soko iweje It's all about soko. Kuna wakati flani hivi media moja ilikua na kampeni yake ya kiuchumi ikawa ina slogan isemayo "ANZIA SOKONI" those guyz wanalikua wanasema ukweli kabisa kwenye ulimwengu huu wa biashara soko it's everything.

Kinachonishangaza wakat wafanyabiashara wengine waki produce bidhaa zao kwa gharama zao wenyewe kwa mitaji yao wenyewe kwa wingi ule wanaoona unayatosheleza masoko yao wenyewe na wanauza na kusambaza popote pale nchini na nje ya nchi hali ni tofauti kwa wakulima na ukichunguza vizuri ni kwamba wakulima na mamlaka (serikali) wanazungumza lugha mbili tofauti huyu anafanya ukulima as seriouz business huyu anaona ukulima ni kwaajili ya kujikimu (kupata chakula tu).

Mkulima akishazalisha mazao yake (anabidhaa tayari) basi hapo hutokea mamlaka inaanza kumpangia wapi pa kuuza, na auze lini. Tukichukulia mfano wa mahindi as the case study mkulima anavuna anaona price ya mahindi hapa nchini haimwezeshi kurudisha mtaji wake anaamua kupeleka bidhaa yake nje serikali inamwekea barn inafunga mipaka huruhusiwi kupeleka nje bidhaa yako! (utarudishaje mtaji hiyo wao haiwahusu) Kama nilivyotangulia kusema soko ndio huamua upeleke nini sokoni na kwa kiwango gani na kwa bei ipi sasa huwezi ukapeleka unga sokoni ili hali soko linataka mahindi, kuna kipindi ilikuja marufuku ya mahindi ya kuchoma katika baadhi ya maeneo kitu ambacho hatuelewani iko hivi mimi kama mfanyabiashara nimeona bidhaa flani inalipa kwa sasa nitafanya juu chini kuizalisha at the maxmum ili kufeed soko.

So kama nimeona mahindi ya kuchoma kwangu ni deal wewe unaponikataza kaa ukijua next season nitapunguza uzalishaji na nitapunguza uzalishaji effect yake mnyororo mzima wa uzalishaji mzunguko wa pesa utapungua sabab km nlikua nalima eka 10 nitalima tano (vibarua watapungua) muuzaji mbegu sitamuungisha nyingi sabab nmepunguza ekari za kulima, mbolea sitanunua kwa kiwango kikubwa hivyo tunafanya biashara hii ya kilimo kua ngumu ngumu pasipo sababu za msingi!.

Najua watawala wana hofu na kukimbilia haraka sana ku monitor mazao ya chakula kutokana na hofu ya kutokea upungufu kwa hapo baadae lakini hii hofu kwa jicho la kibiashara mimi siioni kama inamantikiti yoyote sababu kama tumeamua kua katika soko huria tuwe huria kweli kweli.

Mwisho nataka nitoe angalizo moja kama nilivyotangulia kusema hapo juu soko ndio biashara yenyewe na ndio kila kitu kwenye biashara, pana washauri wa serikali hufikiria sijui tatizo la kilimo nchini ni wataalam wa kilimo sijui nini mimi naona tatizo ni soko ndani na nje. Huwezi ukanishawishi ni mtafute mtaalam wa kilimo anielekeze kulima kitaalam nivune zaidi ili niuze gunia elf 20 (bei ya hasara) haiingii akilini pindi soko linapokua imara mkulima mwenyewe atamtafuta mtaalam si tayari ameshajua kilimo kinavyolipa. Kwa uchache mi ni hayo tu wakuu.
 
acha kulima mahindi mkuu lima bangi
hata hivyo, serikali haijakaza kuuza mahindi, inachokataza ni kuuza raw materials. unatakiwa uongeze thamani ya hayo mahindi yako kabla ya kuyauza
tunataka tutoke kwenye kuwa soko la malighafi kwenda soko la bidhaa
acheni porojo, tuungeni mkono
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom