Kwanini mkono/mguu wa kulia una nguvu na wa kushoto hauna?

Regent

JF-Expert Member
Oct 9, 2020
2,267
2,000
Ni ipi sababu ya kibailojia inayofanya mkono/mguu wa kulia kuwa na nguvu na wa kushoto kutokuwa na nguvu ikiwa ujazo wa misuli na mifupa ni sawa.
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
42,591
2,000
Ni ipi sababu ya kibailojia inayofanya mkono/mguu wa kulia kuwa na nguvu na wakoshoto kutokuwa na nguvu ikiwa ujazo wa misuli na mifupa ni sawa.

Hakuna kitu kama hicho, mikono yote ina nguvu sawa sema ni mazoea tu ndio yanakufanya uhisi kwamba wa kulia una nguvu, ukimuuliza obama atakwambia mkono wake wa kushoto ndio una nguvu.
 
The Icebreaker

JF-Expert Member
Feb 11, 2018
8,543
2,000
Swali zuri,naungana nawe kusubiri majibu,ila kwa kuongezea wapo ambao mkono/mguu wa kushoto unakua na nguvu zaidi ya wa kulia.
 
baraka bb

JF-Expert Member
Mar 20, 2016
2,543
2,000
mkono na mguu wa kulia wa nani ndo ina nguvu,,,, mbona me mguu wangu wa kushoto ndo una nguvu kuliko wa kulia
 
Regent

JF-Expert Member
Oct 9, 2020
2,267
2,000
Hakuna kitu kama hicho,mikono yote ina nguvu sawa sema ni mazoea tu ndio yanakufanya uhisi kwamba wa kulia una nguvu,ukimuuliza obama atakwambia mkono wake wa kushoto ndio una nguvu.
mkono na mguu wa kulia wa nani ndo ina nguvu,,,, mbona me mguu wangu wa kushoto ndo una nguvu kuliko wa kulia
Ninyi ni 10% katika 90% ya tunaoishi duniani, kilakitu kina kinyume duniani So ninyi ni mumeenda kinyume...
 
Tit 4 Tat

JF-Expert Member
Aug 7, 2015
666
1,000
Swali zuri,naungana nawe kusubiri majibu,ila kwa kuongezea wapo ambao mkono/mguu wa kushoto unakua na nguvu zaidi ya wa kulia.
Hata mm wa kushoto una nguvu kuliko wa kulia mm nadhani kwa sababu ndio mkono ninao ushughulisha mara kwa mara ndio maana una nguvu zaidi hii yote kwa ya kuu_training.
 
Elias Manyasi

Member
Mar 19, 2015
9
45
Mmh sio kwamba inategemea na mkono/mguu gani unaoutumia zaidi!? Mfano mm ni right footed na ndio wenye nguvu Sana. Ndivyo hvyo Kwa left footed
 
Regent

JF-Expert Member
Oct 9, 2020
2,267
2,000
Hata mm wa kushoto una nguvu kuliko wa kulia mm nadhani kwa sababu ndio mkono ninao ushughulisha mara kwa mara ndio maana una nguvu zaidi hii yote kwa ya kuu_training.
Mmh sio kwamba inategemea na mkono/mguu gani unaoutumia zaidi!? Mfano mm ni right footed na ndio wenye nguvu Sana. Ndivyo hvyo Kwa left footed
Your Wrong
Sio unanguvu kwasababu unaushughulisha bali ni unaushughulisha kwasababu unanguvu...nguvu ndio imeanza.

Swali kwanini iwe hivyo.
 
BabaDesi

JF-Expert Member
Jun 30, 2007
4,292
2,000
Samahani mpendwa Karu. Sijakuelewa vizuri hapo. Ina maana kila saa unakuwa unajisikiai hamu ya kuwa unatifuliwa na mwanaume, au?? Na ukiishatifuliwa kisawa sawa, INA maana ni baada ya muda gani hamu ya kutifuliwa inakurejea tena???
 
Lukonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
362
500
Ni ipi sababu ya kibailojia inayofanya mkono/mguu wa kulia kuwa na nguvu na wa kushoto kutokuwa na nguvu ikiwa ujazo wa misuli na mifupa ni sawa.

Nadhani jibu lake liko kwenye theory ya Darwin "Use and disuse"

Pale unapoweza kukitumia kiungo chako au viungo vyako ipasavyo, ndivyo ustadi zaidi unakuwepo na kuweza kujijenga zaidi.

Kwa kile kiungo kisichotumika ipasavyo, basi hupoteza uimara wake.
 
Regent

JF-Expert Member
Oct 9, 2020
2,267
2,000
Nadhani jibu lake liko kwenye theory ya Darwin "Use and disuse"

Pale unapoweza kukitumia kiungo chako au viungo vyako ipasavyo, ndivyo ustadi zaidi unakuwepo na kuweza kujijenga zaidi.

Kwa kile kiungo kisichotumika ipasavyo, basi hupoteza uimara wake.
Hapa kiungo kinaanza kuwa na nguvu alafu ndio unakitumia zaidi yaani mimi natumia sana mkono wa kulia kwasababu unanguvu na sio umekuwa na nguvu kwasababu nautumia sana.
 
Lukonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
362
500
Hapa kiungo kinaanza kuwa na nguvu alafu ndio unakitumia zaidi yaani mimi natumia sana mkono wa kulia kwasababu unanguvu na sio umekuwa na nguvu kwasababu nautumia sana.

Si rahisi kuthibitisha hilo.
Hatuelewi kati ya shingo ya twiga kuwa ndefu kulimwezesha kula majani au kula majani ya juu kuliwezesha shingo ya twiga kuwa ndefu.

Nafikiri kinachoanza ni utashi wa kutumia kiungo fulani na hii ni kwa urithi wa kuzaliwa/vinasaba. Na wakati huo wewe hujui suala la kupima uwezo wa nguvu kati ya mkono wako wa kushoto au kulia upi una nguvu.

Ingawa, kwa taratibu za familia nyingine mtoto huweza kukatazwa kutumia mkono wa kushoto.

Mtoto husika atahangaika na mwisho ataweza au kushindwa kuutumia. Na hapo ndo tujiulize, jee mkono utakaoimarika ni upi?
1: Alieshindwa kutumia mkono wake wa kushoto? Je upi utaimarika?
2: Aliyeweza kutumia wa kulia baada ya kuzuiwa kutumia wa kushoto? Upi utaimarika

Tujiulize pia:
1: Genetics/ vinasaba huathiri phenotype/mwonekano wa nje kwenye mazingira.

2: Phenotype/kilichopo kwenye mazingira pia huathiri uwezo wa genotype kujionyesha.

Mfano: Unaweza kuzaliwa na vinasaba vya urefu, lakini ukakutana na lishe mbovu na usiufikie urefu wako halisi.

Nani hushinda ndo huwa anabeba tunachokiona.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom