Kwanini Mkapa na Jitu Patel hawakamatwi?

Nahisi hata Muungwana na EL ni sehemu ya ufisadi. Tangu lini Kesi ya Ngedere hakimu awe nyani? After all inaonekana walifaidika na mapesa yalichotwa BoT. DAWA YAO IKO KWENYE SANDUKU LA KURA. Naomba usiku na mchana Mungu awaangazie wananchi vipofu wa Tz ili waweze kuona mabaya ya sisiemu na kufanya kweli 2010. Mungu ibariki Tanzania na UWABANIKE MAFISADI
 
Mugo"The Great";130394 said:
Nahisi hata Muungwana na EL ni sehemu ya ufisadi. Tangu lini Kesi ya Ngedere hakimu awe nyani? After all inaonekana walifaidika na mapesa yalichotwa BoT.

Kwani hao akina JITU PATELI NA WENGINE walivunja benki?
 
BabaH Karibu JF, ila hiyo yako Avatar (Kipicha) chanisumbua ! unaweza badili ukaweka kama cha Che Guevara ama Mandela? ni ombi tu babaH
 
Mimi Bado Nina Imani Kubwa Ya Kuwa Hakuna Hali Inayoweza Kudumu Milele Na Hili La Mkapa Na Jitu Patel Ni Lazima Litakuja Kuwa Wazi Tu Na Hakuna Atakayeweza Kuzuia. Kinachofanyika Sasa Ni Kuchelewesha Adhabu Tu, Lakini Ipo Pale Pale
 
kumbe blog hii ina mambo mazuri hivi, kwakweli mkapa kukamatwa sio rahisi halafu na wao wakitoka madarakani iweje?
 
NIPASHE

2008-02-28 10:39:19
Na Joseph Mwendapole

Kuhusu tuhuma kuwa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Bw. Benjamin Mkapa, alifanya biashara akiwa Ikulu, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ilisema haitamchunguza Mkapa kwa kuwa hawajapata malalamiko yoyote.

Ofisa Habari wa Sekretarieti hiyo, Bw. Augustus Karia, alisema hawawezi kufanya uchunguzi kwa maneno ya kusikia mitaani.

``Sheria iko wazi na nendeni mkasome, sisi hatuwezi kuchukua hatua hewani lazima kuwe na mtu ambaye amekuja ofisini kwetu kulalamika,``alisema.

Jitihada za kuonana na Kamishna wa Tume hiyo, Jaji Steven Ihema, kwa ufafanuzi zaidi zilishindikana baada ya kukataa kuzungumza na waandishi.

Chanzo: NIPASHE, Alhamishi 28 Feb.2008

SABABU ZA KUTOKAMATWA KWA MKAPA HIZO HAPO JUU kwee kwee kweee, hii Tanzania.....
 
Back
Top Bottom