Kwanini Mkapa??Je CCM Kugawanyika??..Yes I said Makamba Jiuzuru

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
163
Naomba kuuliza Kwanini Mkapa?
Na kwanini iwe baada ya miaka mitatu toka alipotoka serikalini,hawa wanaomsema huyu mzee ni mla Rushwa walikuwa wapi zamani kusema haya,

Rais alisema wamuache Mzee apumzike kwa amani,kwanini ameshindwa kumlida kwa sasa?
Naomba kusema kwamba Chama Chama Mapinduzi kiko Mbioni kugawanyika kama hatua za haraka hazitachukuliwa,Nafikiria upinzani wa kweli ndio uko mbioni kuanza sababu chama kitavunjika hivi karibuni.nimefuatilia kwa ukaribu siasa za chama kwa muda wa miezi mitatu iliyopita ni kwamba chama kimepoteza Mweelekeo sababu viongozi wameshindwa kuhimili mikiki ya wanasiasa,Kimsingi nina wasiwasi mkuwa na uwezo wa Mhe. Makamba katika uongozi,anakipeleka chama sehemu mbaya sababu ameshindwa kuyamaliza matatizo katika chama,hii ni ishara mbaya.kusemwa kwa mkapa navyoamini mimi kunatokana na yeye kususia shughulia za chama kwa sasa na hili ndio jinamizi linalomuandama.

Mbona wabunge wamekalia kuzungumzia kashfa za watu hawazungumzii suala la Njaa na masuala yanayohusu majimbo yao?

Ukiangalia kwa sasa vyama vya upinzani na vyombo vya habari wanazungumzia watu, badala ya kuzungumzia kazi muhimu ya chama cha mpapinzui huko mbeleni.Mambo ya nchi hayajadiliwi mathalani suala linalohusu Njaa,Rejea wito uliotolea na shirika la fedha Duniani,watu hawapewei mkazo kujiandaa na bala hili.??tuje tushtuke baadaye??
Wabunge wamekuwa watu wa kuzungumzia kashfa tu,bila kuangalia matatizo muhimu ya wananchi

Fedha za Serikali zinaliwa kwenye jimbo la Mbunge, lakini anakuja kupigia kelele Bungeni. Anaogopa kusemea kwenye jimbo lake kwa kukosa ujasiri. Hayo nayo ni mapungufu ya ushupavu wa uongozi. Halmashauri au Bunge la watu wenye haraka ya maendeleo ni mahali pa kubadilishana uzoefu wa uhamasishaji na uchangiaji maendeleo huko Wabunge na Madiwani wanakotoka, kila mmoja akieleza aliyoyafanya yeye kwenye jimbo lake, au kata yake, kusudi wengine wamuige. Tusigeuze Bunge, Baraza la Wawakilishi na Halmashauri kuwa mahali pa kumlaumu kila mtu isipokuwa wewe mwenyewe.

Je wapinzania wamejiandaa vipi kwa kugawanyika kwa CCM?

Ukiangalia Mwenendo wa matukio yanayoendelea hivi sasa,hii ni ishara mbaya wka chama cha mapinduzi na nadhani ni wakati wa upiznani w akweli kuanza sababu chama kitavurugika,Muungwana amekaa kimya kwa kile anachosema yeye ni mvumilivu,ila kuchafuana huku kulikoanza mimi nakuhakikishia kama Nidhamu ya chama haitarudi basi chama kitayumba,na bila CCM madhubuti nchi itayumba.


CCM kugawanyika kama hatua madhubuti zisipochukuliwa,na sasa naona lile suala la Muungwana to be one term president linawezakana kwa sasa.
Yes I said Makamba achia Ngazi kwa manufaa ya Chama.
 
Mkuu unajua kile hakikuwa chama kilikuwa ni fichio la maovu. Tuombe mungu waliomo walione hilo. wakifumbuka macho watakamatana wenyewe.
 
Hizi ni dalili za mambo kwenda kombo CCM
Limbani,
Mie nakuhakikishia kwa sasa CCM kila mtu ni kiongozi,kuanzaia huko chini sababu kila mtu anasema mie Fulani ndio Godfather wangu ,na yeye ndiye nayemsikiliza

wew angalia yaliyotokea Mbeya,Mwenyekiti anasema Hivi Mbunge ansema hivi??Je tutafika??hii inaonesha ni mpasuko wa Chama.

angalia suala la Zanzibara,Rais anasema ana nia hii ila kuna watu wanamkwamisha,nani kiongozi??hakuna kiongozi..ila kuna spinning Masters..
 
una akili mkuu, umeileta hoja kama unalalamika vile, kumbe ukweli ndo huo!!!
 
Mkuu unajua kile hakikuwa chama kilikuwa ni fichio la maovu. Tuombe mungu waliomo walione hilo. wakifumbuka macho watakamatana wenyewe.

Sasa naanza kupata vizuri maana ya ile kauli ya Mhe. Lowassa,"..Kama tukianza kuchafuana hapa,sidhani kama kuna mwansiasa yoyote atakeyabaki.."

hii ina amaana kama CCM wakaianza kutajana kila mtu na uozo wake,CCMhaitanaiki kuwa ile CCM ambayo watu walikuwa wameizoea,ila taizo ni nani?Mtendaji Mkuu..amehsindwa kusimamia misingi ya Chama..hii ni ushindi w achee kwa upinzania,nadhani kuna chama kipya kipo mbeleni kuanzishwa!!
 
Gembe,

Haya si ya kusikitikia kwa sababu yalikuwa lazima yaje. Kila lililo na mwanzo lazima liwe na mwisho na huu ndio mwisho wa ibara 15.1 Kila mtanzania sasa anajua jinsi nchi ilivyo na tusingejua haya bila kutokea kwa haya unayoyaona.

Acha watu wapige kelele juu ya Kasfa na ufisadi maana ndiyo wakati wake sasa. Tutaanza kuongea mambo ya njaa na uchumi na maendeleo baada ya kueleweka hili la ufisadi.

Siku za nyuma tumeongea sana suala la uchumi na maendeleo bila kugusia suala la Ufisadi, hakuna aliyethubuti kupaza sauti kwa mafisadi lakini leo tunapaza, tena ingefaa tuachane na mengine yote ili tusafishe kwanza nyumba na baadaye tulete vyombo vipya na hapo tutaongea maendeleo ya kweli.

Tulifikia kipindi tunaongea suala la njaa mwenzio anatafakari namna ya kuitumia hiyo njaa kunufaika hili liko wazi hata tulipopata matatizo ya umeme unajua kilichotokea. Watu walifika hatua kuonmbea majanga yatokee au hata ku-create majanga ili wanufaike.

Hivyo tuache wabunge waseme juu ya ufisadi maana ni wakati wake. tusafishe nyumba kwanza.
 
Marafiki Wa Jk Wanasema Mzee Yuko Ktk Right Track Ya Kuinyosha Nchi Ktk Chama Na Serikali, Nadhani Tumpe Nafasi Ya Kuinyoosha Nchi Kama Alivyoadhamia, Nakumbuka Kusoma Humu Coridoni Mwetu Jf Kuwa Kuwa Hii Ndio Ilikuwa Dhamira Yake Ya Kuichukua Nchi Na Kuirudisha Kwa Wananchi, Let's Wait Coz Weupe Wana Msemo Time Will Tell
 
Bora kuyazungumzia sasa yanayomhusu Mkapa kuliko kutoyazungumzia kabisa, aendelee kutanua tu.
 
Marafiki Wa Jk Wanasema Mzee Yuko Ktk Right Track Ya Kuinyosha Nchi Ktk Chama Na Serikali, Nadhani Tumpe Nafasi Ya Kuinyoosha Nchi Kama Alivyoadhamia, Nakumbuka Kusoma Humu Coridoni Mwetu Jf Kuwa Kuwa Hii Ndio Ilikuwa Dhamira Yake Ya Kuichukua Nchi Na Kuirudisha Kwa Wananchi, Let's Wait Coz Weupe Wana Msemo Time Will Tell
marafiki wakati mwingine wanaweza kukupotosha..Na kweli wanampotosha Mzee wa watu,nilishawahi kuonyoa kuhusu hili kwa kuandika Barua ya Wazi kwa Mhe. Rais kulezea masikitiko wangu,na kuna kipindi alishakiri kuwa kuna watu walimpotosha akamfukuiza mtu kazi.Kama Rafiki zake ndio wanakigawa Chama kwa kukibadili kuwa chama cha wafanyabiashara ndio kukiweka katika Right Track??hawa kina RA ndio hawa hawa wanomshauri??

sitaki Rais ambaye anapenda kuvumilia kwa kipindi kiferu,huu uvumilivu ndio unaoleata mipasuko hukjo Zanzibar.

Yawezekana Tatizo sio kikwete,Tatzio ni hawa watndaji wanaowabusu wafanyabiashara,wamejaa uozo.Ni Heri wachie Ngazi kama wameshindwa kuwa in the right track.

Yes am saying again,Makamba you should go out!
 
Naomba kuuliza Kwanini Mkapa?
Na kwanini iwe baada ya miaka mitatu toka alipotoka serikalini,hawa wanaomsema huyu mzee ni mla Rushwa walikuwa wapi zamani kusema haya,

Mkuu hiii haijakaa sawa, hebu fafanua kidogo?
 
Jibu la kwanini Mkapa kwanini this time ni rahisi sana. Kwanza akiwa ni mkuu wa nchi wa kipindi yalipotokea madudu haya, lazima aliyaona, sasa atueleze kwanini aliufumbia macho wizi na unyang'anyi huu. Why now? Kwa sababu issue hii ingetolewa mapema machozi yangeenda na maji, sasa hivi ni kwamba tunaelekea kwenye 2010 ambako naamini haya yote majibu yake yatasahihishwa mwaka 2010, kuibua issue kama hii sasa hivi ni vizuri, kwa sababu wale jamaa wanapenda kucheza buy time game watafika nayo kwenye kampnei za uchaguzi 2009, so inaonekana kama imeanza kwenye muda muafaka kabisa!
 

Naomba kusema kwamba Chama Chama Mapinduzi kiko Mbioni kugawanyika kama hatua za haraka hazitachukuliwa,Nafikiria upinzani wa kweli ndio uko mbioni kuanza sababu chama kitavunjika hivi karibuni.nimefuatilia kwa ukaribu siasa za chama kwa muda wa miezi mitatu iliyopita ni kwamba chama kimepoteza Mweelekeo sababu viongozi wameshindwa kuhimili mikiki ya wanasiasa,Kimsingi nina wasiwasi mkuwa na uwezo wa Mhe. Makamba katika uongozi,anakipeleka chama sehemu mbaya sababu ameshindwa kuyamaliza matatizo katika chama,hii ni ishara mbaya.kusemwa kwa mkapa navyoamini mimi kunatokana na yeye kususia shughulia za chama kwa sasa na hili ndio jinamizi linalomuandama.[/FONT][/COLOR][/U][/I]



Rejea vikao vya muafaka taarifa aliyopeleka Butiama,Je ndicho walichozungumza miezi 14 na wawakilishi wa CUF?ushauri wa bure cheo,ambacho kingemfaa ni cha propaganda kama walivyo msabaha yule wa ZNZ na Tambwe.Kule huhitaji kuumiza kichwa ni kupiga domo na vichekesho kibao.
 
Gembe,acha hadithi za alnacha, sasa si wakati wa kuwalaumu wabunge,CCM walikuwa madikteta, mbunge asingeweza kusema chochote, na kama angesemwa angeitwa chemba na akaonywa ili asiikosoe ccm,hivyo tambua kuwa sasa wabunge wamefunguliwa plasta walizofungwa kwa miaka mingi. Wewe unamtetea mkapa, kakupa nini mwenzetu? Unajua Mkapa analipwa sh milioni(146) kila siku? pesa za walipa kodi?Naomba ujilekebishe ulete hoja zenye nguvu wala si hoja hafifu.
 
Gembe,acha hadithi za alnacha, sasa si wakati wa kuwalaumu wabunge,CCM walikuwa madikteta, mbunge asingeweza kusema chochote, na kama angesemwa angeitwa chemba na akaonywa ili asiikosoe ccm,hivyo tambua kuwa sasa wabunge wamefunguliwa plasta walizofungwa kwa miaka mingi. Wewe unamtetea mkapa, kakupa nini mwenzetu? Unajua Mkapa analipwa sh milioni(146) kila siku? pesa za walipa kodi?Naomba ujilekebishe ulete hoja zenye nguvu wala si hoja hafifu kama hii.
 
Gembe,acha hadithi za alnacha, sasa si wakati wa kuwalaumu wabunge,CCM walikuwa madikteta, mbunge asingeweza kusema chochote, na kama angesemwa angeitwa chemba na akaonywa ili asiikosoe ccm,hivyo tambua kuwa sasa wabunge wamefunguliwa plasta walizofungwa kwa miaka mingi. Wewe unamtetea mkapa, kakupa nini mwenzetu? Unajua Mkapa analipwa sh milioni(146) kila siku? pesa za walipa kodi?Naomba ujilekebishe ulete hoja zenye nguvu wala si hoja hafifu.

Hivi tayari ameshaanza na kulipwa? Na umeme ameshaanza kuzalisha?
 
Gembe,acha hadithi za alnacha, sasa si wakati wa kuwalaumu wabunge,CCM walikuwa madikteta, mbunge asingeweza kusema chochote, na kama angesemwa angeitwa chemba na akaonywa ili asiikosoe ccm,hivyo tambua kuwa sasa wabunge wamefunguliwa plasta walizofungwa kwa miaka mingi. Wewe unamtetea mkapa, kakupa nini mwenzetu? Unajua Mkapa analipwa sh milioni(146) kila siku? pesa za walipa kodi?Naomba ujilekebishe ulete hoja zenye nguvu wala si hoja hafifu kama hii.
Hadithi ipi hapo nimetoa,kamwe sipendi hadithiCCM ni chama,udikteata ni tabia ya Mtu,Wabunge sio walikuwa hawasemi chochote,nachoweza kukwambia wabunge wamakuwa na kiburi cha kuongea kwa sasa baada ya CCM kuparanganyika kipindi cha uchaguzi,kila mtu ana kambi yake ..na sasa kinachofanyika ni ule ushabiki wa muaribie huyo..

Mkapa amiliki kampuni hiyo ambayo Yona anamiliki,na hata ukienda Pale BRELLA hakuna faili linaloonyessha Kiwira coal minning inamilikiwa na Mzeee Mkapa.

Hoja zenye nguvu ni zile za kulipua mabomu tu?zile za Mzindakaya wa Zamani.kimsingi Bunge sasa hivi hakuna kitu,wabunge waejaa ushabiki tu wa mambmo huku wakiacha mambo yanayohusu majimbo yao bila kushughulikiwa,this is what i can tell you.

kila Mbunge anatafuta umaarfu wa kumlipua flani,na mara zote hawajali shida wazipatazo wananchi.embu fikiria kwa umakini wananchi wa Nantumbo wana matatizo mangapi ambayo Mbunge wao hawajayasemea?

Kuna suala la Bei ya vyakula kupanda ,Je kuna Mbunge yeyote aliyeshapeleka Hoja Binafsi juu ya tahadhari ya chakula cha ziada??

kuna suala la Malbino,Mwnakijiji aliwasaidia kwa kuwapa jambo la kuanzia,je kuna mtu amepeleka hja binafsi juu ya hili?

Kuna suala la vyombo vibovu vya kupimia VVU,Je kuna mtu kaliongelea hili,au kwasabababu linawagusa wadogo??

kuna suala la Daraja la kigambano,e kuna mtu aliyehsapeleka hoja binafsi juu ya hili??

Kuna suala la Mfumo mbovu wa majitaka katika Jiji la dar es salaam,hasa wakati wa kipindi cha mvua,Huyu Mbunge wet alishalisema hili?

nenda Baadhi ya maeneo ya kimara,Msewe,sinza na temeke hakuna maji ,Je ni nani alishalisemea hili..??

Hoja na kero za wananchi ni nyingi na hazijasimamiwa ipasavyo ,wabngwe wamekuwa watu wa kushadadia kashfa tu za watu na hakuan hatua zozote wanazochukua baada ya kuwaadhibu.

Angalia suala la kina Lowassa,Je ni nani ametoa hoja binafsi ya kutaka kujua progrees ya pesa za RDC zimefikia wapi?kwanini hawambani Pinda kipindi cha Alhamisis asemehe haya?

Tunaenda wapi?tunaelekea wapi?tuwakome giladi mafisadi ila tuangalie wananchi wetu walitumia vitu gani??

Nayasema haya sababu Jumamosi iliyopita nilikuwa Dodoma,na kuwasikia wabunge wakiwa wnapiga soga kujua nanai kafaya hivi nani kafanya vile na nani atakuwa kinara wa kutoa mabomu kwa mwaka huu.

Wakati mwingine hata kauli ya Lowassa inaweza ikawa ina maan,"..labda sababu ni uwaziri mkuu.."

naomba kuwasilisha,
 
Rejea vikao vya muafaka taarifa aliyopeleka Butiama,Je ndicho walichozungumza miezi 14 na wawakilishi wa CUF?ushauri wa bure cheo,ambacho kingemfaa ni cha propaganda kama walivyo msabaha yule wa ZNZ na Tambwe.Kule huhitaji kuumiza kichwa ni kupiga domo na vichekesho kibao.
Ukitaka kujua mtu ni kiongozi bomu,utamjua kwa vitendo.Wewe na akili yako unakwenda kununua watu ili wakusaide propaganda wati una watu kbao wamekuzunguka,inaonesha ni uoga wa khali ya juu.

Hawa kina Hiza ni kama watumwa,utakubaje kununuliwa??mie tena kwa kuanzia ..nadhani Vijana tuamke,na nitamsupport J.J Mnyika for 2010. pale Ubungo..

nadhani geeque,kaba na hii www.johnmnyika2010.com
 
1.
Gembe
Re: Kwanini Mkapa??Je CCM Kugawanyika??..Yes I said Makamba Jiuzuru

2.
FDR
Mtendee haki Gembe mkuu, yuko wazi ktk kila mstari ulio na maneno yake.

1. Mkuu FDR acha jazba, nimeomba ufafanuzi kwanza ndio nitoe hukumu sasa nitende haki ipi hiyo bilka kujua charges?

2. Kwa kutumia hicho kichwa cha habari, kwamba eti CCM itagawanyika kwa sababu ya mkapa? Au kwa sababu ya kutaka achunguzwe? Kwa sababu siioni sababu yoyote ya msingi hapo ya kuifanya CCM iliyokuwepo kabla mkapa hajajiunga nayo (TAA) ya kina Doss Aziz ivunjike, haitavunjika, lakini makpa atachunguzwa na kufikishwa kwenye sheria.

3. Hivi Gembe, hebu kuwa mkweli hivi Makamba toka amekuwa katibu wa CCM, naomba nitajie one thing as a policy au utekelezaji alichowahi kufanya ambacho ni so bad kwamba anahitaji kujiuzulu? Amekaa muda gani kwenye hiyo nafasi kiasi kwamba amevuruga tayari na anahitaji kuondoka?

Ndio maana mkuu FDR niliomba ufafanuzi zaidi, je sasa ninaweza kuupata?
 
Back
Top Bottom