Kwanini Mkapa amekosa tena tuzo ya Mo Ibrahim? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Mkapa amekosa tena tuzo ya Mo Ibrahim?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 7, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,611
  Trophy Points: 280
  Kwa nini Mkapa amekosa tena tuzo ya Mo Ibrahim?

  Joseph Mihangwa Novemba 5, 2008
  Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

  KWA mara ya pili mfululizo, kuanzia mwaka jana, na tena mwaka huu, Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa, ameikosa tuzo ya kila mwaka ya Mohamed Ibrahim inayotolewa kwa kiongozi wa Afrika mstaafu aliyeonyesha na kuthibitisha kuwa mtawala bora wakati wa uongozi wake.

  Lengo la tuzo hiyo ni kutambua mchango wa viongozi wa Afrika ambao wamesimama imara kuondoa umasikini na kuendeleza mazingira mazuri ili nchi zao ziweze kujitegemea.

  Tuzo hiyo, ambayo hutolewa kwa mtu mmoja mmoja, kila mwaka, ina thamani ya dola za Kimarekani milioni tano (6.5m/=) anazolipwa mshindi papo hapo, na dola 200,000 (240m/=) hadi atakapofariki. Walengwa ni marais wastaafu ambao hawajamaliza miaka mitatu tangu kustaafu.

  Kwa hiyo, kushindwa tena kwa Mkapa kuipata tuzo hiyo mwaka huu, ina maana kwamba imemponyoka moja kwa moja, kwa sababu mwakani atakuwa amepoteza sifa katika kinyang'anyiro hicho; kwa kuwa atakuwa amevuka miaka mitatu tangu astaafu.

  Mara ya kwanza (2007) mshindi wa tuzo hiyo alikuwa Rais mstaafu wa Msumbiji, Joachim Chissano, na mwaka huu, (2008) tuzo imekwenda kwa Rais Mstaafu wa Botswana, Festus Gontembaye Mogae aliyeiongoza nchi hiyo tangu 1998 hadi Aprili, 2008. Wengine mbali na Mogae na Mkapa, waliochuana katika kinyang'anyiro hicho ni marais wastaafu Olesagun Obasanjo wa Nigeria na Ahmed Tejan Kabbah wa Sierra Leone.

  Ni mambo yapi yamemfanya Mzee Mkapa aikose tuzo mara mbili wakati akina Chissano na Mogae, maraisi wasio na majina makubwa barani Afrika kuipata kwa urahisi? Kwa nini mwanadiplomasia huyu mahiri, aliyewahi kuwa Mwenyekiti mwenza pekee wa Tume ya Dunia ya Utandawazi kutoka Afrika, ameshindwa kuwika?

  Yapo mengi, lakini hatutamtendea haki Mzee wetu Mkapa kwa kuanza na mapungufu yake bila kutaja mazuri aliyotenda. Kwanza ni zile juhudi zake za mwanzo za kampeni dhidi ya rushwa, alipounda Tume ya Jaji Warioba ya kubaini mianya ya rushwa.

  Pili, ni jitihada zake za kudhibiti mfumuko wa bei, ujenzi wa miundombinu ikiwa ni pamoja na majengo ya kisasa na barabara. Tatu, aliweza kurudisha heshima ya wafanyakazi wa umma kwa kuwaongezea mishahara, marupurupu na mafao ya uzeeni. Nne, alipanua na kuboresha mfumo wa elimu ikiwa ni pamoja na kuongeza udahili wa wanafunzi Vyuo Vikuu.

  Lakini mapungufu ya Mkapa yalikuwa mengi vilevile kama kiongozi wa nchi. Ukatili wake dhidi ya wapinzani wa kisiasa na wasioafikiana naye kwa jambo, ulikuwa haufichiki. Watanzania hawatasahau ubabe wake dhidi ya wapinzani kwenye chaguzi zote ndogo kwa matumizi ya nyenzo na nguvu kubwa za dola kuminya demokrasia. Ingelikuwa enzi za Mkapa, leo, CHADEMA kisingeshinda uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime mwaka huu.

  Hakuna asiyejua pia jinsi alivyotumia nguvu ya fedha na matajiri kuteteresha demokrasia ya uwakilishi nchini, na kuruhusu siasa kuvamiwa na matajiri waliongia kwa lengo la kujinufaisha na kupora utajiri wa nchi.

  Ni wakati wa utawala wake kwamba utajiri ulinunua siasa na siasa ilinunua na kujilimbikizia utajiri. Viongozi walitawaliwa na tamaa ya utajiri badala ya kutumikia kwa wema. Matajiri waliojaribu kujiunga na upinzani walivurumishwa na biashara zao zikafa.

  Ule usemi kwamba "Ukitaka biashara yako ikunyokee, jiunge na Chama tawala" haukuwa wa bure. Ulikuwa ni ubaguzi dhahiri unaokiuka haki za binadamu na Katiba ya nchi.

  Wasomi na wanaharakati waliotoa chamgamoto ya kweli juu ya ujenzi wa demokrasia na utawala bora nchini, walionja hasira ya Mkapa. Jenerali Ulimwengu, mwanaharakati, mwandishi, mwanasheria na mwanadiplomasia makini, alivuliwa uraia kwa sababu tu aliweza kuikosoa Serikali ya Mkapa.

  Kwa nini tusiamini hivyo; wakati Ulimwengu huyo huyo aliweza kushika nyadhifa nyingi ndani ya Chama na Serikali zikiwemo ukuu wa wilaya na ubunge? Aidha, alikuwa mmoja wa timu ya kampeni ya Mkapa 1995 na mmoja wa washauri wake wakati wa kuunda baraza lake la kwanza la mawaziri.

  Ulimwengu amekuwa mwakilishi wa Tanzania katika Shirikisho la Vijana barani Afrika (PYM) nchini Algeria kwa zaidi ya miaka 10, ametumikia sekta ya habari serikalini wakati wa ukiritimba kwa miaka mingi. Iweje 2003, ghafla-bin-vuu awe si raia wa Tanzania?

  Aliyekuwa mhadhiri wa sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wakili na mwanaharakati, Dokta Masumbuko Lamwai, ilipodhihirika kwamba yeye ni ngome ya chama cha NCCR – Mageuzi, alipoteza wadhifa wake UDSM, akafungiwa pia uwakili Tanzania Bara, akapoteza ubunge jimbo la Ubungo na udiwani wa Manzese.

  Aidha, ni Rais Mkapa aliyeshinikiza Amani Abeid Karume agombee urais Zanzibar licha ya kushindwa katika kura za maoni kwa kushika nafasi ya tano, chini ya Dakta Gharib Bilal, Ahmed Hassan Diria, Amina Salum Ali na Abdisalaam Issa Khatib.

  Mauaji ya watu 26 walioandamana Zanzibar, mwaka 2001, yalitokea wakati wa Serikali ya Mkapa na kuchafua sura ya demokrasia nchini. Wakati wa utawala wake, Mkapa alijenga utaratibu wa kuhamishia ofisi ya Rais kila mara Bunge lilipokaa Dodoma, ili kufuatilia kwa karibu mienendo na kauli za wabunge bungeni; hasa wenye kupenda kuhoji mwenendo wa serikali yake.

  Ni Mkapa, kama Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, aliyekemea kwa kuwatisha wabunge wenye tabia ya kuhoji, kwamba asingewapitisha kugombea ubunge muda wao ukiisha. Mkapa alikuwa mkeketaji mkubwa wa demokrasia ya uwakilishi.

  Hakuwa na watu; hakuwa mtu wa watu, alikuwa mtu wa Serikali tu. Hakupambana na umasikini wa wananchi; bali alipambana na umasikini wa Serikali, akaona fahari kuona uchumi wa Taifa ukikua, wakati uchumi wa wananchi ukiendelea kudidimia.

  Hii inathibitishwa na ukweli kwamba, alikurupuka kuanzisha Mkakati wa Kupambana na Umasikini na Kuinua Uchumi Tanzania (MKUKUTA) mwaka wa 10 mwishoni mwa awamu yake.

  Hii ni kwa sababu maendeleo na ubabe aliouonyesha havipikwi chungu kimoja vikaiva. Shabaha ya maendeleo ni kuongeza uhuru na maisha bora ya wananchi; shabaha hiyo haiwezi kutimizwa kwa nguvu.

  Kuna mambo muhimu mawili katika maendeleo ya watu: Kwanza ni uongozi wa kueleza. Mkapa alipungukiwa uongozi wa aina hiyo; kwani alikuwa mvivu wa kueleza, aliwaita "wavivu wa kufikiri" au "wenye wivu" wale waliothubutu kuhoji utawala wake.

  La pili, ni demokrasia katika kuamua mambo; kwani uongozi siyo kuwakemea watu; maana yake siyo kuwatukana watu au kikundi cha watu usiokubaliana nao; wala maana yake si kuwaamuru watu kutenda hili au lile.

  Uongozi maana yake ni kuzungumza na kushauriana na watu, ukiwaeleza na kuwashawishi. Mzee Mkapa hakuwa na lugha wala ari ya ushawishi. Alijua sana kufoka na kuumbua watu.

  Wala uongozi hauwezi kuchukua nafasi ya demokrasia. Uongozi lazima uwe sehemu ya demokrasia kwamba, watu wenye mawazo tofauti, hata wakiwa wachache, lazima wawe na haki ya kutoa mawazo yao bila ya hofu wala kusumbuliwa. Mawazo yao yashindwe katika hoja, siyo kwa vitisho na mabavu.

  Alisahau nasaha za Mwalimu Nyerere juu ya ubaya wa majigambo katika kitabu "Binadamu na Maendeleo" kwamba, "Tanzania ni ya Watanzania, na Watanzania ni wote. Hakuna mtu mwenye haki ya kusema, "Mimi ndiye watu", wala hakuna Mtanzania mwenye haki ya kusema "Najua linalowafaa Watanzania, na wengine ni lazima wafuate. Watanzania wote lazima waamue mambo ya Tanzania".

  Mkapa, kama alivyokuwa Mfalme Louis wa XVI wa Ufaransa kabla ya kuangushwa na Mapinduzi ya 1789, alikaribia udikteta uliokubuhu, mithili ya kukaribia kusema "Mimi ndiye Taifa na Taifa ndilo mimi".

  Mkapa alitelekeza mapambano dhidi ya rushwa mapema ambapo si tu aliungana hima na utamaduni wa rushwa; bali pia aliruhusu chama chake kikumbatie rushwa katika chaguzi ikapewa jina la "Takrima".

  Mkataba mbovu wa IPTL ulitiwa sahihi wakati wa utawala wake. Na ingawa alionywa mapema, na alikuwa na uwezo wa kuuzuia kabla ya kuleta madhara, lakini aliunyamazia kimya. Leo, Taifa linaporwa Tshs. 3.6bn/= kwa mwezi kwa umeme usiokuwapo, na itaendelea hivyo kwa miaka 20 ijayo.

  Ni wakati wa Mkapa uporaji wa mabilioni ya fedha za EPA ulipofanyika; na ndiye pia aliyemwajiri kinara wa mtandao wa uporaji huo, hayati Daudi Balali.

  Mzee Mkapa, licha ya kukumbushwa kwamba Ikulu ni mahali patakatifu, alikwenda kinyume cha uongozi mwaka 1999 kwa kuanzisha (biashara) kampuni binafsi ndani ya majengo ya Ikulu inayojulikana kama ANBEN LTD; huku yeye na mkewe wakiwa wakurugenzi.

  Na mwaka 2002 kampuni hiyo ilipewa mkopo wa dola za Kimarekani 500,000 (hs. 620m/=) na Benki ya CRDB.

  Mlamba asali haishii kuchovya mara moja. Mkapa, kwa kushirikiana na Waziri wake wa Nishati na Madini, Daniel Yona alianzisha Kampuni ya umeme ya "Tanpower Resources," ambayo mwaka 2005, karibu na kung'atuka kwake, aliitumia kununua hisa za mgodi wa Taifa wa makaa ya mawe wa Kiwira kwa ajili ya kuuza umeme kwenye gridi ya Taifa.

  Na ingawa thamani ya mgodi huo ilikuwa zaidi ya TShs. 340bn/= ulithamanishwa upya chini ya bilioni moja, na Tanpowers Resources ikalipa chini ya kiwango kipya na kukabidhiwa mgodi.

  Ndiyo kusema kwamba, Mzee Mkapa alianza kufanya biashara na Serikali aliyokuwa akiiongoza akiwa madarakani, na hilo hajakanusha mpaka sasa. Zipo tetesi pia kwamba alijipatia ubia wa kibiashara katika kiwanda cha Sukari cha Mtibwa, wilayani Mvomero, sambamba na shamba la miwa la ekari 600 eneo la Dizungu wakati akiwa Rais.

  Vivyo hivyo inadaiwa kuwa alikuwa mbia katika Benki tata ya "Bank M" na pia alimweka jamaa yake katika menejimenti ya kigeni iliyokuwa ikiendesha Shirika la Umeme nchini, (TANESCO), kampuni ya Net Group Solution.

  Kampuni hiyo iliingia na kuchukua ofisi za TANESCO kwa ulinzi mkali baada ya watumishi na umma, kwa ujumla, kuonyesha kutokuwa na imani na madhumuni ya kampuni hiyo. Kama ilivyotabiriwa na umma wa Kitanzania, Net Group Solution ilibwaga manyanga na kuiacha TANESCO ikiwa hoi. Serikali haijakiri kosa lake mpaka leo.

  Kuongoza ni kumulika njia. Kwa kiasi kikubwa Rais Mkapa alishindwa kumulika njia. Na kwa sababu hii ndio maana ameikosa tuzo ya Mo Ibrahimu mara mbili mfululuzo licha ya umaarufu wake Kimataifa.

  0713-526972

  jmihangwa@yahoo.com [/email]
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,611
  Trophy Points: 280
  Nadhani hapa kuna makosa. Kama sikosei thamani ya Kiwira Coal Mine inasemekana ni shilingi bilioni nne. Kama kuna yeyoye hapa anayeweza kupata thamani halisi ya mgodi huo labda kutoka STAMICO aiweke hapa.
   
 3. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Shilingi bilioni nne? Thats less than four million dollars, that's house money, kama unataka kuchimba some deep holes in the ground and process some serious coal I would think the equipment alone should cost more than that.

  But then again I am not sure if Kiwira is mgodi or kimgodi.
   
 4. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  maelezo ni mengi na mwandishi anaonekana kuongozwa na HISIA zaidi. kuna maeneo yenye ukweli kuhusu upungufu wa utawala wa MKAPA ila HISIA zimezidi.
  mwandishi anaonekana kulilia sana Jenerali ulimwengu kunyanganywa uraia eti ni mtu alityelitumikia taifa nyadhifa mbalimbali na alikuwa kwenye timu ya kampeni ya mkapa. sawa je ikibainika kuna hitilafu kwenye uraia wake isifuatiliwe?

  pili mkapa pamoja na mapungufu yote bado anabakia kiongozi imara katika taifa hili katika kujenga uchumi ndo maana KWENYE MO IBRAHIM AWARD ni MSHINDANI MAKINI. Ataendelea kubakia mtu na kiongozi thatbiti aliyetambua mahitaji ya taifa lake kwa wakati wake. cha msingi kama ulivyotaja mapungufu ya utawala wake, BADO chama chake naona kipo madarakani na hakina budi kurekebisha ili kiendelee kuaminiwa na si KUTULAGHAI.

  Binafsi bado naamini matatizo ya taifa hili yatatatuliwa na viongozi makini waliotokana na JAMII IMARA. Tujenge taasisi imara za kuongoza ili tupate watu makini.
  Tanzania ni taifa nasi ni sehemu yake na tunapita lenyewe litakuwepo kwa siku zijazo.
  Kuhusu MKUKUTA kama mpango wa kurekebisha uchumi labda utupe mpango mbadala maana naona bado watumika kuendeshea nchi na kuomba misaada ya kiuchumi.
  KWA TAARIFA TUU NI LINI TUMEKUWA NA VISION YA KITAIFA BAADA YA AZIMIO LA ARUSHA KUFAA???????
   
 5. M

  Masatu JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkataba wa IPTL haukusainiwa wakati wa serikali ya Mkapa bali Mwinyi mwandishi hajafanya homework yake vizuri
   
 6. B

  Bull JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2008
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uimara gani aliokua nao Mkapa wakati anasign mikataba isiyo nufaisha taifa bali yeye na familia yake, si ndo yeye alie jilimbikizia mimali, majumba na wengine kuwarithisha rafiki zake? Hivi hujui JK hadi sasa bado anarekebisha uchafu wake Mkapa? Amakweli mwenyekupenda haoni!

  Tunamsubiri Mkapa Mahakamani na kama JK ataendeleakumkingia kifua, wananchi wenye hazira watapambana nae
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Wote wawili hamna tofauti.
   
 8. K

  Kjnne46 Member

  #8
  Nov 12, 2008
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Awali ya yote, huko kukosa kwa hili Tuzo miaka miwili mfululizo INAMAANISHA KUWA MKAPA HAKUSTAHILI KUWEPO KATIKA ORODHA YA MARAIS WA KUFIKIRIWA (eligible and QUALIFIED candidates). Vinginevyo, ni zipi sababu zilizomkosesha Tuzo hilo 2007 lakini "sifa' zingine zikaongezeka 2008?
  Pili, Nyauba hajajibu MADA iliyowasilishwa bali "amekosoa" tu kuhusu Jenerali Ulimwengu na kuyataja yale "mafanikio" ya Mkapa eti kiongozi makini wakati wananchi amewaacha maskini kuliko alipoingia madarakani!

  Tatu, mbona hiyo "hitilafu ya uraia" wa Ulimwengu ilifuatiliwa kwa nguvu zote za dola baada ya kuchapishwa taarifa ya vifo vya hao Wazanzibar 26 na akaandika kuwa "Rais Mkapa anaendelea ziara yake ‘majuu' badala ya kuikatisha na kurudi nyumbani kutokana na huo msiba mkubwa wa Taifa!" (maneno halisi ya ‘Mtanzania'? siyakumbuki). Tukio hilo ni sawa na yale yaliyompata Prof. Hamza Njozi alipomtaja Mkapa katika kitabu chake Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania kuhusiana na Hotuba yake ya 04 Novemba Bungeni Dodoma na Mkapa akaamua kukipiga marufuku hicho kitabu mpaka leo that ban is not lifted.

  Ndio, Mkapa ana hasira, ukali na ubinafsi na wala hajali maslahi ya Wananchi! Isitoshe, hayaonekani hayo maendeleo ya Mtanzania wa kawaida aliyoyapata katika utawala wake. Ni kukua gani kwa uchumi unakozungumzia, Nyauba? Those economy growth reports are cooked figures which any good Accountant can produce to impress the International Community!!


  KWA KUHITIMISHA, NASEMA KUWA MKAPA HASTAHILI KUPEWA HIYO TUZO SIO TU KWA SABABU "HAKUFIKIA KIWANGO KINACHOTAKIWA NA MO IBRAHIM AWARD" BALI PIA ANA MADHAMBI KIBAO NA UFISADI UNAOMKABILI BINAFSI!!
   
 9. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Jibu ni EPA
   
 10. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #10
  Nov 12, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Tule ni tujisenti kidogo tu; hatumkoseshi usingizi kabisa Mzee Mkapa. Kwani hata yeye anaweza kutangaza kutoa tuzo za aina hiyo kutoka mfukoni mwake!!

  teh!!!!! teh!!!!!teh!!!!!teh!!!!!teh!!!!!
   
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  Nov 12, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Very strong!
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Nov 12, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,611
  Trophy Points: 280
  Naam Watanzania tuna kila sababu za kumfikisha fisadi huyu mahakamani maana nia tunayo, uwezo tunao na sababu pia tunazo.
   
 13. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #13
  Nov 13, 2008
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  TUSISUKUMWE NA HISIA ZA KIDINI, UKABILA, MAKUNDI NA CHUKI BINAFSI KTK KUMHUKUMU MKAPA, NINA MASHAKA NA MWENENDO NA MAANDISHI YA MIHANGWA, NA WEWE NILIYEKUNUKUU HAPA, NIMEMSOMA PIA BAGENDA KTK LILE GAZETI LAKE LAKINI NI MTIZAMO WA WENGI WA WAANDISHI NA BAADHI YA WATU WENYE HESHIMA ZAO KIDOGO KTK JAMII, HUENDA WENZETU MNGEPENDA TUAMINI KUWA MKAPA IS THE WORST PRESIDENT EVER IN AFRICA +TZ, SASA TANGIA 2005,21.DESEMBA MPAKA SASA WATU WALIONEKANA KUWA JAPO MAKINI HUKO NYUMA KWAO HABARI NA HOJA NI MKAPA. NILIWAHI PINGANA NA MKUU WA MEDANI KUWA HAITATOKEA BENJAMIN WILLIAM MKAPA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KAMA YEYE ALIVYOBASHIRI, NA ILIFIKIA PAHALA MKUBWA WANGU FMES AKAONYESHA HASIRA YAKE WAZI KWANGU NA KUNITUHUMU KUWA NINAMFUATAFUATA, NIKAMWELEZA MIMI NI KIJANA MDOGO SANA TENA SI WA DARAJA HILO HIVYO ASIPOTEZE NGUVU ZAKE ZAKE NA MUDA MWINGI JUU YANGU PERSONALLY BALI AENDELEE KUTUPATIA SHULE AMBAYO DAIMA NINAIHESHIMU SANA. SASA NINATOA WITO KWA MIHANGWA NA WEWE MFANYE HIMA KUMFIKISHA MKAPA MAHAKAMANI ILI KWELI IBAINIKE, ILA KUENDELEA KUTUIBIA MIA TANO TANO ZETU KWA MAKALA YA KWANI MKAPA KANYIMWA TUZO YA MO IBRAHIMU, HAPANA HILO NALIKATAA. HUU NI MSIMAMO WANGU AMBAO NITAUSIMAMIA DAIMA, KAMA UNAMTUHUMU MTU USIISHIE KUPIGA DOMO, THIBITISHA WEWE MBELE YA SHERIA. MKAPA KAMA NI MUUAJI WA WAPEMBA SAWA KABISA MAANA TUNAANGALIA TULIPOANGUKIA NA SI PALE TULIPOJIKWAA, WAPEMBA WALIHITAJI LILE SOMO NA NDIO MAANA 2005 MAPAKA SASA HATUJASIKIA WAKIJISAIDIA KTK VISIMA VYA MAJI NA WALA KUPORA SILAHA KTK VITUO VYA POLISI. MWEMBECHAI, NI MATOKEO YA UNAFIKI WA BAADHI YA VIONGOZI NDANI YA JAMII YA KIISLAMU NA WAISLAMU WALIOKUWEPO SERIKALINI, YEYE KAMA MKUU WA NCHI ANAWAJIBIKA KUMHAKIKISHIA KILA MWANANCHI USALAMA WAKE HATA KAMA KWA KUFANYA HIVYO AMEJIKUTA AKIKOSANA NA WAISALAMU, NASEMA ALITEKELEZA WAJIBU WAKE BILA HOFU. PROF.nJOZI NI MTU RADICAL, MPOTOSHAJI WA MAKUSUDI AILI MRADI TU AONEKANE MBELE YA HADHIRA YA KIISLAMU KUWA NI MUUNGWANA. MIMI NIMEBAHATIKA KUKISOMA KITABU HICHO, MLE NDANI NI CHUKI DHIDI YA UKATOLIKI WA MKAPA NA NYERERE +++++. SI KWELI KUWA WAISALAMU WAMEKUWA OPPRESSED KIASI CHA KUWANYIMA HADHI YA UTANZANIA WAO. WATZ TUACHE UNAFIKI KWENYE MAMBO YA MSINGI WA NCHI YETU.
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Nov 13, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  FDR Jr.
  Lakini kubali kuwa Mkapa ametuangusha wengi tuliokuwa na matumani naye.
  Yeye na mkewe hawana tofauti na Mwinyi na Mama Sitti. He could and should have done better.
   
 15. a

  andreakalima JF-Expert Member

  #15
  Apr 28, 2016
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 2,917
  Likes Received: 1,813
  Trophy Points: 280
  safar hii lazima Tanzania tuibuke kidedea
   
Loading...