Kwanza niwapongeze wale wote walioamua kuwa uchunguzi ufanywe ili kubaini wizi wa mitihani uliotokea kwa watahiniwa wa utabibu. Naamini hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika kwani imekuwa kawaida yao kufanya kitendo hiki kwa muda mrefu.
Pamoja na hayo yote, naomba kuuliza, je kwa nini upande wa uuguzi hakuna uchunguzi wowote unaofanyika wakati mitihani yao ilivuja vile vile kama ya utabibu?
Nashauri udhibiti uwe mkubwa kwani hii si mara ya kwanza na imekuwa mazoea hasa kwa kada ya utabibu, ambapo karibu kila mwaka mitihani inavuja na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa.