Kwanini mitaa ambamo kuna Balozi za nchi tano zenye nguvu duniani isiitwe majina ya vivutio vya utalii vya Tanzania?

Mkuu mbona hata huko ulaya kuna mitaa na sehemu zinazotumia majina yetu maarufu ya huku kwetu, kuna Dar es salaam huko ujerumani, Zanzibar na zaidi. Sioni kama kuna shida hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo shida ipo kaka mkubwa. Mimi sijafika ulaya ila kwa namna ninavyowafahamu wazungu, hiyo mitaa yenye majina ya yetu kama Dar Es Salaam na Zanzibar haipo prime areas kama hapa kwetu. Hiyo mitaa itakuwa ipo sehemu za walala hoi wa huko German.

Ila hapa kwenye sehemu sensitive na prime kama mitaa ya balozi ya nchi zenye nguvu duniani ndio tunapaita Hamburg badala ya Serengeti, Manyara au Mikumi
 
Vipi kuhusu barabara na mitaa lukuki hapa TZ yenye majina kma Mandela, Sam Nujoma, Samora, Mwaki Kibaki, Obama Drive etc tunaifanyaje hii mana sio majina ya tanzania??

Hoja ya kutangaza nchi ni ya msingi ila kubadili majina ya mitaa kufikia hilo ni hoja hafifu na ya kibaguzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haisaidii chochote,tuache kupoteza muda kwa petty issues.
Nadhani mtoa hoja hakumaanisha majina kama mbuzi, kobe nk bali alimaanisha majina yanayohifadhi vivutio vyetu kama vile serengeti, mikumi, kilimanjaro nk. Kwamba kama mtaa wa balozi zetu ukiitwa kilimanjaro au serengeti kwa kiasi fulani inaweza saidia katika kutangaza maeneo yetu ya utalii hata kama ni kwa kiasi kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utalii hauendi hivyo kijana.

Hata nchi nzima mkabadili majina yenu mkajiita Swala, Simba, Chui haitaongeza utalii kama mnavyofikiria.

Kujua pull factors za utalii ila majina hayaleti mabadiliko yeyote.

Mwaka 2017, Spain ilitembelewa na watalii milioni 58. Wakatumia jumla ya $68billion.

Unadhani hao wote walifuata majina ya Simba, sijui Swala au Konokono?

Majiji makubwa duniani kama Paris, Hongkong, Beijing, Moscow, Berlin, Milan, Venice wanatembelewa na mamilioni ya watalii, sio kwasababu ya majina ya mitaa, ila kwasababu wamepata sababu ya kuwavuta waende pale kila siku.

Kubadili jina la mtaa kutoka Hamburg kwenda Swala sijui Kobe hakutaleta mtalii hata mmoja.

Unaongelea vipi Ikulu kuwepo Barack Obama Road? Au barabara za Mandela au Sam Nujoma au Mwai Kibaki?

Nako si tubadilishe kuitwe Pundamilia, sijui Mbuzi au Kifaru? Ili kuvutie watalii?

Vipi mitaa iliyo nje ya Tanzania yenye majina ya vitu au miji ya Tanzania. South africa na UK kuna mtaa wa Nyerere. Germany wana mtaa unaitwa Dar es Salaam n.k

Unadhani kuna watalii wapo Chicago watawaza kuja Dar kuangalia mtaa unaoitwa Swala au Kondoo?

Utalii ni zaidi ya majina.

Na pia kuna utofauti kati ya uzalendo na umasikini aka ushamba. Masikini na Washamba ndo wazalendo, wajanja wanaonekana sio wazalendo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakika umenichekesha sanaaaaaa
Eti mitaa tuite Mbuzi, Kondoo, Chura, Kenge, Kobe n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (last born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Kwanini mitaa ambamo kuna Balozi za nchi tano zenye nguvu zaidi duniani (Five Permanent UN Security Council Members with Veto powers - France, United States, UK, Russia, China) isiitwe majina ya vivutio vya utalii vya Tanzania? au;

Kwanini mitaa ambamo kuna Balozi za nchi ambazo watalii wengi wanatokea isiitwe majina ya vivutio vya utalii vya Tanzania?

Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba jana wakati ninapitia makala kadhaa katika internet ninakumbana na picha ya ofisi za Ubalozi wa Uingereza zilizopo Dar Es Salaam Tanzania eti zipo mtaa wa "HAMBURG". What the hell is HAMBURG? Are we Germans? Hapana. Sisi sio wajerumani. Sisi ni watanzania tuna majina yetu ya asili kutoka katika kila kabila. Kama mitaa mnaiita Hamburg mara Ohio basi uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere nao uitwe J.F.K International Airport au Frankfurt Am Main. Please Tazama picha hapo chini kwanza. Tunasikitisha kwa kweli.

View attachment 1336870

Baada ya kifo cha mwanahabari mwenye uraia wa Saudi Arabia ndugu Jamal Khashoggi, shirika la kimataifa la kutetea haki ya binadamu la Amnesty International lilizindua campaign ya kuhamasisha nchi zote duniani kubadili majina ya mitaa ambamo kuna balozi za Saudi Arabia na kuita mitaa hiyo Khashoggi Street ili kutengeneza kumbukizi ya kila wakati ya mauaji ya mwanahabari huyo kwa watumishi wa balozi za nchi hiyo dunia nzima. Yaani kila akiingia kazini na kutoka anakutana na bango la Khashoggi Street na hii mpaka kwenu address ya documents za ofisi anakutana na jina la bwana Khashoggi

Tazama picha hapo chini;

View attachment 1336872
Amnesty International today renamed the street outside the Saudi Arabian embassy in central London as “Khashoggi Street” to mark a month since the Saudi journalist Jamal Khashoggi was murdered in the Saudi consulate building in Turkey.

Sasa kama Amnesty International shirika linalofadhiliwa na serikali ya Uingereza limeona ni bora wakatengua jina la mtaa uliokuwa unaitwa let's say Saint James huko London na kuamua kupachika jina la raia wa Saudi Arabia (Jamal Khashoggi) jambo ambali lina manufaa kwao katika kusukuma agenda yao ya utetezi wa haki za binadamu, kwanini sisi tuendelee kung'ang'ania majina ya miji ya Ulaya kama hayo akina "Hamburg Street" pamoja na "Ohio Street"

Kwanini na sisi watanzania tusiwe na majina yetu ya hapa hapa nyumbani (ninapendekeza majina ya vivutio vya utalii) ili tusukume vema agenda yetu ya uzalendo?

Mimi bado sijafika ulaya na Amerika ila kwa namna ninavyowafahamu wazungu, hiyo mitaa yenye majina yetu kama Dar Es Salaam na Zanzibar haipo prime areas kama hapa kwetu Hamburg na Ohio Avenues tulivyoziweka sehemu nyeti.

Hiyo mitaa itakuwa ipo sehemu za walala hoi wa huko German na Ulaya.

Ila hapa kwenye sehemu sensitive na prime kama mitaa ya balozi ya nchi zenye nguvu duniani ndio tunapaita Hamburg badala ya Serengeti, Manyara au Mikumi.

Simaanishi kuwa tunapaswa kubadili majina ya mitaa ya balozi zote za nchi za ulaya na marekani, hapana, ila tunaweza kubadili majina ya mitaa ambamo kuna ofisi za balozi ambazo nchi zao zinatuletea watalii wengi zaidi tupunguze huu uzungu uzungu mwingi ambao hauna tija yoyote kwa manufaa ya taifa.

OUR MOTTO: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Sounds good!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna push and pull factors za kuboresha ongezeko la watalii eneo husika, kwanza miundo mbinu namaanisha hoteli,usafiri hali ya barabara n.k ,pia utengamano wa kisiasa (amani) , na ukarimu wa watu sio watalii wanakuja wanaporwa, wanabakwa ,wanatapeliwa.
Hamna uhusiano wa moja kwa moja kati ya utalii na jina la sehemu
Ndugu infant Soldier kabla ya kutoa mawazo yako soma kwanza upate ufahamu zaidi (fanya literature review)
 
Back
Top Bottom