Kwanini michezo ya mapigano ni marufuku Zanzibar?

lwambof07

JF-Expert Member
Jul 12, 2016
4,593
5,202
Omar Mkambara
BBC Swahili

Mchezo wa masumbwi ama ndondi ni moja kati ya michezo mashuhuri na pendwa duniani kote na ukiwapa umaarufu na utajiri wa mabondia na watu walio katika sekta hiyo.

Licha ya ukubwa na umaarufu wa mchezo huu lakini katika visiwa vya Zanzibar ni marufuku mchezo wa ndondi kuchezwa pamoja aina nyingine za sanaa za mapigano.

Katazo la mabondia kutokupiga lilianza mwishoni mwa miaka ya 60, baada ya mapinduzi na aliyetoa agizo la kutokupigana alikuwa ni rais wa kwanza wa Taifa hilo Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Je zipi zilikuwa sababu masumbwi na michezo ya kufanana nayo kupigwa marufuku?
Amiri Mohamed Makame ni kamishina wa idara ya michezo Visiwani Zanzibar anasema sababu za ambazo zilimfanya Rais Karume, kukazata mchezo huu kuwa kupigana sio tabia za kibinadamu ni tabia za wanyama na kidini sio jambo jema watu kupigana.

''Kuna kauli ya katazo iliyotolewa na marehemu Hayati Sheikh Abeid Amani Karume akisema michezo ya ngumi isichezwe visiwani humo kwa kuwa kupigana ni tabia za wanyama na sio utu kwa watu kupigana na hata kidini sio sawa''. Amiri Mohamed Makame aliiambia BBC.

Kauli ya katazo iliyotolewa na raisi Karume haikuwa sheria lakini kamishina wa michezo idara ya michezo anasema '' Kauli ya kiongozi na kauli ya rais ni agizo hiyo alivyotoa kauli ile watu wengi walisikia na wakafuata agizo lake''

Mabondia wanamichezo wengine wanacheza michezo ya sanaa za mapigano wanaruhusiwa kufanya kufanya mazoezi tu katika visiwa hivyo na sio kupigana mapambanio rasmi ikiwa bondia anataka kupigana anatakiwa kutoka nje ya visiwa hivyo.

Mapema mwaka uliopita serikali ya mapinduzi ya Zanzibar iliunda kamati iliyokuwa inaongozwa na kamishina wa idara ya michezo Amiri Mohamed Mohamed na jukumu la kamati hii ilikuwa kuangalia je kuna haja ya mchezo wa masubwi kuruhusiwa.

Na mwishoni mwa mwaka jana kamati ilimaliza awamu ya kwanza ya utafiti wao na kwa sasa kamati hiyo inafanya mchakato wa kupata maoni ya wazi na wananchi kama wanahitaji kuruhusiwa kwa mchezo huu na baada ya hapo serikali itatoa maamuzi yake.

Je kuna matumaini yoyote michezo hiyo kuruhusiwa?
''Sisi kama kamati tulishafanya kazi yetu ya awali lakini mwamuzi wa mwisho ni Serikali ''. Kiongozi wa kamati aliambia BBC.

Mabondia wamekuwa wakiomba Serikali ya mapinduzi kutoa ruhusa kwa mchezo huo kufanyika ili kuweza kuwapa fursa ya ajira vijana wengi ambao wana vipaji vikubwa vya mchezo ya masumbwi.

Hassan Bandani ni bondia na mwalimu wa masumbwi anasema toka ameingia katika mchezo huo amekuwa akitoka nje ya visiwa hivyo na kwenda Tanzania bara na nje ili kuweza kupigana na hata hivyo wanaendelea kufuatilia kwa serikali ili kurushusiwa kucheza mchezo wao.

''Tunafanya jitihada nyingi kuzungumza na viongozi mbalimbali hivi juzi tulienda baraza la wawakilishi kuongea nao lakini msukumo umekuwa mdogo sana tunasubiri uamuzi wa serikali kujua watafanya nini''.

Licha ya kuwepo changamoto hiyo ya kutokurusiwa kwa mapambano, Kampuni ya ZanFIT inayojihusisha na usimamizi wa mabondia pamoja na kituo cha mazoezi kwa ajili ya michezo masumbwi na sanaa za mapigano inafanya mipango ya kuwasaidia mabondia kwa kupata mapambano nje ya Visiwa vya Zanzibar.

Zanfit kwa kushirikiana na Kampuni ya moja ya michezo ya Kimarekani wameingia mkataba wa kuwasaidia mabondia kupata mapambano nje ya visiwa vya Zanzibar ambapo si ruksa kupigana

Ally Semi Ally ni bondia na mkufunzi wa michezo ya sanaa za mapigano akiongoza Kampuni ya Zanfit anasema kuwa ushirikano na kampuni hiyo ya Marekani utasaidia kuwapatia mapambano makubwa mabondia wa Zanzibar

''Kampuni hiyo iko Atlanta nchini Marekani na hivyo itatusaidia kupata mapambano lakini pia kutuletea walimu wazuri wa mchezo wa masubwi na hata katika mapigano ya UFC kwa sababu wanawapiganaji wao kule ''.Ally Semi Ally aliiambia bbc.

Ni jambo la kusubiri muda ili kuona kama baada ya miaka mingi mchezo wa masumbwi utaruhusiwa na kuwapa fursa vijana wa Visiwani Zanzibar kucheza mchezo wa ndondi ukiwa ni miongoni mwa michezo yenye mashabiki wengi duniani.
FB_IMG_1643375048756.jpg
FB_IMG_1643375115374.jpg
FB_IMG_1643375101494.jpg
 
Back
Top Bottom