EWGM's
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 1,521
- 2,109
Unapoongelea viwanda ni moja kwa moja unajikita kwenye biashara. Ili biashara ianze lazima kuwe na wazo, na wazo linawekwa kwenye maandishi au mwenye wazo anakuwa na uwezo wa kulieleza kiufanisi ni vipi wazo lake litafanikiwa. Kisha kunakuwa na mikakati mahususi ilikuweza kukamilisha wazo ikihusisha rasilimali mbali mbali (watu, fedha, malighafi, n.k.)
Moja ya rasimali ni watu na kwenye wazo la Magufuli moja moja linagusa wananchi wake. Hapo ndipo kikwazo kuwa wazo halitatimia sababu akili za waTanzania walio wengi haziko sawa. Tatizo ni msingi mbovu wa elimu ulikuwepo nchini na tamaduni au hurka chafu zilizokomaa vichwani mwa wananchi wake.
Mfano mdogo leo nimeona kwenye huu uzi hapa ambao uliletwa kuhusiana na Mh. Lema tweet; Godbless Lema: Nimempekala Mtoto Agakhan Hospital Bima (NHIF) Imekataliwa!! Kwa ustadi ukisoma maelezo ya wengi utaona kabisa vichwani waTanzania wengi hawako sawa. Na nilichojifunza wengi tumetawaliwa na “hear say” hatufanyi utafiti binafsi na kujiridhisha kuwa hichi ninachosikia au kukisema ni sawa au si sahihi. Tunakurupuka tu maneno meengi ya khanga na cha kushangaza wengi hawajui wanachokisema au kukiandika.
Hivyo Mheshimiwa Rais, ukiachilia mbali kuwa hatujaona mpango wa maandishi na hata ule wa meneno bado unamikanganyiko mingi tu. Ila kikwazo kikubwa kitakuwa waTanzania ambao unawategemea kama rasilimali watakuangusha vibaya sababu vichwani hawajawekeza vya kutosha kuweza kukusaidia kutimiza lengo lako.
Nakuomba badili gia angani kama inawezekana badili wazo na wekeza kwenye vichwa vyao kwanza ili nchi miaka 15 ijayo iweze kujisamia yenyewe ila kwa sasa unatwanga maji kwenye kinu. Au ukubali kufungua milango ya mipaka ya nchi na uruhusu majirani zetu waje kutusaidia kutimiza lengo lako lakini si hawa vijana walio mtaani, bure kabisa.