Kwanini Mh. Rais Hutafanikiwa Kwenye Wazo la Nchi ya Viwanda

EWGM's

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
1,521
2,109
Unapoongelea viwanda ni moja kwa moja unajikita kwenye biashara. Ili biashara ianze lazima kuwe na wazo, na wazo linawekwa kwenye maandishi au mwenye wazo anakuwa na uwezo wa kulieleza kiufanisi ni vipi wazo lake litafanikiwa. Kisha kunakuwa na mikakati mahususi ilikuweza kukamilisha wazo ikihusisha rasilimali mbali mbali (watu, fedha, malighafi, n.k.)

Moja ya rasimali ni watu na kwenye wazo la Magufuli moja moja linagusa wananchi wake. Hapo ndipo kikwazo kuwa wazo halitatimia sababu akili za waTanzania walio wengi haziko sawa. Tatizo ni msingi mbovu wa elimu ulikuwepo nchini na tamaduni au hurka chafu zilizokomaa vichwani mwa wananchi wake.

Mfano mdogo leo nimeona kwenye huu uzi hapa ambao uliletwa kuhusiana na Mh. Lema tweet; Godbless Lema: Nimempekala Mtoto Agakhan Hospital Bima (NHIF) Imekataliwa!! Kwa ustadi ukisoma maelezo ya wengi utaona kabisa vichwani waTanzania wengi hawako sawa. Na nilichojifunza wengi tumetawaliwa na “hear say” hatufanyi utafiti binafsi na kujiridhisha kuwa hichi ninachosikia au kukisema ni sawa au si sahihi. Tunakurupuka tu maneno meengi ya khanga na cha kushangaza wengi hawajui wanachokisema au kukiandika.

Hivyo Mheshimiwa Rais, ukiachilia mbali kuwa hatujaona mpango wa maandishi na hata ule wa meneno bado unamikanganyiko mingi tu. Ila kikwazo kikubwa kitakuwa waTanzania ambao unawategemea kama rasilimali watakuangusha vibaya sababu vichwani hawajawekeza vya kutosha kuweza kukusaidia kutimiza lengo lako.

Nakuomba badili gia angani kama inawezekana badili wazo na wekeza kwenye vichwa vyao kwanza ili nchi miaka 15 ijayo iweze kujisamia yenyewe ila kwa sasa unatwanga maji kwenye kinu. Au ukubali kufungua milango ya mipaka ya nchi na uruhusu majirani zetu waje kutusaidia kutimiza lengo lako lakini si hawa vijana walio mtaani, bure kabisa.

 
Kilimo kwanza ingefanikiwa ingerahisisha ujenzi wa viwanda hata hivyo viwanda vitapatikana kwa nguvu zote
 
Kilimo kwanza ingefanikiwa ingerahisisha ujenzi wa viwanda hata hivyo viwanda vitapatikana kwa nguvu zote


Lilikuwa wazo zuri sana na likuwa linaendana na mfumo wa nchi. Zaidi ya asilimia 72 ya waTanzania ni wakulima, moja ya tatu ya nchi ni pori tu ilikuwa safi kabisa
 
Ili kuendelea:-
1. Yafaa vinapoongelewa viwanda serikali ijielekeze zaidi kwenye sera zinazosaidia uwekezaji binafsi, na hayo ndiyo nategemea kuyasikia toka kwa wenye mamlaka.
2. Ijulikane katika jamii maendeleo si viwanda peke yake, kuna mengine mengi pia. Hayo pia yanahitaji kuwekewa mazingira ya kuyaendeleza
 
mimi ningekuwa magu ningeanza na research ya viwanda vya zamani vilivokufa kujua nini kiliua kama ni management, vilipitwa na wakati au ni issue ya quality. u never know with introduction of new technology and quality improvement things might turn around. I lost hope with jpm anataka kuendesha kwa akili yake binafsi hakuna nchi kama hiyo duniani
 
'''Cowords dies many times before their death''' Achebe chinwa alisema. Uoga wa nini viwanda vipo mkuu na vitaendelea kuongezeka. Rais JPM anafanya vizur kabisa kaamua kuanza na miundimbinu kwanza na baadae viwanda sasa kama mvua. Cheki anataka uwepo umeme wakutosha, je unaweza kuendesha viwanda bila umeme? Barabara, viwanda bila barabara ndugu inawezekana? , na bado mwanao anamsomesha bure ili afikie malengo ama '''ELIMU UNAYOTAKA YA AINA GAN'' ¶¶¶Make kumbuka mchicha ulianza kama mbuyu¶¶¶¶ na hakuna mti ukuao bila ushilikiano wa viungo vyake. Wewe kama wewe pia wa weza kuwa mchango mkubwa sana kwenye hili.
LAKIN CHA KUFANYA NI KWAMBA UUNGANA NAE ILI MTI IMALA UKUE.
 
'''Cowords dies many times before their death''' Achebe chinwa alisema. Uoga wa nini viwanda vipo mkuu na vitaendelea kuongezeka. Rais JPM anafanya vizur kabisa kaamua kuanza na miundimbinu kwanza na baadae viwanda sasa kama mvua. Cheki anataka uwepo umeme wakutosha, je unaweza kuendesha viwanda bila umeme? Barabara, viwanda bila barabara ndugu inawezekana? , na bado mwanao anamsomesha bure ili afikie malengo ama '''ELIMU UNAYOTAKA YA AINA GAN'' ¶¶¶Make kumbuka mchicha ulianza kama mbuyu¶¶¶¶ na hakuna mti ukuao bila ushilikiano wa viungo vyake. Wewe kama wewe pia wa weza kuwa mchango mkubwa sana kwenye hili.
LAKIN CHA KUFANYA NI KWAMBA UUNGANA NAE ILI MTI IMALA UKUE.


Una mengi ya kujifunza na si kudandia treni tu, ulivyovitaja vyote vinajiendesha vyenyewe tu??

Hivi ndizo akili JPM angewekeza kwanza zikae sawa kwenye kufikiri kabla ya kufanya jambo/kuongea
 
EWGM's

Katikakampeni yake ya urais, Magufuli alijitapa kwamba hakupokea hata senti ya mchango wa wafanyabiashara kwenye mfuko wa kampeni. Huu ulikuwa uongo, kitu kibaya kwa kiongozi, lakini hoja yangu si kwamba kasema uongo .

Hoja yangu ni kwamba, Magufuli ndani kabisa moyoni mwake ni anti-business.Kauli hii inaonyesha mtu anayewachukulia wafanyabiashara wote kama wezi tu, hawafai kumchangia yeye mtu safi.

Kwa msimamo kamahuu, hatuwezi kujenga nchi ya viwanda, kwa sababu viwanda vinajengwa kwa kiasi kikubwa na wafanyabiashara.Na kama rais anawanyanyapaa wafanyabiashara na kuwaona wezi tu, basi hawezi kufanikiwa kutupanchi ya viwanda.

Tutabakisha maigizo tu.
 
Kuna ukweli fulani mkuu vijana chenga nyiiingii, hawako serious na maisha, hata hawa wanaojitahidi kuwekeza wanakutana na changamoto za manpower

Aiseee km unaroho nyepesi waweza sitisha uwekezaji siku hiyohiyo.
 
Back
Top Bottom