#COVID19 Kwanini mganga wa Hospitali Mwananyamala alimwingiza Rais chumba cha wenye Covid-19 bila kumfahamisha kabla?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,307
12,602
Corona ni ugonjwa hatari wa kuambukiza kwa njia ya hewa, Rais alitakiwa kufahamishwa kuwa sasa anaingia wodi ya wagonjwa wenye corona ili ajiandae kimwili na kiakili, pia ahiari mwenyewe kuingia au kutoingia wodi ile.

Rais ameonekana hadharani kushitushwa kwa kujikuta katikati ya wagonjwa wa corona kiasi cha kushindwa kuzuia kuonyesha hamaki na wasiwasi yake.

Kwani madhumuni ya kumpeleka mama kimyakimya kwenye wodi ile yakulikuwa ni nini?

Je, ni kwakuwa alivaa barakoa?
Je, nikumuonyesha kuwa kuna wagonjwa wa corona?
Je, njia ya kumwambia mkuu kuwa wahudumu wanahitaji vifaatiba na vya kujinga na corona
Je, kumwambia mkuu wanafanyakazi za hatari kuliko watu wengine kama walimu?
Je, ni kuangalia wajonjwa wote bila kubagua magonjwa
Au ni nini hasa kile?

Pia soma > Mwananyamala: Rais Samia ala kona baada ya kuambiwa wodi anayotaka kuingia ni ya wagojwa wenye matatizo ya kupumua
 
Ile ilikua plani ya kuja kupata namna ya kusema Kuna wagonjwa 100 wa korona
Kuna hospitali 3 ndani katika kipindi cha wiki kuna wagonjwa 24. Mbili za private moja ya rufaa ya Mkoa. Zote ziko Dar. Hizo hospitali 3 Dar nzima. Sasa wewe mwenye utaangalia kama hiyo 100 haiwezekani na utakuta kuna zaidi
 
Ile ilikua plani ya kuja kupata namna ya kusema Kuna wagonjwa 100 wa korona
Exactly. Na mleta mada ame frame wrong question to wrong person, hilo swali lilipaswa kuelekezwa kwenye security detail ya Rais-Lakini kwa sababu limefanyika intentionally-Hakuna hatua yoyote yaweza fanyika.
 
Na wale macameramen waliotangulia ndani kabisa?Unawafikiriaje?
... kujiandaa ku-shoot lile igizo! Haiwezekani Rais mwenye kila aina ya taarifa kiganjani na kila aina ya ulinzi, unaoonekana na usioonekana, unaojulikana na usiojulikana, akashtukizwe kuingizwa wodi ya wagonjwa wa Corona Mwananyamala Hospital.

Kwanza, kabla ya Rais kupita, hours before, kuna wale "wasafisha njia" hupita na kila aina ya zana including mbwa wenye mafunzo level ya CIA kusafisha njia eti wasijue ni wodi ipi wamelazwa wagonjwa wa Corona! Huyo daktari mwenyewe aliyekuwa anatoa maelezo most likely ni TISS!
 
Lile tukio halikupaswa kutokea kabisa coz wagonjwa wa Covid-19 wanatakuwa kua chini ya quarantine.
 
Au ilipangwa ili kuonyesha kuna wagonjwa wengi wa korona (Urais ni maigizo kwa mujibu wa rais wa awamu ya pili wakati akimuelezea JPM kwa amelifanyia kazi vyema igizo la urais)
 
Lile tukio halikupaswa kutokea kabisa coz wagonjwa wa Covid-19 wanatakuwa kua chini ya quarantine.
Mungu kafanya litokee lilivyi tokea ili kuwapelekee ujumbe watu flani kwamba hawawezi shindana na huyu Mungu wa Mbinguni, watashindwa tu pale wanapotaka kuonesha kumtegemea Mungu ikikuwa ni makosa sasa Tumeamua kuenda na dunia inavyo enda.
 
Ulitaka nani aingizwe pale?
Hee, kwani wote wanaoingia pale wote huwa wanahamaki kama vile? Kuhamaki huwa kunashusha kinga ya mwili na kupunguza uwezo wa kijilinda dhidi ya maambukizi
 
Back
Top Bottom