Kwanini mfumo wa kupokezana madaraka kati ya wakristo na waislamu Africa mashariki upo Tanzania tu?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,810
Katika nchi za Africa Mashariki, Tanzania ndio taifa pekee ambalo kuna mfumo wa kuachiana madaraka kati ya mkristo na muislamu. Yaani akitawala mkristo miaka kumi na miaka kumi muislamu, nimeupenda huu mfumo wa kupokezana madaraka.

Lakini inakuwaje ngumu kwa majirani zetu kushidwa kuachiana madaraka ya urais?

Ukiangalia nchi kama vile

1. Uganda kwa Yoweri Museveni

2. Kenya kwa Uhuru Kenyatta

3. Rwanda kwa Paul Kagame

4. Burundi kwa Pierre Nkuruzinza

5. Sudan Kusini kwa Salva Kirri

6. DRC kwa Joseph Kabila

Je ni kwanini inakuwa ngumu kuachiana madaraka katika nchi hizi? Nakumbuka Uganda mara ya mwisho kutawala Muislamu ilikuwa kipindi cha Iddi amin Dada
 
Ni kwa sababu ni Tanzania tu ndipo idadi ya wananchi wake imegawanyika karibu sawa kati ya Wakristo na Waislam.

Hizo nchi zingine ulizozitaja ni majority Christian nations. Ni sawa sawa na ushangae kwanin Mkristo hajawahi kuwa Rais Zanzibar.

Japo Tanzania hakuna mfumo rasmi juu ya hilo,kuna nchi zingine kama Lebanon hiyo ipo kwenye katiba kutokana na idadi inayokaribiana kati ya dini hizi mbili.Lebanon ndio nchi pekee ya Kiarabu ambayo kwa mujibu wa katiba Rais anapaswa awe Mkristo.
 
Katika nchi za africa mashariki tanzania ndio taifa pekee ambalo kuna mfumo wa kuachiana madaraka kati ya mkristo na muisalamu...... ...

Yaani akitawala mkristo miaka kumi na miaka kumi muisalamu nimeupenda huu mfumo wa kupokezana madaraka... ....

Lakini inakuwaje ngumu kwa majirani zetu kushidwa kuachiana madaraka ya uraisi ukiangalia.

Ukiangalia nchi kama vile

1.uganda kwa yoweri museveni

2.kenya kwa uhuru kenyata

3.rwanda kwa paul kagame

4.burundi kwa piere nkurunzinza

5.sudan kusini kwa salva kirri

6.joseph kabila wa congo

Je ni kwanini inakuwa ngumu kuachiana madaraka katika nchi hizi nakumbuka uganda mara ya mwisho kutawala muisilamu ilikuwa kipindi cha iddi amini dada
Ndiyo hapo unapaswa kuamini kuwa Tz ndiyo mkombozi wa bara la Afrika, na babalao wa Demokrasolia.
 
Ni kwa sababu ni Tanzania tu ndipo idadi ya wananchi wake imegawanyika karibu sawa kati ya Wakristo na Waislam.

Hizo nchi zingine ulizozitaja ni majority Christian nations. Ni sawa sawa na ushangae kwanin Mkristo hajawahi kuwa Rais Zanzibar.

Japo Tanzania hakuna mfumo rasmi juu ya hilo,kuna nchi zingine kama Lebanon hiyo ipo kwenye katiba kutokana na idadi inayokaribiana kati ya dini hizi mbili.Lebanon ndio nchi pekee ya Kiarabu ambayo kwa mujibu wa katiba Rais anapaswa awe Mkristo.
Lebanon sio waarabu
 
Katika nchi za africa mashariki tanzania ndio taifa pekee ambalo kuna mfumo wa kuachiana madaraka kati ya mkristo na muisalamu...... ...

Yaani akitawala mkristo miaka kumi na miaka kumi muisalamu nimeupenda huu mfumo wa kupokezana madaraka... ....

Lakini inakuwaje ngumu kwa majirani zetu kushidwa kuachiana madaraka ya uraisi ukiangalia.

Ukiangalia nchi kama vile

1.uganda kwa yoweri museveni

2.kenya kwa uhuru kenyata

3.rwanda kwa paul kagame

4.burundi kwa piere nkurunzinza

5.sudan kusini kwa salva kirri

6.joseph kabila wa congo

Je ni kwanini inakuwa ngumu kuachiana madaraka katika nchi hizi nakumbuka uganda mara ya mwisho kutawala muisilamu ilikuwa kipindi cha iddi amini dada
Kati ya Iddi Amini na Yussuph Lule nani alikua wa mwisho?
 
Aloo, hebu kasome katiba halafu utuambie kama kuna mahali limetajwa hilo la kupokezana watu wa dini hizo mbili. Vinginevyo we we ni mchochezi.
 
Kwa mujibu wa katiba yetu, hakuna kipengele kinachoongelea utaratibu huo
 
Nchi zetu za Africa Mashariki mifumo yetu ya democracy bado imejaa kasoro nyingi sana. Na hii ni kwa sababu watawala kutumia vyombo vya dola kukandamiza sauti za wananchi.

Hapa kwetu CCM wako radhi wapokezane madaraka wao kwa wao lakini si na wengine eg Zanzibar. Sasa hapo uhalali na kujisifu kunatoka wapi??!! . Kenya wana tatizo la ukabila ktk kupokezana madaraka nalo si la kujivunia, Uganda kuna ufalme wa mtu unaotokana na bunduki nalo si la kujivunia hata kidogo . Rwanda, South Sudan & Burundi tatizo ni kama Kenya ukabila
 
Wenyewe wanajiita Phonecian, sijui ndio watu gani. Ingia google ujisomee

Tukiingia kwenye hiyo debate hatutafika.

Kufupisha maneno itoshe kusema kuwa tunaposema dunia ya Kiarabu basi Lebanon ni nchi moja wapo, kuthibitisha hilo Lebanon ni mwanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Arab League.

Hivyo sijakosea kusema ni nchi pekee ya Kiarabu ambayo kwa mujibu wa katiba Rais ni lazima awe Mkristo.
 
Nchini Lebanon kuna:
1. Waislam wa Madhehebu ya Kishia 27%,
2. Waislam wa Madhehebu ya Kisunni 27%,
Haya makundi mawili ya Kiislam hayakai zizi moja, ni maadui wakubwa, na kuna
3. Wakristo kwa ujumla wao 40%.

Hata iyo 40% ya wakristo ni madhehebu tofauti wasio endana Kwa lolote
 
Back
Top Bottom