Kwanini Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) haiwatambui wala kuwapa tuzo wanachama wake wanaokaa miaka mingi pasipo kuugua?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
14,777
2,000
Shikamooni wakubwa zangu wote wa humu jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Eti, Kwanini Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) hawatoi tuzo kwa wanachama wanaokaa miaka mingi pasipo kuugua ili iwe motisha kwa wengine kuzidi kuzingatia kanuni za afya hivyo kukaa muda mrefu bila kuugua jambo litakaloiwezesha NHIF kupunguza kiwango cha fedha inacholipa kila mwezi kwenye vituo vya afya.

Kuna jamaa yangu ninakaa naye huku mtaani ni mtumishi wa kampuni moja ya mawasiliano ya simu pia ni mwanachama wa NHIF, anasema huu ni mwaka wa sita sasa hawajahi hata kumeza tu Paracetamol achilia mbali kuumwa malari. Kuna baadhi ya watu wanaumwa magonjwa sababu ya kutozingatia kanuni za msingi afya.

Watu kama hawa wanapaswa kupewa special recognition na NHIF ili wawe ni mfano wa kuigwa na wanachama wengine.

NHIF wanavyo vitega uchumi chungu nzima nimefanya nao kazi field attachment hivyo ninawajua vema.

Pesa za wanachama zinazungushwa hivyo wanapata sana faida

OUR MOTTO: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,190
2,000
Shikamooni wakubwa zangu wote wa humu jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Eti, Kwanini Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) hawatoi tuzo kwa wanachama wanaokaa miaka mingi pasipo kuugua ili iwe motisha kwa wengine kuzidi kuzingatia kanuni za afya hivyo kukaa muda mrefu bila kuugua jambo litakaloiwezesha NHIF kupunguza kiwango cha fedha inacholipa kila mwezi kwenye vituo vya afya.

Kuna jamaa yangu ninakaa naye huku mtaani ni mtumishi wa kampuni moja ya mawasiliano ya simu, anasema huu ni mwaka wa sita sasa hawajahi hata kumeza tu Paracetamol achilia mbali kuumwa malari.

OMBI: NSSF nipeni pesa zangu mtaani maisha ni magumu sana.

MKIFA TUTAWAKUMBUKA SAWA EEH
 
mnengene

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
2,330
2,000
Ndio mfumo wa bima ulivyo dunia nzima. hela zake wanatibiwa wengine , unaweza kuta mtu kachangia miezi 2 tu Ila kaumwa NHIF wanamgharamia matibabu Milioni 20. Hata yeye anaweza kuumwa na kugharamiwa zaidi ya michango yake aliyochangia .

Mfano magonjwa ya kansa .
Kuna mtu namjua Mungu amuweke mahala pema peponi kwani ameshafariki.
Huyu Jamaa alikuwa na kansa alitibiwa akaletewa bili ya Million 45 NHIF ndio waliomlipia.

Yeye michango yake kwa kipindi chote Cha zaidi ya miaka 10 hayafikii kiasi hicho.
Mkuu bima ndio ilivyo, unaweza pata ambacho hujapanda na unaweza usivune chochote kwa ulichopanda.

Mwisho wa siku Ni bora usivune chochote pale ulipopanda linapokuja suala la bima hususani bima ya afya.
Hakuna mtu atakayetaka kuumwa ili eti akatibiwe na bima yake.
Kwenye magari angalau Kuna watu wanafanyafanya ujanja kupata fidia ya bima kwa kuangusha au kuyachoma Moto magari yao maksudi
 
mnengene

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
2,330
2,000
Mkuu, una maanisha kwenye bima ya afya hakuna fraud cases za watu ku-fake magonjwa???
kwenye Bima ya afya mtu mwenyewe sio rahisi kwani hela zinalipwa kwa hospitali iliyotoa huduma,ila nimesikia tetesi kwamba kuna baadhi ya hospitali zinafanya fraud za kuhusu wagonja waliotibiwa kwa bima ya afya ili hiyo hospitali ijipatie malipo ya kwa njia ya udanganyifu kutoka NHIF
 
BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,190
2,000
Shikamooni wakubwa zangu wote wa humu jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Eti, Kwanini Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) hawatoi tuzo kwa wanachama wanaokaa miaka mingi pasipo kuugua ili iwe motisha kwa wengine kuzidi kuzingatia kanuni za afya hivyo kukaa muda mrefu bila kuugua jambo litakaloiwezesha NHIF kupunguza kiwango cha fedha inacholipa kila mwezi kwenye vituo vya afya.

Kuna jamaa yangu ninakaa naye huku mtaani ni mtumishi wa kampuni moja ya mawasiliano ya simu, anasema huu ni mwaka wa sita sasa hawajahi hata kumeza tu Paracetamol achilia mbali kuumwa malari.

Watu kama hawa wanapaswa kupewa special recognition na NHIF ili wawe ni mfano wa kuigwa na wanachama wengine.

OUR MOTTO: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

OMBI: NSSF nipeni pesa zangu mtaani maisha ni magumu sana.
USHAWAHI SIKIA WOSIA MTU AKIWA HAII....
 
mnengene

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
2,330
2,000
Kuna baadhi ya watu wanaumwa magonjwa sababu ya kutozingatia kanuni za msingi afya.
Ni ngumu sana kuthibitisha hilo mkuu, ukichukulia maisha ya nchi zetu hizi za dunia ya tatu,.kuna watu wanapata kansa from no where yaani hajui amaepataje unaweza ukala chakula kipo contaminated unapata kansa hadi inakuja kudevelop huwezi kujua ulipataje,
au maleria wanasema tutumie neti wakati tunapolala kuepuka kuumwa na mbu wanaoambukiza maleria, wakati unaweza kungatwa na mbu wakati upo nje unapunga zako upepo.
Hilo suala ni gumu sana kuthibitisha .
Unaweza kupata ajali ya gari kutokana na udhembe wako lakini bima ya afya hawangali hilo wanakulipia matibabu tu, NHIF hawawezi kusema embu kalete traffic report ya ajali yako ndio tulipie haya matibabu uliyoyapata kutokana na kuumia kwenye ajali, hakuna kitu kama hicho
 
Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
14,777
2,000
Ndio mfumo wa bima ulivyo dunia nzima. hela zake wanatibiwa wengine , unaweza kuta mtu kachangia miezi 2 tu Ila kaumwa NHIF wanamgharamia matibabu Milioni 20.
NHIF wanavyo vitega uchumi chungu nzima nimefanya nao kazi field attachment hivyo ninawajua vema.

Pesa za wanachama zinazungushwa hivyo wanapata sana faida
 
mnengene

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
2,330
2,000
NHIF wanavyo vitega uchumi chungu nzima nimefanya nao kazi field attachment hivyo ninawajua vema.

Pesa za wanachama zinazungushwa hivyo wanapata sana faida
nafahamu wanafanya uwekezaji kupitia michango wanayokusanya, ila hata hivyo NHIF ni mfuko mchanga sana uwekezaji wake bado ni mdogo sana , ado wanasafari ndefu ili kweli wawe vizuri
 
maramojatu

JF-Expert Member
Mar 16, 2012
207
225
Ni ngumu sana kuthibitisha hilo mkuu, ukichukulia maisha ya nchi zetu hizi za dunia ya tatu,.kuna watu wanapata kansa from no where yaani hajui amaepataje unaweza ukala chakula kipo contaminated unapata kansa hadi inakuja kudevelop huwezi kujua ulipataje,
au maleria wanasema tutumie neti wakati tunapolala kuepuka kuumwa na mbu wanaoambukiza maleria, wakati unaweza kungatwa na mbu wakati upo nje unapunga zako upepo.
Hilo suala ni gumu sana kuthibitisha .
Unaweza kupata ajali ya gari kutokana na udhembe wako lakini bima ya afya hawangali hilo wanakulipia matibabu tu, NHIF hawawezi kusema embu kalete traffic report ya ajali yako ndio tulipie haya matibabu uliyoyapata kutokana na kuumia kwenye ajali, hakuna kitu kama hicho
wewe ndio unadanganya watu sana. Vifo zaidi ya asilimia tisini ni uzembe. Hata hizo ajali unazosema ni uzembe mfano mwendokasi, kung'oa alama za barabarani etc. Hata kansa zinahusiana na jinsi tunavyokula, kuchafua mazingira, vyanzo vya maji etc
Kwa hiyo mtoa ana point ya maana sana
 
Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
14,777
2,000
wewe ndio unadanganya watu sana. Vifo zaidi ya asilimia tisini ni uzembe. Hata hizo ajali unazosema ni uzembe mfano mwendokasi, kung'oa alama za barabarani etc. Hata kansa zinahusiana na jinsi tunavyokula, kuchafua mazingira, vyanzo vya maji etc
Kwa hiyo mtoa ana point ya maana sana
Umenisaidia sana kaka. Be blessed.
 
mnengene

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
2,330
2,000
wewe ndio unadanganya watu sana. Vifo zaidi ya asilimia tisini ni uzembe. Hata hizo ajali unazosema ni uzembe mfano mwendokasi, kung'oa alama za barabarani etc. Hata kansa zinahusiana na jinsi tunavyokula, kuchafua mazingira, vyanzo vya maji etc
Kwa hiyo mtoa ana point ya maana sana
nadhani umekurupuka mkuu.
Ungesoma tokea posti ya kwanza ya mtoa mada,
Hadi nilipokuja kutoa maelezo hayo usingeandika huu upuudhi ulioandika.
Ngoja nikukumbushe.
Mada kuu ilikuwa pesa za wanaochangia bima ya afya kama mtu hajaumwa kwanini asirudishiwe pesa yake au sehemu ya pesa yake? hiiyo ndio ilikuwa hoja ya kwanza mimi nikachangia kwenye thread namba 9.
Muanzisha thread akaulizwa swali kwenye post namba 10 kwamba watu hawawezi kudanganya?
Nikachangia kwenye post namba 11 kwamba kwenye bima ya afya wanaolipwa ni hospitali na sio indivuduals so mtu kama mtu kufoji sio rahisi labda hospitali.
Ndio mtoa post akaja na hoja kwamba kuna watu wanapatwa magonjwa kutokana na udhembe wao.
Mimi nikachangia kwamba kwenye bima ya afya hata ukipata ugonjwa kwa uzembe wanakutibu mradi wewe ni mwanachama na ndio nikatoa mfano kwamba unaweza ukasababisha ajali kutokana na udhembe wako na ukaumia.
Pamoja na kwamba ile ajali ulisababisha wewe kutokana na udhembe wako lakini kwa kuwa umeumia na unahitaji matibabu na una bima ya afya, Bima ya afya hawawezi kukataa kulipia matibabu yako eti kwa sababu uliumia kutokana na uzembe wako.
Sasa wewe sijui umekula maharagwe ya wapi unakurupuka kupost vitu usivyoelewa, kwa kifupi embu tuliza akili uelewe hoja zilizokuwa zinachangiwa nahisi umekurupuka uelewi hata tulichokuwa tunajadili
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom