mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,701
Siku Paulo anaitwa kuwa mpleka injili Mungu alimtambulisha kwa anania kama "CHOMBO CHANGU KITEULE NILICHOKICHAGUA ILI APATE KULICHUKUA JINA LANGU KWA MATAIFA NA WAFALME" Matendo 9:15
Pia ukisoma Isaya 49, Utagundua MTUMISHI wa Mungu ni cheo kikubwa kuliko wafalme na marais. Anasema hapo wafalme,wake zao, wenye vyeo We we ndiye utakuwa mlezi wao, Watakuja kukusujudia (kukuangukia kuomba msaada wa kiroho)
Kwanini Mungu anakata utumishi wako papo hapo unapoonyesha nia ya kuwa mwanasiasa vyama vingi.
1: Wewe ni chombo chake.ukiingia kwenye vyama vingi sio tena chombo cha Mungu Bali chombo kinachoongozwa na katiba za chama na ilani na maamuzi yao.
2: Ushawishi uliopewa ni ili watu wamjue Mungu kupitia sio wakujue wewe kupitia Mungu.
3: Vyama pinzani na hasimu vitapelekea we we ugawanye waumini kwa Misingi ya siasa badala ya kuwagawa kwa misingi ya Utakatifu na Udhambi wao ili wadhambi wasaidiwe.
4: Umepewa kondoo uwachunge, Siku ile Utaulizwa "liko wapi kundi lile nililoliweka mikononi mwako?" Utakuwa umelitapanya kwa Uccm wako au uchadema wako
5: Mungu atakukata katika teuzi zake maana sio lazima uwe tu, anao watu lukuki kwenye queue wanalilia kutumikia kwa dhamiri isiyoghoshiwa.
Mwisho wakati wa Yesu miaka 2000 iliyopita kulikuwa na harakati nyingi sana za kisiasa. Zilikuwa Kali kiasi hata wafuasi wake walimfanya na yeye kama mgombea wa kuwatoa warumi uyahudi. Zaidi ya kuwakemea Yesu hakuwahi kutoa kauli yoyote kuunga au kupinga harakati za kisiasa zaidi ya Kuwatoa watu kuangalia serikali za dunia waangalie serikali ya Mbinguni ambayo haina Wizi, Rushwa,Kujipendekeza,upendeleo, hakuna hospital, hakuna shida. Inamambo ambayo Macho hayajawahi kuona wala sikio haijawahi kusikia.
Kuacha Utumishi na kujihusisha na siasa za vyama vingi au kufanya vyote ni ushahidi kwa kuikana madhabahu takatifu na kuchagua kuwa mtumwa wa mimbari na madhabahu ziharibikazo za wanasiasa.
Usiwe mfuasi wa Mungu kupitia watu hawa maana Mungu hayuko upande wao.
Usiogope kumkemea waziwazi na kumshauri achague moja kuliko kuwa vuguvugu maana atatapikwa.