Kwanini mbunge Musukuma anapenda kuwadharau wasomi wetu?

Hajapata dawa yake ngoja atakuja kupatikana msomi mjenga hoja na asie ogopa uchawi atampukutisha.
 
Nchi hii hakuna wasomi. Msukuma yuko sahihi kabisa

Wasomi ndiyo wanapiga kelele kuilalamikia serikali juu ya ukosefu wa ajira. Tulitegemea wao ndiyo watatuzi wa tatizo hili badala yake wao ndiyo wanalikuza.

Bibi yangu maisha yake yote anaishi kwa kupambana na ametulea. Hawa wasomi uchwara hawana jipya mtaani
Sio kwamba watu hawapambani kama vile Bibi alivyopambana kukulea, watu wanapambania maslahi bora na hali bora ya maisha kuliko enzi za Bibi yako...

Maisha uliyoishi wewe na wengine wengi huenda si mazuri kihali, licha ya kwamba wajivunia Bibi kupambana lakini huenda usijivunie dhiki na shida alizopitia (kama ulipitia).

Nyakati ni tofauti na ulimwengu unakuwa kwa kasi kubwa kiasi kwamba suala la ajira ni changamoto, huu ukweli haupingiki, kazi ambazo zamani zingefanywa na wasomi 40 zinafanywa na msomi mmoja tu, hivyo tatizo la ajira isiwe lawama kwa wasomi tu ati ni uchwara, ni jambo pana linalohitaji fikra kubwa...
 
Nchi imeongozwa na masomo toka mwanzo,
Wanaoharibu uchumi wa nchi ni wasomi haohao,
Wezi kwenye mabenki yetu ni wasomi,
Walioruhusu shule za matajiri zifundishe kwa kiingereza na za maskini zifundishe kwa kiswahili ni wasomi haohao.
Wanaoodoa na kuweka vikokotoo ni wasomi haohao.
Wanaotamani watanzania wenzao wawe maskini ili wawatawale ni wasomi haohao.
Wanaoshinda kwa waganga ili wawe watawala wa milele ni wasomi haohao.
Waliopanda ndege kwenda madagaska ni wasomi haohao.
Waliokwamisha katiba mpya ni wasomi haohao.
Waliosema Magufuli atawale milele na Leo amekufa wamegeuka ni wasomi haohao. Yako mengi ya kuandika.
Msukuma yuko sahihi
 
Nimesikiliza kwa makini wakati mbunge Musukuma akichangia leo bungeni, moja alikua akichangia kuhusu bajeti na kuwaita wataalamu wetu wa uchumi kua wataaalamu uchwara, hasa akitetea kuhusu wamachinga na kuondolewa barabarani hasa Kariakoo.

Hali iliopelekea Naibu Spika kumtaka aondoe neno hilo. Hivi kwanini mheshimiwa mbunge Musukuma kila akichangia anakua akiwasigina wasomi na kuwatukuza darasa la saba?

Hii inatokana na kutojiamini kwa kukosa elimu au kuna nini kafanyiwa na wasomi hadi chuki yake kufikia kiwango cha juu?

Au ndio kutaka kuwawini wananchi wengi ambao hawana elimu?
inferiority complex.

Kwa mtazamo wake, elimu ya juu iwe ni darasa la saba tu. Tufute sekondari na vyuo vyote visiwepo.
 
Hakukua na haja 'msomi' kufungua uzi kulalamika kuhusu mtazamo wa msukuma kuhusu wasomi...
 
Nimesikiliza kwa makini wakati mbunge Musukuma akichangia leo bungeni, moja alikua akichangia kuhusu bajeti na kuwaita wataalamu wetu wa uchumi kua wataaalamu uchwara, hasa akitetea kuhusu wamachinga na kuondolewa barabarani hasa Kariakoo.

Hali iliopelekea Naibu Spika kumtaka aondoe neno hilo. Hivi kwanini mheshimiwa mbunge Musukuma kila akichangia anakua akiwasigina wasomi na kuwatukuza darasa la saba?

Hii inatokana na kutojiamini kwa kukosa elimu au kuna nini kafanyiwa na wasomi hadi chuki yake kufikia kiwango cha juu?

Au ndio kutaka kuwawini wananchi wengi ambao hawana elimu?
Mosi msukuma ana wivu maana elimu imemkataa hivyo ana chuki nayo maana ukiangalia mporomoko wa biashara zake unatokana na "wasomi uchwara aliowaajiri!!"

Pili ni mtu mpumbavu pekee awezae kutusi wasomi ilhali akijua atakwenda maabara, kwa daktari, atatumia mtandao... mwanae anafundishwa shuleni... atatunza fedha zake benki nk kazi na huduma zote hizo ni wasomi wanazifanya...

Tatu; mshamba akiingia mjini akawa na vijisenti vichache lazima ajulikane!!

Nne; kama kweli anawapenda sana machinga basi awaachie eneo analoegesha mabasi yake mabovu pale Natta barabarani ili tumuamini akisemacho.

Tano; Ni kweli wapo baadhi wasomi wetu wanastahili kuitwa hivyo kwa maana wao na msukuma hawatofautiani....
 
Anahasira maana huenda elimu ilimkataa either kwa hali ya maisha yao yakipindi hicho au hali ya huko upstairs
Hivi mradi wake wa mabasi ya abiria, umeishia wapi? Au ni wasomi hao hao wamemharibia? Je, alishauriwa na wasomi kununua mabasi makuukuu, au ni IQ yake mwenyewe? Nauli Bukoba Mwanza kawaida elfu 20, yeye aliamua iwe elf 10, wajawazito na wazee bure. Sasa hivi mradi chali. Labda hayo ndo yanamchanganya akili
 
Nimesikiliza kwa makini wakati mbunge Musukuma akichangia leo bungeni, moja alikua akichangia kuhusu bajeti na kuwaita wataalamu wetu wa uchumi kua wataaalamu uchwara, hasa akitetea kuhusu wamachinga na kuondolewa barabarani hasa Kariakoo.

Hali iliopelekea Naibu Spika kumtaka aondoe neno hilo. Hivi kwanini mheshimiwa mbunge Musukuma kila akichangia anakua akiwasigina wasomi na kuwatukuza darasa la saba?

Hii inatokana na kutojiamini kwa kukosa elimu au kuna nini kafanyiwa na wasomi hadi chuki yake kufikia kiwango cha juu?

Au ndio kutaka kuwawini wananchi wengi ambao hawana elimu?
Mkuu angalia wasomi waliopo kwenye siasa nadhani utakubaliana kabisa na hoja za msukuma. Fanya utafiti japo kidogo juu ya wasomi wetu kabla na baada ya kuingia kwenye politics za bongo
 
Mwache awadharau kama wasomi wwnyewe kina KABUDI KINA KIGWANGALKLA MKUMBO AFADHALI HATA DARASA LA SABA
 
Mara zote dharau ni matokeo ya kutokujiamini au kujiamini kupita kiasi...

Ni ukuta ambao mtu hujijengea kumzunguka ili watu wasichokonoe udhaifu wake...

Hakuna nchi iliyoendelea inayoacha watu wake wafanye shughuli zao kiholela tu bila mpangilio, kama anawapenda sana hao wamachinga basi atoe hoja za namna ambavyo hawaharibu mpangilio qa miji/majiji...
 
Nimesikiliza kwa makini wakati mbunge Musukuma akichangia leo bungeni, moja alikua akichangia kuhusu bajeti na kuwaita wataalamu wetu wa uchumi kua wataaalamu uchwara, hasa akitetea kuhusu wamachinga na kuondolewa barabarani hasa Kariakoo.

Hali iliopelekea Naibu Spika kumtaka aondoe neno hilo. Hivi kwanini mheshimiwa mbunge Musukuma kila akichangia anakua akiwasigina wasomi na kuwatukuza darasa la saba?

Hii inatokana na kutojiamini kwa kukosa elimu au kuna nini kafanyiwa na wasomi hadi chuki yake kufikia kiwango cha juu?

Au ndio kutaka kuwawini wananchi wengi ambao hawana elimu?
Hiyo ndio silka ya wasio na elimu
 
Kwa sababu anaamini ana pesa, ila ni mjinga tu kama wajinga wengine
Ujinga wake ni Bora kuliko profesa aliyeacha jukumu lake na kukimbilia siasa ambayo imemungiza Bungeni, ndani ya Bunge hatoi wazo wala hashauri kabaki kupiga meza yupo nao huko ataacha kuwadharau.
 
Tena Jenista ni mbunge jimboni kwetu, lakini mambo anayofanya ni ujinga plus upumbavu mtupu. Halafu mroho wa madaraka hataki kuachia wengine. Msieeeew zake, tena ana Diploma tyuuh. Hovyoooooh
Tatizo wangoni mnaabudu sana watu wa CCM.

Sijui iliwapa nini?

Sisemi lazima mchague chama kingine, ila at least chagueni watu tofauti tofauti.
 
Kwa vile hajasoma,..Cha ajabu akiugua anaenda kutibiwa na wasomi na sio wasio wenzie...
 
Back
Top Bottom