Kwanini mbunge Musukuma anapenda kuwadharau wasomi wetu?

Kwani kila siku anaokota dhahabu?

Mtazamo finyu sana huu! Alichimba dhahabu pengine akapata mara moja au mbili lkn akaweza kuendeleza huo mtaji alioupata kupitia dhahabu huo pia ni uwezo si jambo la kubeza.

Au tuseme Kama kuokota dhahabu ni rahisi hivyo kwann hao wenye vyeti wanaojiita wasomi hawaendi kuokota?
Sasa fuatilia wanaoendesha biashara zake ili kuuendeleza utajiri wake sasa hivi uone kama ni LA SABA wenzake?
 
Siku ile nimemsikia alipokua akimdhalilisha profesa Muhongo ndio nilipoacha kumsikiliza Msukuma, jamaa ni muongo kupita maelezo yaani, eti "profesa Muhongo nilimwambia, mchanga wa Geita unaosafirishwa una dhahabu, profesa akabisha, raisi alivyopima akakuta kuna dhahabu" baadae nikafanya ka utafiti kangu kadogo, Geita ipi iliokua inasafirisha Mchanga? Nikapata jibu, GEITA HAISAFIRISHI mchanga anywhere in the world, now Msukuma alitoa wapi hiyo? Migodi iliokua inasafirisha mchanga ilikua ni 2 tu, nayo ni Buzwagi pamoja na Buli na yote haipo Geita, ni migodi ya Barrick/Acacia. Since that day, darasa la saba nitakae muheshimu ni Dr. Jumanne Kishimba pekee, mwanzilishi wa biashara ya supermarkets Tanzania, wakongwe mnaikumbuka Imalaseco ile ya Pamba house miaka ya 90? Sio huyu jamaa
 
Unakuta professor mzima kutoka chuo kikuu anamshukuru mwanasiasa kwa kumtoa JALALANI.

Unabaki unajiuliza,
Ina maana Miaka yote iyO professor alikua akifundisha JALALANI?

Inamaana zile nots na nondo zote alizokua akiwalisha vijana wetu zilikua Ni TAKATAKA za jalalani?

Unapata jibu kua,
Professor elimu haijamkomboa, Bali yeye ndie alieikomboa elimu
tapatalk_1584949270792.jpg
 
Bado tu hujaona kuwa hao wanaojiita wasomi wanajidharaulisha wenyewe kuajiriwa na darasa la saba?
Halafu kwani kuna league ya nani zaidi ?

Kwanini anahisi wasomi wanashindana naye ?

Vipi yeye watoto wake hapeleki shule ?

Maana Bakheresa ambaye naye hakwenda shule lakini alipeleka watoto wake na ndio wsnaendesha makampuni.
 
Unakuta professor mzima kutoka chuo kikuu anamshukuru mwanasiasa kwa kumtoa JALALANI.
Vyuo vikuu ni sawa na jalalani mkuu. Maslahi na mazingira ya kufanyia kazi ni duni sana ukilingqjisha na muda waliopoteza kuutafuta uprofesa .
 
Halafu kwani kuna league ya nani zaidi ?

Kwanini anahisi wasomi wanashindana naye ?

Vipi yeye watoto wake hapeleki shule ?

Maana Bakheresa ambaye naye hakwenda shule lakini alipeleka watoto wake na ndio wsnaendesha makampuni.
Wasomi wengi ni wakujiita tu wasomi kwasbb walitunikiwa vyeti lkn hawana impact yyte linapokuja suala la kuisaidia nchi.
 
Huyu hana usomi wowote huyu. Watu wa Pwani na elimu wapi wapi ? Ameunga unga sana huyu.

Anajua ngono tu huyu. Hapo alipo wana wake 4 na vimada wa kutosha.
Hilo suala la vimada na wanawake wanne ni maisha yake binafsi tujikite kwenye mada.
 
Kabisa!. Fikiria msomi kama Lisu anaamisha watu kwamba yeye akichaguliwa kuwa rais ndio tatizo la ajira litaisha wakati bibi yako kapambana bila hata Lisu kuwa mwenyekiti wake wa kitongoji na amewasomesha!
Ndio maana Msukuma anawadharau watu kama nyie
 
Vyuo vikuu ni sawa na jalalani mkuu. Maslahi na mazingira ya kufanyia kazi ni duni sana ukilingqjisha na muda waliopoteza kuutafuta uprofesa .
Kama mazingira ni duni,

Kwanini wasijiajili,
yaani professor mzima kabisa umesoma na una digrii zako nne inashindwa kabisa kujiajili na wewe unanung'unika mtaani Kama Walimu wa diploma.

Sasa elimu yako yote imekusaidia Nini Sasa Kama huwezi KUFANYA chochote mtaani kwako.

Afu ukikaa bungeni unashauri vijana wajiajiri.
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom