johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,915
- 141,872
Mbunge wa kinondoni ametokea kuwa maarufu sana katika siasa za nchi yetu hali iliyopelekea kuwavuruga kabisa Chadema na watoa nyaraka wengine. Ikumbukwe kuwa hata kule wilayani kwa mwenyekiti wa Chadema Hai katika jimbo la Siha alishinda Mollel aliyetokea Ukawa pia na kujiunga CCM lakini huyu haongelewi kabisa. Ndio najiuliza umaarufu wa Mtulia unatokana na nini?.......Je ni ukubwa wa chama alichotoka yaani Cuf au ni vile anatoka katika wilaya ya wajanja jijini Dsm?! Ni hayo tu, Pasaka njema!