Kwanini Mbatia haitishi kikao baada ya wabunge wake kususa muswada? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Mbatia haitishi kikao baada ya wabunge wake kususa muswada?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KING COBRA, Nov 16, 2011.

 1. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Nimefurahi sana kusikia kuwa Viongozi wa Juu wa Chadema wameitisha Kikao Cha kamati kuu kujadili Masuala nyeti baada ya Wabunge wake wote kutoka ndani ya Bunge kususia Kusomwa kwa Mara ya pili Mswaada wa Katiba mpya!!

  Pia nimefuatilia sana kwa Upande wa NCCR wabunge wawili tu (Davidi Kafulila na Felix Mkosamali) ndio waliotoka nje na kuungana na CHEDEMA wakati Moses Machalo na Agripina Buyoya walibakia ndani ya Bunge Kupima joto na baada ya joto la wananchi kuwa kali nao wametoka kinafiki na kuungana na CHADEMA.

  Hofu yangu ni Kwamba Jemu Mbatia ni CCM-C, Wakati CUF ni CCM-B, sasa CHADEMA wameitisha mkutano wa Kamati kuu kujadili suala hili na kulipeleka kwa Wananchi , Lakini Jemus Mbatia amenyamazishwa na CCM mpaka sasa Wabunge wake hawana msimamo wanasubili tamko la kamati kuu ya CDM.

  Pia Katibu mkuu NCCR alianza kwa kuwaponda Kafulila na Mkosamali huku akiwapongeza Moses na Agripina Je , hapo kuna Usalama!!
  Je, Kwa nini Jemus Mbatia asiweke wazi Msimamo wa NCCR na kukaa pamoja na Freeman Mbowe na kuweka msimamo wa pamoja juu suala la kugomea Mswaada???

  Je kuna umoja wa dhati kati ya Mbatia (CCM-C) na Chadema ??

  Mimi naona Mbatia ametumwa na CCM kuja kuharibu suala la maandamano ya katiba!!!
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  font uliyotumia inaonesha wewe ni kilaza na hatusumbuki kumwelekeza kilaza hapa
   
 3. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #3
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Maria,
  Angalia amejiunga lini na post zake zote zinahusu nini. Ndiye huyu huyu anajiita king cobra
   
 4. i

  ibange JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Msimamo wa Kafulila na Mkosamali si msimamo wa NCCR. Mbatia na uongozi wake ni wasaliti sawa na CUF lakini nawapongeza sana Kafulila na Mkosamali kwa ujasiri hata kuweza kutofautiana na chama. Kwanza hawawezi kuwafanya kitu hamkupata ubunge kwa vile mligombea kwa NCCR bali kwa nguvu yenu binafsi. Ingekuwa ni chama mgombea urais angepata kura kule. Unganeni na wazalendo wa chadema na nashauri chadema iwape nafasi za uwaziri kivuli
   
 5. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Hii hoja yako imekaa kimajungu majungu, kila mpenda mabadiliko hivi asa anatakiwa kutumia nguvu, raslimali alizonazo kuelimisha wote wanaomzunguka nini maana ya muswada kusmwa kwa mara ya kwanza na ya pili badala ya hizi personal issues
   
 6. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #6
  Nov 16, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Posti yako imekaa kimajungu majungu tu,
  unaonesha una chuki binafsi na James Mbatia.
  Pia tabia yako ya kukosea majina ya watu
  makusudi siyo nzuri kabisa, jifunze ustaarabu...
   
Loading...