Kwanini mawaziri wapya wa JK wanaingilia Bodi za wakurugenzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini mawaziri wapya wa JK wanaingilia Bodi za wakurugenzi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jun 7, 2012.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  1) Sikatai kabisa ATCL ilifanya madudu mengi sana katika nyanja zifuatazo:-

  a) uteuzi wa wakurugenzi waandamizi bila ya kufuata taratibu.

  b) Ukodishaji wa ndege kinyume na utaratibu na kulisababishia taifa hasara za mabilioni.

  Hapa na pale anakuja Waziri Mwakyembe - huyu ni mpya kabisa kutoka dukani - badala ya kuiwajibisha Bodi inayoongozwa na Mustafa Nyang'anyi yeye anawawajibisha watendaji waandamizi kazi ambayo siyo yake ni ya Bodi ya wakurugenzi.

  Mimi nilifikiri waziri shupavu atakachofanya ni kuiondoa Bodi ya wakurugenzi kwa kuhalalisha madudu lakini yeye anairuka Bodi iliyoko ndani ya uwezo wake na kuingilia kwenye majukumu ambayo yako nje ya uwezo wake na kuyafanya! Huu kweli ndiyo utawala bora?

  2) Sikatai kwenye shirika la TBS upo ushahidi wa kutosha wa ya kuwa TBS kufanya madudu makubwa ambayo yameligharimu taifa zaidi ya mabilioni 30.

  Sasa Waziri mpya kabisa naye kanunuliwa kwa bei mbaya kutoka dukani anakuja kuiagiza Bodi ya TBS kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu kwa minajili ya kupisha uchunguzi, kazi ambayo Bodi hiyo walipaswa waifanye na hawakuifanya.

  Kwa lugha nyingine Bodi tajwa imeshindwa kulisimamia shirika tajwa na ndiyo ilipaswa kufanya kazi na imechelea kwa sababu wazijuazo wao. Huu kweli ni utawala bora wa kuacha kuwajibisha chombo kilichoko ndani ya uwezo wa waziri na kuingilia Bodi kwenye majukumu yake?

  Sababu kubwa ya kuziweka Bodi za wakurugenzi ni kupunguza na kufifilisha wanasiasa kuendesha taasisi za umma kwa minajili ya kukidhi mahitaji yao ya muda mfupi ya kisiasa.

  Pamoja na nia nzuri ya kufuta ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka ndani ya taasisi za umma lakini mawaziri hawa wapya wa JK wanapovunja taratibu kwa visingizio kuwa lengo ni kurekebisha makosa siyo sahihi hata kidogo. Huwezi kuvunja sheria na kutumia visingizo vya kuboresha wakati wewe mwenyewe ni mkosaji tu............

  Nionavyo mimi ni kuwa hawa mawaziri wapya wa JK wanawaogopa wenyeviti wa Bodi kwa sababu hawakuwateua wao bali wameteuliwa na Raisi. wanaogopa kuhatarisha posho yao n ahivyo wanzilinda Bodi za wakurugenzi lakini wanaelewa pia ili kuulinda mlo wao lazima wachukue hatua na hivyo kusababisha huu muingiliano wa majukumu ambao unakatzwa na sheria.

  Hivyo badala ya kuwaondoa watajwa hao basi mawaziri wanawaingilia kwa kufanya yale ambayo wao mawaziri wanataka yafanyike kwa sababu zao za kisiasa na hivyo kufifilisha maana nzima ya kuwa na hizi Bodi za wakurugenzi ambazo zinatugharimu mapesa mengi sana katika kuzikarabati.


   
 2. Kyaiyembe

  Kyaiyembe JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Una majibu ya swali lako mkuu, Waziri hawezi kumgusa mjumbe wa BODI YA WAKURUGENZI maana wote ni watoto wa baba mmoja na wote lao moja "wizi"
  Sasa ili waonekane wamefanyakazi ulitaka wafanye nini?.
  Yote yanatokana na madaraka makubwa aliyonayo Rais.
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Inasemekana wakurugenzi ndo waliosababisha mawaziri wenzao kuwajibishwa!
  Wapo makini kweli!
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Kyaiyembe hawa wakubwa wameingilia kazi za Bodi na hayo ni matumizi mabaya ya madaraka.......mawaziri hawa wameingia kazini kaw pupa lakini wanavuruga nchi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  hoja nzuri Mungi..........jana naona uliingia mitini ....lol............ni kweli hawa ndiyo walisababisha wenzao wafukuzwe kazi na hadi leo bado wanatesa.................ikoje hii wamerukwa na wadogo zao kitanzini
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mkuu ni kweli niliahidi kurudi lakini ndo hivyo, hata uongo ni sehemu ya mwanasiasa. Rutashubanyuma
  Hao wenzao wamekwepa kitanzi kwasababu hawakuwa signatories
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #7
  Jun 7, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Hivi kwanini taratibu sizibadilishwe ili wenyeviti/ wakurugenzi wa bodi mbali mbali wawe wanateuliwa na mawaziri wa wizara husika ili pindi waziri ama mtendaji anapo vurunda waziri aonekane wazi wazi kufanya kazi..japokua kutakua na kukingiana kifua lakini hii itawamwaga sana watendaji wa mashirika ya umma kwa kutolewa kafara na bodi za wakurugenzi..mazashit!-
   
 8. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Nchi yetu inamatatizo makubwa sana kwenye governance kiasa kwamba watu hawaheshimu mipaka ya kazi zao tena. kwa ATCL haina bodi kwani ilishamaliza muda wake na sasa ni zaidi ya mwaka shirika linaendeshwa kimagumashi.
  TBS kulindana kwingi kulianzia waziri hadi bodi kwani wajumbe si kawaweka waziri.

  kinachotakiwa kifanyike kama sekta binafsi kwamba waziri angeteua wajumbe wa bodi kisha miongoni mwao wachague wenyewe mwenyekiti kisha wakabidhiwe shirika na wao ndio wafanye interview ya Mkurugenzi wa shirika(Kama hamna) ambaye atawajibika kwao. sio huu mtindo bodi kaweka waziri mkurugenzi kaweka waziri/raisi nani atawajibika kwa nani? wakurugenzi wanaviburi kwa bodi kama nini maana haijamuweka hapo.
   
 9. Ng'wamapalala

  Ng'wamapalala JF Gold Member

  #9
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 6,332
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 145


  Hapo umenena lakini kumbuka Wenyeviti/Wakurugenzi wanateuliwa na Raisi baada ya kushauliana na Waziri wa wizara husika, tatizo linakuja pale uteuzi unakuwa niwa kisiasa kisiasa badala ya kiutendaji na ndiyo maana inakuwa vigumu kwa waziri anayeteuliwa au kuhamishiwa kwenye wizara na kuikuta bodi hiyo ya wakurugenzi ambayo mara nyingi huteuliwa kisiasa kisiasa. Waziri kisheria anakuwa amepewa madaraka ya kuiwajibisha lakini "kisiasa", anakuwa hana hayo madaraka. Hapa ndo tunarudi kwenye tatizo la Raisi kuwa na madaraka makubwa.
   
 10. m

  mamajack JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  yaani tunaoga kuwajibishana maana tunapenda sifa za kijinga,na mie nawaambia,haya mambo yakiendelea baada ya miaka nchi hii tutakuwa na hali mbaya sana,watu wanofanya madudu wanaogopwa sababu wanae mtu mkubwa anayewalinda na hayo mabaya yao yanafaida kwake,na pia kunawatu wanatumiwa kurahisisha mambo ya watu,mwisho wa siku wanakuja kuumia na kuumbuka wao,wewe unapewa kazi usimamie ila mwenyenyumba au waatoto wake wakitaka kitu wanauhuru wakuchukua mda na wakati wanaotaka wao.aibu inabaki kwako sasa,sie wanachi tunakuona wewe,na majibu ya maswali yetu tunataka kutoka kwako,wakati kuna watu uliokubali wakutumie nawewe kwa vile unataka utoke(utajirike)unakubali tu bila kuangalia nini kitatoke.then yakiharibika mambo unapozwa kwa maneno ya matumaini hapo ulishaharibu heshima utu etc.wateuliwa fanyeni kazi kwa akiri na utashi mlopewa na mungu,penye kusema no semeni.BORA KUWAJIBISHWA KWA KUTENDA JEMA KULKO KUPATA SIFA AMBAZO ZINAKUHARIBIA SIFA,UTUNA UZALENDO.
  paul chizi wewe ni mzalendo na umewajibishwa kwa kutenda jema,though tunajua hakuna aliyemkamilifu.
   
 11. W

  WFM Senior Member

  #11
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 122
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 45
  Waziri - KCU amemsimamisha kazi DG wa Bodi ya Pamba wakati ambao msimu unatakiwa kufunguliwa na bei ya pamba kutangazwa. System ime-paralyse hadi waziri mwenyewe anaonekana hajui cha kufanya. Bodi ilitakiwa kuwajibika kwa kushindwa kumwajibisha DG. Hii serikali sasa ndo inazidi kuwa kichekesho. Wasipostuka sijui km watafka 2015.
   
 12. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  mbona nasikia hawana bodi sikun nyingi tu!
   
 13. Ng'wamapalala

  Ng'wamapalala JF Gold Member

  #13
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 6,332
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 145

  Sikubaliani na wewe kuhusu hili. Kuna mifano mingi tu ambayo inaonyesha kuwa wakati mwingine ni vizuri kuvunja sheria kwa manufaa ya umma katika mazingira yanayohitaji utekelezaji wa haraka ili kujipanga upya badala ya kusubiri taratibu za kisheria ambazo zinachukua muda mrefu kuzikamilisha. Kumbuka sheria zetu mara nyingi ni mbovu na zinahitaji marekebisho( sisemi kama ndiyo excuse) lakini hiyo ni sheria ya hekima na busara katika mazingira kama hayo.
   
 14. Kyaiyembe

  Kyaiyembe JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Jaribu kumshawishi Rais akuteue Wenyeviti/Wakurugenzi kutoka upinzani ili wasionewe huruma na watawala!.
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Mungi huo sio utetezi kwani mawaziri walipowajibishwa walikuwa ni ma-signatories................ni uwajibikaji wa eneo ambalo unalisimamia tu..........
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  [MENTION]
  Kyaiyembe[/MENTION] tatizo mie ni ccm siko upinzani.....lol
   
 17. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #17
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  [​IMG] [MENTION] Ng'wamapalala[/MENTION] sheria ni msumeno na unakata pande zote mbili.....tukiruhusu huu utaniutani wako basi siku moja tutasema people's power waongeze nchi na kisingizio sheria zetu zina mapungufu................kama zina mapungufu ni kuzirekebisha na wala siyo kuzisigina tukifnya vinginevyo ni kuashiria vurugu..............kuchukua sheria mkononi ni vurugu tupu na inapoanzia kwa viongozi ni balaaaaaaaaaaaaaa
   
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  [MENTION]andrewk[/MENTION] kama hawana bodi tena ni mbaya zaidi kwanini isiteuliwe ikafanye kazi isije wanchelewesha kuteua bodi ili kupitisha mambo yao..............na bodi zipo kisheria iwepo isiwepo huwezi kuiingilia..................period
   
 19. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #19
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  If they were not signatories, na kwamba issue ni accountability, bado unakubaliana na mimi kuwa wakubwa walistahili kuwajibishwa kwa kuwa manaibu hawakuwa the finals. Rutashubanyuma
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  mamajack ninaamini wamekusikia
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...