Kwanini Mawaziri wanemwachia Waziri Mkuu suala la Ngorongoro! Kiti chake kipo salama tuendako?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Kwa mtizamo wangu suala la Ngorongoro ni suala la sekta au Wizara na siyo suala linalopaswa kusimamiwa Moja Kwa Moja na Waziri Mkuu. Ni suala lenye dynamics nyingi zikiwemo zinazoweza kufifisha Imani ya mataifa mbalimbali dhidi ya utawala uliopo madarakani. Ni suala linalofifisha ndoto za Mhe. RAIS Kwenye Royal tour, ni suala linaambatana na matumizi ya nguvu na umwagaji damu.

Kwa mfumo unaoona mbele, Waziri Mkuu asingepaswa kuwa mstari wa mbele, Wizara zilipaswa kupichakata na kwenda nalo huku Waziri Mkuu akipewa mrejesho. Kitendo Cha Waziri Mkuu kuonekana mwongo kilichotokana na kauli yake, kauli ya RC na Mbunge kinatosha kufungua milango ya nafasi yake kuwa wazi Kwa Waziri Mkuu mpya. Kitendo hiki kingetoa Kwenye nchi ambazo binadamu wanaamini damu ya maskini na tajiri zote ni dawa na uhai ni mmoja basi Waziri Mkuu alipaswa kujiuzulu au kufutwa kazi.

Lakini swali ninalojiuliza ni Kwanini Kila wakati Waziri Mkuu amekuwa akigombanishwa na wananchi? Kipindi cha koroshio alilazimishwa kuwakana ndugu zake wa kusini lakini Leo hii anabebeshwa mzigo ambao naamini wakubwa zake wasingetamani waubebeshwe. Kwanini wamempa hii kazi?

Kwa muundo wa Sasa wa serikali TAMISEMI ipo chini ya Rais na Kwa mantiki hiyo tulitegemea Waziri mwenye dhamana achukue hatua na Waziri Mkuu awe awe mpokea taarifa tu: Kwanini wamemweka mbele? Ndivyo muundo wa serikali unavyotaka au Kuna kupitiwa?

Naamini suala hili tayari limemwondolea credits za Kisiasa na linazidi kumpaka matope. Nitoe Rai Kwa wanaomtakia utumishi mwema Waziri Mkuu na wanaopenda abaki na Imani yake ya dini bila kuathiriwa na majukumu wamtue huu mzigo. Hata kama ni mwanzo wa Vita ya Urais basi Bora mpitie njia nyingine lakini siyo hii ya loliondo. Mtueni huu mzigo upekelekeni Kwa wakuu wa wilaya, Mikoa na msimamizi wa TAMISEMI. Likibumburuka basi viongo watatu wa juu mpate wa kukuwajibisha kuliko kuvunja baraza la Mawaziri.

Naamini Mhe. Waziri Mkuu unapousoma ujumbe huu utaelewa Kwanini Lowasa alisema TATIZO NI UWAZIRI MKUU; siyo vicheko vyote ni vicheko, unaelekea kuwa mhombea after samia lakini unapoteza sifa hizo Kwa kuishi na marafiki ambao siyo marafiki; mwombe MUNGU akupe upeo wa kupita njia sahihi kufikia malengo Yako kisiasa
 
Let them hang him out to dry. That SOB is a pathological liar! Jitu ongo kiasi hicho la nini sasa?
 
Back
Top Bottom