Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Kuna kitu ambacho kinanishangaza sana kuhusu Mawaziri wetu hasa kuhusu matamko yao, wamekuwa wakitoa matamko mengi na yenye deadline lkn mwisho wa siku deadline hupita na hakuna kinachofanyika, sasa swali langu ni kwamba ni kwa nini unatangaza kitu kama unajua kwamba utekelezaji wake ni mgumu sana?
Kwa mfano sasa hivi nimemsikia W. wa Elimu akitangaza kwamba Vyuo visivyo na vigezo na amevitaja hivyo vigezo kufungiwa lkn ukweli ni kwamba kulinganana na mazingira yetu jinsi yalivyo siamini kama kweli hivyo Vyuo vitafunngiwa hata kama havikidhi hivyo vigezo na sababu kubwa ni moja, hao wanafunzi watawapeleka wapi? Kwa maana kulinganana vigezo walivyovitoa ni kwamba vyuo vingi sana havitimizi, sasa kuna ulazima gani kutangaza? Kwa nini wasifanye tu kimya kimya?
Haya leo nimesikia W. Ardhi Lukuvi katoa siku 18 kwa Jengo la ghorofa 16 libomolewe ukweli ni kwamba hizo siku zitapita na halitabomolewa, sasa kuna haja gani ya kusema kwanini wasitende tu?
Si muda mrefu W.Mkuu aliwapa DART na Halmashauri mpaka tarehe 10 Januari mradi wa mabasi uwe umeanza kazi leo ni tarehe 14/01 hata dalili za kuanza hamna, sasa yote hii ni ya nini?
Siwafanye kazi kimya kimya tu halafu watu tuone matokeo badala ya kutangaza halafu hakuna kinachotokea?

Last edited: