Kwanini matumizi ya data Halotel ni makubwa ukilinganisha na Vodacom/Airtel?

wolf5100

Member
Apr 9, 2016
58
26
Habari wakuu, naomba kufahamishwa kitaalamu.Mimi ninafanya shughuli za ujenzi na shughuli mbalimbali za kiuchumi.

-Huwa natumia sana internet ya vodacom na halotel.Lakini nimekuwa nikichunguza kwa makini nikagundua halotel data zinakwenda sana ninapotumia kuliko vodacom.

-Je ni kwasababu ni mkonga wa Bahari au? Na hao wengine vodacom wanatumia nini?Sio mjuzi sana kwenye mambo ya telecommunications. NAWASILISHA.
 
Ni kawaida ndugu, strength ya mtandao ndiyo ina determine data consumption, kwa maana nyingine kadri mtandao wako unavyokuwa na kasi/speed ndivyo data zinatumika kwa kasi zaidi.


Kwa kufupisha ni kwamba Halotel mtandao wao uko strong zaidi ya Voda.
 
Hapo kwenye H ya vodacom ni sawa na E halotel hujatenda haki mkuu embu tuambie spee ya E na speed ya H?hata huo mtandao wa E ungekua mwendo wake ni wa konokono au kinyonga ukweli E hauwezi kuupita uwe mkweli kwa hilo au weka data sahihi kwa manufaa ya wengi
 
Hapo kwenye H ya vodacom ni sawa na E halotel hujatenda haki mkuu embu tuambie spee ya E na speed ya H?hata huo mtandao wa E ungekua mwendo wake ni wa konokono au kinyonga ukweli E hauwezi kuupita uwe mkweli kwa hilo au weka data sahihi kwa manufaa ya wengi

Kweli wengi wanaongea ushabiki humu, seriously kivipi kwanza mtu utaanza kupambanisha mtandao wenye EDGE vs HSDPA
 
Kweli wengi wanaongea ushabiki humu, seriously kivipi kwanza mtu utaanza kupambanisha mtandao wenye EDGE vs HSDPA
Hi pia inawezekana, utofauti kati ya EDGE na HSDPA unategemeana na aina yako ya simu unayotumia, mfano ni ngumu sana kwa smartphones kufanya vizur ikiwa ipo EDGE, lakin kwa simu za kawaida kama vi Itel Vya kawaida EDGE huwa inasupport vizuri tu mkuu
 
sasa 500mb kwa 500tzs si hadi niwe na simcard ya nwanachuo? Mi ninasimcard niliyonunua halotel shop.so sijui kama ni ya mwanachuo
 
Mhh hii mpya inawezekana lakini sio kweli kama kila kitu ukikifanya sawa moja haiwezi kuisha haraka zaidi ya nyingine mfano natumia tigo 4g yenye speed zaidi ya halotel lakini zile 600 mb kwa buku, sijaona kama za tigo zinaisha kabla ya za halotel au za halotel kabla ya za tigo kwa matumizi yangu ya kawaida Facebook, instagram, youtube 360p, jamii forums, reddit, whatsapp, update applications.

Na pia kumbuka data wanaokupa mitandao ya simu kama ni 500mb hiyo ni both upload na download data.
 
inategemea unafanya nini internet kwa haraka haraka hizi zinaweza kuwa sababu.

1. unaingia websites ambazo zinakupa data kutokana na speed yako mfano youtube, jinsi speed yako ya internet inavyokuwa kubwa na wao wanakupa video zenye quality zaidi na zinazokula mb nyingi.

2. vifurushi unavyojiunga havipo sawa, kama huna line ya chuo halotel vifurushi vyao ni bei ghali na mb ni chache hivyo inawezekana umenunua kifurushi kina mb kidogo na kupelekea kuzimaliza mapema.
 
Speed mkuu, halotel iko speed Sana compare na hizo kampuni nyingine. More speed more data consumption

How? speed ina-determine how fast/long data can be downloaded/uploaded, siamini kama niki-download movie ya GB 1 kwa halotel ziende GB 2 eti kisa ni speed. Speed itaninfanya nidownload hiyo GB 1 kwa haraka na sio kuongeza idadi ya kile ulichopakua. Tafadhali niambie how GB 1 inavyoongezeka kwa sababu ya speed
 
Back
Top Bottom