Kwanini Matajiri wa siku hizi hawawezi kuishi na watu wengi majumbani mwao kuliko wale wa enzi za zamani?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,570
15,319
Miaka ya nyuma, hata urudi katika vitabu vitakatifu, watu matajiri waliishi na watu wengi nyumbani na wote walinyooshwa na kutii sheria za nyumbani.

Mfano Nabii Ibrahim alikuwa Bilionea aliyeishi na mamia ya watu kwenye familia yake. Alikuwa hadi anajeshi la watu 300 ambao ni sehemu ya familia yake.

Wazee wetu matajiri wa zamani walikuwa na wake wengi pamoja na watoto kibao. mji ulikuwa na ndugu lukuki hadi wale walioomba jujiunga na undugu. Bado wote walinyooshwa kwa mkono wa chuma, unaweza usisikie hata mtoto anamimba bila kuolewa.

Siku hizi tatizo ni nini?

Unakuta mtu tajiri, hajiamini, anaishi na vitoto vyake viwili na housegirl/Boy na mkewe. Hataki kusikia shangazi, mjomba wala kuarika watu kwake.

Karibuni kwa maoni.
JE uwezo wa wanaume wenye pesa mingi kutiisha familia zao umeshuka?

Je, utajiri wa hofu?

Je, ndugu na marafiki wa zama hizi usnitch na umbea umezidi kiasi kwamba huwezi kuwanyoosha?

Unadhani kwanini
 
Umagharibi unatuumiza, tunafata maisha ya magharibi, tunageza kila Jambo.

Hatimae siku hizi hatuna mapenzi, mtu anaishi miaka dahari hajuk jirani yake anaishi vipi, ni kwenye gari, akirudi ndaani.
Nyumbani ni yeye na watoto zake wawili, mbwa na wafanyakazi.

Hilo moja, pili(nazungumzia mpaka masikini) Maisha yamebadilika, mahitaji siku hizi si nguvu ni pesa inahiitjika, zamani unaishi na mtoto wa mjomba, sijui nani na nani, ila una shamba kubwaa nguvu ya kulima((nguvu kazi ipo) una ng'ombe kadhaa.

Asubuhi mnakamua lita kadhaa ndani mipunga kibao na mahindi, nyuma kisamvu, matembele, maboga maisha yanasogea. Ila siku hizi kimbembe, ugali tabu, huna hela hujala, mjini una chumba na sebule tu.
 
Ila kweli nakumbuka mjomba wangu mwenyezi Mungu amrehem ukifika kwake ilikuwa ndio sehemu yakujua ndugu maana nyumbani kwake kila mwenye shida na asiye na shida ilikuwa kimbilio, la wagonjwa, wanataka kusoma, kazi au mtaji na katika biashara zake walikuwa ndugu na jamaa wa karibu.

Sasa kabaki yule Shangai mnoko hatari, kweli kizuri akiishi daima.
 
Lakini ujue jambo hili, kwamba katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari zilizo ngumu kushughulika nazo.2Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda pesa, wenye kujidai, wenye majivuno, wakufuru, wasiotii wazazi, wasio na shukrani, wasio washikamanifu,3wasio na upendo wa asili, wasiotaka makubaliano yoyote, wachongezi, wasiojizuia, wakali, wasiopenda wema,4wasaliti, wenye vichwa vigumu, waliojaa kiburi, wanaopenda raha badala ya kumpenda Mungu,5wakionekana kama watu wanaomwogopa Mungu lakini wakizikana nguvu zake; nawe jiepushe nao.
 
Miaka ya nyuma, hata urudi katika vitabu vitakatifu, watu matajiri waliishi na watu wengi nyumbani na wote walinyooshwa na kutii sheria za nyumbani.
Mfano Nabii Ibrahim alukuwa Bilionea aliyeishi na mamia ya watu kwenye familia yake. Alikuwa hadi anajeshi la watu 300 ambao ni sehemu ya familia yake.

Wazee wetu matajiri wa zamani walikuwa na wake wengi pamoja na watoto kibao. mji ulikuwa na ndugu lukuki hadi wale walioomba jujiunga na undugu. Bado wote walinyooshwa kwa mkono wa chuma, unaweza usisikie hata mtoto anamimba bila kuolewa.

Siku hizi tatizo ni nini?
Unakuta mtu tajiri, hajiamini, anaishi na vitoto vyake viwili na housegirl/Boy na mkewe. Hataki kusikia shangazi, mjomba wala kuarika watu kwake.

karibuni kwa maoni.
JE uwezo wa wanaume wenye pesa mingi kutiisha familia zao umeshuka?

Je utajiri wa hofu?

Je ndugu na marafiki wa zama hizi usnitch na umbea umezidi kiasi kwamba huwezi kuwanyoosha?

unadhani kwa nini
Hizi ni siku za mwisho hii traller kuna mengi yanakuja
 
Hapana, watu hawana fadhila tu siku hizi.

Unamuweka mtu kwako anaanza kufanya upuuzi na watoto wako. Unasomesha watoto wa dada zako lkn wakienda kwao wanakusema hadi unapariwa ukiwa unakula,

Yaan watu tumekuwa wa kukosa shukran kabisa. Zamani kama mtu sio mtoto wa familia anapokaa anakua anajua nafasi yake, ila siku hizi mtoto wa shangazi kaja kukaa hapo anataka na yeye ahudumiwe vilevule kama watoto wa mwenye mji, akikosa hata point atakupaka maneno wakati anapewa vitu ambavyo wazazi wake wasingeweza kumpa.

Ni kubadilika tu kwa tabia za watu hasahasa wanaosaidiwa ndo kumeleta hii hali
Umesema kweli ,kama una shamba wakalime wasikae bure
 
Kuna hutuba moja ya Nyerere anasema"ni fahari Sana kuitwa mzungu mweusi ilihali huku tukiacha utamaduni wetu"kwasasa ni baba/mama na watoto Tosha kabsa uzungu weusi umetuingia sasa,

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Ila kweli nakumbuka mjomba wangu mwenyezi mungu amrehem ukifika kwake ilikuwa ndio sehemu yakujua ndugu maana nyumbani kwake kila mwenye shida na asiye na shida ilikuwa kimbilio, la wagonjwa, wanataka kusoma, kazi au mtaji na katika biashara zake walikuwa ndugu na jamaa wa karibu.

Sasa kabaki yule Shangai mnoko hatari, kweli kizuri akiishi daima.
Tafuta kazi ufanye

Hospital kwa sasa zipo kila kanda sio lazima kwenda kwa watu

Unamchukia mtu kisa kwake
 
Ila kweli nakumbuka mjomba wangu mwenyezi mungu amrehem ukifika kwake ilikuwa ndio sehemu yakujua ndugu maana nyumbani kwake kila mwenye shida na asiye na shida ilikuwa kimbilio, la wagonjwa, wanataka kusoma, kazi au mtaji na katika biashara zake walikuwa ndugu na jamaa wa karibu.

Sasa kabaki yule Shangai mnoko hatari, kweli kizuri akiishi daima.
Kwahiyo unabishana na mzee makamba 😅
 
Back
Top Bottom