Kwanini mataifa yote duniani yasizalishe hela nyingi ili kuondokana na umasikini?

Rwekaxa Autonomy

JF-Expert Member
Apr 6, 2021
460
492
Heshma kwenu wadau,

Nimekuwa nikijiuliza Kwa nini kila nchi duniani isizalishe hela nyingi ili watu wao waondokane na umaskini hasa kwenye nchi zetu za Afrika na Asia.

Naomba kwa wabobezi mnisaidie hapo je hatuwezi kuzalishwa hela nyingi?

Au kiuchumi ,uzalishaji wa hela una gharama kubwa Sana?

NATANGULIZA SHUKRANI
 
Ningependa nikupe assignment, Google "why money was introduced". Ukimaliza google " why can't we print more money?"
 
Muulize hilo swali Mugabe marehemu na Zimbabwe. Watakujibu. Mfano ukizalisha sana Tshs. Hakuna nchi yeyote duniani inatumia tshs zaidi ya Tz. Manake tshs zitajazana nyingi sana Tz. Kila mtz atakuwa na hela. Sasa kama kila mtu ana hela nyingi Tz, hata mmachinga ambaye sasa hivi ana labda shs 20,000 kwa akaunti akawa na 200,000. Mtu mwenye 2,000,0000 akawa na tshs 20,000,000. Una 20,000,000 unataka kununua kiwanja ambacho awali kilikuwa kinauzwa kwa shs 2,000,000 (2 million). Huyo mtu wa kiwanja na yeye alikuwa anashika 300,000 kwa mwezi, sasa ana 3,000,000 kwa mwezi na kiwanja hauzi tena. Mwanzoni watu watakusanya tu hela, na kila mtu akishakuwa nazo nyingi, ndio kila mtu ataona kuuza vitu bei ya mwanzo haifai sababu teari ana hela nyingi. Manake nina shs 20million, sasa ni kwa nini niuze kitu nipate laki moja? Kila mtu atapandisha bei ya vitu = INFLATION, na itazidi kupanda tu hadi mwisho hela inakuwa haina thamani tena kama zimbabwe. Kwa ufupi, kitu kikiwa kingi sana hata mahindi, thamani yake inapungua. The same pia kwa hela.
 
Mkubwa anataka tuwe tunagawiwa, bila kutafuta shughuli yetu iwe moja tu, kufanya matumizi, halafu tunagawiwa tena hivyo hivyo, simpo!:D

Everyday is Saturday...............................
sio bure KWA nn umasikin utamalaki dunian
 
Heshma kwenu wadau,

Nimekuwa nikijiuliza Kwa nini kila nchi duniani isizalishe hela nyingi ili watu wao waondokane na umaskini hasa kwenye nchi zetu za Afrika na Asia.

Naomba kwa wabobezi mnisaidie hapo je hatuwezi kuzalishwa hela nyingi?

Au kiuchumi ,uzalishaji wa hela una gharama kubwa Sana?

NATANGULIZA SHUKRANI
Hii ingekua ni siri yako wewe mwenyewe kwa kutengeneza hela nyingi kama wanavofanya wategeneza pesa bandia, kwa vile wewe ndio mwenye shida ya hela.
 
Back
Top Bottom