Kwanini Masoud Kipanya (KP) ni bora kuliko wengine kwenye sanaa ya uchoraji vibonzo?

KITAULO

JF-Expert Member
Apr 27, 2018
1,926
2,777
Wana JF,

Kati ya cartoonist/ wachora vibonzo ninao wahusudu/ wakubali basi wa kwanza ni bwana Masoud Kipanya. Huyu msanii anajua. Narudia tena kusema anajua kuwakilisha ujumbe mahususi kwa kutumia vibonzo/lugha ya picha, mara nyingi huwa zinachekesha na wakati huo huo kutoa ujumbe kwa jamii/kuelimisha.

Nachopenda kutoka kwake sana sana ni kwa vile mtu mzima huyu hana double standard, hukosoa yeyote yule anayekiuka bila kujali nafasi yake. Tumeona mara nyingi akichora vibonzo vya Mheshimiwa Magufuli na mara kadhaa serikali imekuwa ikimchukulia hatua ikiwemo kushikiliwa na Jeshi la Polisi.

Mara nyingi ni vigumu kung'amua nini anachotaka kuelezea, ni werevu pekee ndio huwa wanaelewa japokuwa vibonzo vyake huwa na maana zaidi ya moja.
 
Wanakuambia Class is permanent Form is temporaly.

Kichwa kikubwa kimebeba makubwa.
 
Back
Top Bottom