Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,152
- 10,862
Hizi mashine eti zinajaa na ikitokea hivyo unanunua kwa bei ile ile ya karibu ya milioni.
Ajabu ni kuwa mashine hizi zinazotumiwa na TRA kukusanyia kodi haziendi hata miaka 3 kujaa kwake na hasa ukiwa ni mlipa kodi mzuri unayetoa risiti kwa kila mauzo.
Inakuwaje mashine hizi zikijaa zisifutwe tu kile kilichojaa kama hakitakiwi tena na mlipa kodi akaendelea na mashine yake.
Au kwanini kusiwe ni kifaa cha pesa ndogo kubadilishwa na mashine kuendelea kutumika.
Kwanini tumeruhusu teknolojia ya kinyonyaji na kuongeza uzito wa biashara.Na kwanini tuendekeze matakwa ya makampuni ya kinyonyaji badala ya wao kufuata masharti yetu katika kutuuzia vifaa vyao.
Ukiondoa huko kujaa kwa mashine pia mashine zenyewe hazikawii kuharibika na kosa lolote wasambazaji wanataka pesa tele kuiangalia.
Vipi TRA hawaoni kuharibika mara kwa mara kwa vifaa hivi vinachangia kupunguza kodi na kwamba ni mzigo kwa mlipa kodi.