SoC01 Kwanini mashabiki wa mpira wanakufa kwa matatizo ya moyo?

Stories of Change - 2021 Competition

Bayga

New Member
Sep 20, 2021
1
1
Mashabiki wengi kipenzi wa mpira wapo hatarini kufa au kuathiri afya zao kutokana na magonjwa ya moyo, Kiharusi na matatizo ya kisaikolojia kwa mjibu wa utafiti uliochapishwa katika jarida la Current problem in cardiology na katika jarida la Stress and Health mwaka 2020.

19-01-52-images.jpg

#Picha | Mwanaspoti

Timu ya mpira inapofungwa homoni ya cortisol huzalisha kwa wingi ambayo hiyo huathiri mpaka utendaji kazi wa moyo. Hiyo ilithibitika baada ya kuchuguzwa kwa mashabiki katika kombe la dunia la mwaka 2014 ambapo Brazili walifungwa magoli 7 kwa 1 na Germany.

Je inakuwaje mpaka mtu anakufa kwa sababu ya ushabiki?

18-53-08-heart-attack.png

#Picha | Cardiac speciality institute.

Jambo ambalo hutokea kwake ni mabadiliko ya utendaji kazi wa moyo kwa sababu ya homoni na athari zake katika mishipa ya damu.

Mabadiliko ya gafla katika mzunguko wa damu, kushindwa kufanya kazi kwa sehemu za ndani za mishipa ya damu ile midogo ya arteri na kusisimuka sana kwa neva za sympathetic baada ya timu kufunga goli huathiri moyo kuzuia damu isigande.

Kitendo hicho kupelekea kutengenezwa kwa mazingira ya damu kuganda na kuvurugika kwa mapigo ya moyo. Damu ikiganda inaweza kuziba kwenye mishipa hiyo midogo ya damu.

Pia, kushindwa kufanya kazi ipasavyo kwa sehemu za ndani(epithelium) za mishipa midogo ya arteri huathiri damu ufikaji wa damu kwenye misuli ya moyo. Mishipa hiyo husinyaa sana na kupunguza au kutokupitisha damu kabisa kwenda kwenye misuli ya moyo. Misuli ya moyo hushindwa kufanya kazi ipasavyo au moyo kufa kwa gafla kwa sababu ya kukosa oksijeni inayobebwa kwenye damu.

Mabadiliko ya gafla wakati hasa goli linapofugwa hupandisha shinikizo la juu la damu. Shinikizo la juu la damu huleta usumbufu kwenye mtiririko wa damu, hiyo inaweza kupelekea damu kuganda na kuziba kwenye mishipa midogo ya damu au mishipa midogo ya damu kushinyaa gafla kuliko kawaida na kupunguza damu inayokwenda kwenye misuli ya moyo.

Damu ikipungua ua kutokupita kabisa, moyo unaweza kushindwa kufanya kazi vizuri gafla (shambulio la moyo) au moyo kufa gafla.

Kama mtu amepata shambulio la moyo anaweza kufa gafla au kuhisi maumivu makali ya kifua, kwenye mkono au chini ya titi la kulia, kifua kuwa kizito, kushindwa kupumua, uchovu usioelezeka, kutoka jasho, kizunguzungu, tumbo kujaa au kushindwa kusaga chakula na mapigo ya moyo kwenda haraka au bila utaratibu.

Hali huwa mbaya sana kwa mshabiki kipenzi wa mpira ambaye tayari ana historia ya matatizo ya moyo.

Mbali na magoli kitu gani tena huchochea homoni za mwili kabla ya mechi?

Matangazo, matangazo mengi na majigambo kabla ya mechi huamsha hamasa kubwa kupita kawaida kwa wachezaji na mashabiki. Kwa sababu ya hamasa hiyo huleta athari mbaya hasa timu inapofungwa au kupoteza mechi.

picture.jpg

#Picha | Medicinenet.

Ni magonjwa gani mengine hutokea kwa sababu ya kufungwa katika mechi.

Uchunguzi wa mechi mubashara( live) - Scottish live match in Scottish spectators), uchunguzi wa New Zealand na uchunguzi uliofanyika Japan ulionyesha pia shida ya kupumua, kifua kuuma na matatizo ya moyo ni magonjwa hutokea kwa mashabiki wa mpira.

Athari za kisaikolojia kwa mashabiki hasa timu inapopoteza au kufungwa magoli.

Mashabiki kipenzi hupata athari nyingi na kupita vipindi vigumu baada ya timu yao kufungwa.

Hizi ni athari zinazotokea baada ya timu kufungwa; Migogoro binafsi, Huzuni, Msongo wa mawazo, matusi, kujihukumu, kuwalaumi viongozi wa timu au wachezaji, kuhama timu, kuanza tabia ya kula vyakula visivyo na faida (junk food). Kupigana - yaani mashabiki kipigana wao Kwa wao. Kupiga viti uwanjani au nyumbani na kuopoga watu (mtu anakuwa ni wa kujitenga).


18-57-41-images.jpg

#Picha | East Africa Television.

Je unaweza kufanya nini Ili ushabiki wako usiathiri afya yako?

Tambua ni mchezo tu.
Hii maana yake ni kwamba usikuze mchezo huo sana akilini mwako kiwango ambacho unakuwa na uhasama na wengine kwa sababu tu umefungwa magoli mengi_ Hapana.

Kubali matokeo. Kukubali ya kuwa umeshindwa, kwa kufanya hivyo unaupa moyo wako kupumzika, akili zako zikipumzika na mwili unatulia. Usisema, “ aaah hapana.... nyie hamna uwezo, leo tu mmebahatisha.... hamjatushinda bwana n.k”_Hapana. Kubali ya kwamba, ndio mmetufunga magoli matatu mmeshinda, tusubiri mechi nyingine.

Jichanganye katika jamii. Watu ni dawa, lakini kuishi maisha ya upweke yanaweza kuongeza msongo wa mawazo na kuathiri Afya yako.

Epuka makundi ya wapinzani: Kaa mbali na wapinzani wako kwa sababu maneno ya hasira yanaongeza hatari ya homoni ya cortisol ambayo hiyo huathiri mwili wako. Kaa mbali nao ikiwezekana mpaka muda upite kama unaona hauna uwezo wa kuhimili maneno yao.

Eleza hali yako kwa wengine: Hii maana yake ni kwamba usikae kimya ile hali huku wewe unapata huzuni na msongo wa mawazo. Mara unapomweleza mwingine atakushauri na utajisikia vizuri.

Wasiliana na daktari wako: Kwanza; Kama una tatizo la shinikizo la juu la damu. Pili; kama unamafuta mengi mabaya mwilini, hakikisha uko kwenye dawa. Tatu; Kama wewe huwa unasisimuka sana wakati wa mashindano wasiliana naye kabla ya mchezo.
Nne; Baada ya mashindano kama utaona hali inazidi kuwa mbaya wasiliana na daktari wako ili kupata tiba sahihi.

KUMBUKA: Kama tayari una shida ya moyo hakikisha unawasiliana na daktari wako kabla ya kwenda kuangalia mechi ya mubashara (live) ili kupata ushauri wake.

Asante kwa kujifunza pamoja nami.

Hakikisha unanipigia kura kabla haujaondoka.
 
Back
Top Bottom