Mlenge
R I P
- Oct 31, 2006
- 2,125
- 2,291
Hudhaniwa na wengi kwamba Marekani hupenda sana vita, hasa kwa nchi zenye mafuta. Vita ni moja ya mbinu za kupata uwanja wa kujigemea mafuta wapendavyo. Dhana hii inaweza kuwa yakinzana na uhalisia. Marekani haipendi vita, ndio maana wanajitahidi sana uwanja wa vita uwe ugenini.
Marekani inalinda sarafu yake ya dola (USD). Hicho ndicho kipaumbele nambari moja. Pana mstari fulani nchi isiyo na nguvu sana ikiuvuka, Marekani huingia vitani. Saddam na Ghadafi ni mfano mmojawapo. Wote hawa waliamua kuitosa sarafu ya Marekani na kuamua kutafuta mbadala.
Chukulia wewe umetengeneza printa. Wino na karatasi za kumwaga unazo. Ukiprinti vikaratasi ni kama huna gharama yoyote. Lakini vikaratasi unavyoprinti ndio vinatumika na watu wote kama njia ya kubadilishana mali zao.
Yaani mtu kalima kapata magunia ya mahindi. Anabadilishana mahindi na mtu aliye na vikaratasi ulivyoprinti. Halafu mtu huyo anachukua vikaratasi hivyo anatumia kwenye mahitaji yake mengine. Ni hivyohivyo kwa kila mtu na kwa kila bidhaa. Siku ikitokea mkulima mmoja wa mahindi akaamua kuacha kutumia vikaratasi vyako, akaanza kutumia vikaratasi vya mwingine, na kana kwamba hiyo haitoshi, akaanza kushawishi na wengine, ukiwa na uwezo utaacha kumshughulikia? Watazamaji watadhani una shida ya mahindi ya huyo jamaa. Mahindi ya nini wakati ukiyahitaji tu unaprinti vikaratasi unawagawia wenye mahindi, wanakukabidhi matani ya mahindi?
Hitimisho: Marekani haipendi vita, ndio maana haitaki vita uwanja wa nyumbani. Marekani inapambana kuhakikisha sarafu yake ndio sarafu kinara kwenye miamala yote ya maana duniani.
Angalizo: Nazungumzia kiini cha vita; sizungumzii uhalali au la wa kuingia vitani.