Kwanini Marekani imewazidi Mexico kwa mbali sana tofauti na Ujerumani inavyotaka kulingana na Ufaransa ilhali hizo zote sio nchi za ndani ya Afrika?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania;

Kwanini Marekani imewazidi Mexico kwa mbali sana tofauti na Ujerumani inavyotaka kulingana na Ufaransa ilhali hizo zote sio nchi za ndani ya bara la Afrika?

sdsdffffffffffgfgfff.jpg


Je, ushahidi huu ni udhibitisho mwingine tena wa ule msemo/dhana maarufu ya kwamba kuishi karibu na mahakama sio kujua sheria kwa maana nchi ya Mexico ipo karibia kabisa na mahakama (Marekani) lakini bado sio wabobezi wa sheria (Global Influence) tofauti na Wafaransa wanavyojitahidi kutaka kulingana na Wajerumani.

Kwanini utofauti ni mkubwa hivi na hawa wote ni rangi nyeupe?

Kwa kipindi cha muda mrefu sana kumekuwapo na dhana sijui niseme ni kasumba ya kuamini kwamba ukikaa karibu na mzungu basi wewe ndio umefanikiwa. Tazama maendeleo ya nchi kama South Afrika ukilinganisha na jirani zao wa Msumbiji waliojawa na umasikini wa kutupwa.

Asilimia kubwa ya watu wanaamini ya kwamba maendeleo yale ya vitu yametokana na wao kukumbatia wazungu waliokuwapo nchi ile enzi na enzi pamoja na uamuzi wa mzee Madiba wa kutotaka kuwafukuza punde baada ya kumalizika kwa utawala wa kikaburu (Apatheid Regime)

images (14).jpg


Tukirudi hapa nyumbani kwetu Tanzania, moja kati ya sera za baba wa taifa Mwalimu Julius Nyarere ambazo baadhi ya wanazuoni wamekuwa wakizikosoa kwa nguvu zote na kudai ya kwamba ndio chanzo kikuu cha Tanzania kutokuwa na uchumi kama wa South Afrika ni ile ya kuwafukuza wazungu nikiwa na maana kwamba aliwafukuza kwa kufuta lugha ya kiingereza kama medium of instruction katika taasisi zetu za elimu ya msingi pamoja na utaifishwaji wa mali zao.

Achilia mbali sera za Mwalimu Nyerere pamoja na Makaburu wa South Afrika, bali turudi huku uswahilini kwetu tunapokaa. Just imagine leo hii umepita ukiongozana na mzungu barabarani huku uswahilini tunapokaa, unafikiri watu watasemaje. Lazima viji maneno vitambae utasikia daaaah yule jamaa si ndio Infantry Soldier.

Yule si ndio hapa juzi alikuwa analialia eti ameangusha pesa yake 300,000/= ya rambirambi ila leo anaongozana na wazungu hakika ametoboa kimaisha. Kwanini hii dhana ya mafanikio huletwa ukaapo na mzungu imekuwa si halisi kwa Mexico?

SWALI LA KIZUSHI: Je, ni mara ngapi uliwahi kukataa kupiga picha na mzungu? (Kuwa Mkweli)

Si unajua kule america wale black huku tungewaita white. Kama obama anaitwa black but huku kwetu tungemwita obama white.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Hispanics hamna tofauti na sie wengine

Mi naona sababu kubwa kwa nini Mexico Kama vile ilivyokuwa kwa nchi zetu kuwa nyuma licha ya kupakana na nchi tajiri duniani ni kukosa ustaarabu, corruption ya viongozi Kama sio mfumo unaoendesha nchi



Anyway hawako mbali sana na kuingia status ya dunia ya kwanza sababu Mexico GDP per capita ni zaidi ya USD 10000

Kadiri muda utavyoenda kipato kinavyokuwa watafika tu
 
Kuna rais mmoja wa Mexico mwanzoni mwa karne ya 20 akiitwa Porfirio Díaz aliwahi kusema "Poor Mexico, so far from God and so close to the United States!"
Akimaanisha Mexico ilikuwa ikimtegemea mungu aliye mbali aisaidie ilihali Marekani yupo karibu na anaweza kutatua changamoto zake kama akimtumia.

Nadhani Mexico hawajaifanyia kazi kauli hii vya kutosha hata miaka 100 tangu itamkwe.
 
Hispanics hamna tofauti na sie wengine

Mi naona sababu kubwa kwa nini Mexico Kama vile ilivyokuwa kwa nchi zetu kuwa nyuma licha ya kupakana na nchi tajiri duniani ni kukosa ustaarabu, corruption ya viongozi Kama sio mfumo unaoendesha nchi



Anyway hawako mbali sana na kuingia status ya dunia ya kwanza sababu Mexico GDP per capita ni zaidi ya USD 10000

Kadiri muda utavyoenda kipato kinavyokuwa watafika tu
Ila kuna watoto wakali Mexico. Hao Hispanics Latinos mixture ya wahispania na natives Indians yani huo ukanda wote wa central America Honduras, Panama, Elsalvador, Costa Rica, Nicaragua ni hatarii signorita.

Wahamiaji kutoka uhispania waliwabaka sana natives Indians na kuzaa nao baadaye wakachanyikana ndio hao Latinos/hispanics

JESUS help us
 
Nadhani mexco walichelewa kujua nini cha kufanya wakabaki wanapambana na mabeberu ili wabaki wao masikini ndio kilicho waumiza kwa mda mrefu.

Ila siku za hivi karibuni wameanza kushirikiana na USA na kuwaona kama ma rafiki na sio mabeberu hivyo mexco umeanza kujua kwenye secta ya kilimo, mawasiliano na Teknolojia
 
Back
Top Bottom